Heshima Mzee:
Lakini hapa unachemsha. Watumishi wa serikali ambao nafasi zao sio za kisiasa hawatakiwi kuwapo kwenye mikutano ya vyama.
Kama sera za chama chenu ni za uchumi, mnaweza kufanya hivyo kwa kumwita waziri wa fedha na manaibu zake au kumwita waziri wa miundo mbiu za mikoa kwa sababu hao wanashikiria nafasi za kisiasa na ni wanachama wa CCM. Masuala ya ulinzi na usalama ni muhimu. Kwanini basi mkuu wa majeshi ya ulinzi au Inspector mkuu wa polisi asiende huko. Vilevile Tanzania ina matatizo ya njaa, kwani mabwana shamba hawapo kwenye kikao hicho? Wanasiasa ni lazima mkubali kuwa kazi zingine ni professions ambazo hazitakiwi kuingiliwa kisiasa.
..watu wa musoma wako tofauti kabisa.
Hawa watu wa Musoma walikuwa wanampinga hata Mwalimu uso kwa macho na Mwalimu alilijua hili.Sasa JK na Serikalo ndiyo haipendwi kabisa hapa mkoani ila wana wapambe na wanatumia mabavu ndiyo unaona CCM wapo lakini ukweli ni kwamba watu hawaitaki CCM hapa Musoma .
Killuminati,
Tatizo hapa ni watu kuwa na wasiwasi na kila jambo ambalo CCM wanafanya.
Idea yenyewe sio mbaya, hao NEC ndio wanapango mipango ambayo serikali ya CCM inatekeleza, kupigwa lecture na prof. Ndullu linaweza kuwa jambo zuri, of course kama wako tayari kusikiliza.
Hivyo hivyo hata CHADEMA au chama kingine wanaweza kumwita kwenye mkutano wao kama wanataka kujua hali ya uchumi na kumwuliza maswali juu ya mwenendo wa uchumi wetu.
Wenzetu walioendelea wana mikutano na gavana mingi tu kuanzia wasomi, wafanyabiashara, wabunge mpaka wanasiasa wengine.
Idea sio mbaya, labda tupinge kwasababu hatuamini CCM wataitumia vizuri hiyo
taarifa.
Labda sasa CHADEMA au chama kingine nao kama wanataka lecture ya prof. wafanye hivyo na kama atakataa bila sababu, hapo tunaweza kuifanya kuwa issue, vinginevyo tunachopinga ni kama CCM walivyopinga innovation ya Mbowe ya kukampeni kwa helikopta, baada ya muda na wao wakajiona wajinga na kuanza kutumia helikopta.
Mkuu Nyangumi,
Ninakuheshimu kuwa ni kichwa, Gavana wa BOT na waziri wa hazina ni watekelezaji wa sera za CCM on uchumi side, nashangaa sana kuwa ulikuwa hulijui hilo, maana ushindi wa CCM kwenye uchaguzi wa wabunge na rais, maana yake ni moja tu nayo ni CCM kuwa na mandate ya wananchi kutekeleza sera walizoziahidi kwenye kampeni, sasa sera hizo zitatekelezwa na nani? Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM, akiwatumia wasaidizi wake wanaotambulika kisheria, who are they? ni pamoja na waziri wa hazina pamoja gavana wa BOT, sera za CCM zinatengenezwa na nani NEC,
Sasa kweli unasema kumuita gavana na waziri wa hazina NEC, ambao ndio watengenezaji wa sera zetu za taifa ni uhuni na ukosefu wa akili? are you serious? Maana nina wasi wasi watu wenye akili nyingi wakiisoma hii topic watashindwa kuelewa exactly nani mwenye uhuni na ukosefu wa akili mkuu,
Halafu, hivi ni kweli ilibidi utumie haya maneno very low kuwa-describe NEC ambao wameamua kuwaita watekelezaji wa sera zao kwa taifa?
I am very dis-appointed mkuu!
Mtanzania,
Kama NEC igekuwa huru a Bunge ningeelewa nia ya kuitwa Ndulu huku Butiama. Lakini baraza la mawaziri, karibu 60% ya wabunge wa CCM, wote hawa ni wanachama wa NEC na CC, hivyo suali ni kitu gani kipya atakachofundisha ambacho wao walipaswa kumhoji waziri wao wa fedha?
Mazingira ya Tanzania sasa hivi na hasa kutokana na Uhujumu wa EPA ambao unasadikika kuwa CCM ndiyo mvunaji mkubwa au mtuhumiwa wa uhujumu, unafanya kila mtu atilie mashaka mwaliko huu. Je Ndulu anaenda kufundwa, kunyamazishwa au kupewa mikakati mipya ya Saidia CCM ishinde 2010?
Ikiwa ni vigumu kwa Bunge kupata habari kamili za utendaji wa Serikali na mwelekeo sahihi wa uchumi, je ni vipi CCM iwe na nafasi ya Kwanza na si Bunge?
Naona watu mnatanguliza hasira badala ya kufikiri kwa makini.
Hivi CCM kama wanataka kumfunda Prof. Ndullu kweli wanahitaji kuitangazia dunia nzima? Si wangemwita tu Ikulu na kujaribu kumwambia wanachotaka? Labda kwa nyumbani ni kitu cha ajabu lakini katika mizunguko yangu ya maisha, sioni ajabu yoyote kwa gavana kuitwa kwenda kutoa lecture au semina kwenye chama cha siasa, jumuia za wasomi au hata jumuia za kibiashara.Binafsi sijui CCM wanataka kupata lecture kwenye nini lakini sioni kama jambo la ajabu. Ni afadhali wametutangazia wote na tumejua kuliko walivyokuwa wanamfuata Ballali kimya kimya.
NEC ndio watunzi wa sera ambazo serikali ya CCM inatekeleza, uchumi ndio nguzo kuu katika sera za nchi yoyote ile, kwahiyo kupigwa lecture huko kama kukitumiwa vizuri kunaweza kuwa na faida kwa nchi. Hata vyama vingine vinaweza kukutana na gavana. Bahati mbaya vyama vyetu karibu vyote, havina sera za kichumi na vyote vinatumia muda mwingi kwenye malumbano bnadala ya kusema watafanya nini kwenye utawala wao.
Rev. Kishoka,
Naona watu mnatanguliza hasira badala ya kufikiri kwa makini.
Hivi CCM kama wanataka kumfunda Prof. Ndullu kweli wanahitaji kuitangazia dunia nzima? Si wangemwita tu Ikulu na kujaribu kumwambia wanachotaka?
Labda kwa nyumbani ni kitu cha ajabu lakini katika mizunguko yangu ya maisha, sioni ajabu yoyote kwa gavana kuitwa kwenda kutoa lecture au semina kwenye chama cha siasa, jumuia za wasomi au hata jumuia za kibiashara.
Binafsi sijui CCM wanataka kupata lecture kwenye nini lakini sioni kama jambo la ajabu. Ni afadhali wametutangazia wote na tumejua kuliko walivyokuwa wanamfuata Ballali kimya kimya.
NEC ndio watunzi wa sera ambazo serikali ya CCM inatekeleza, uchumi ndio
nguzo kuu katika sera za nchi yoyote ile, kwahiyo kupigwa lecture huko kama kukitumiwa vizuri kunaweza kuwa na faida kwa nchi.
Hata vyama vingine vinaweza kukutana na gavana. Bahati mbaya vyama vyetu karibu vyote, havina sera za kichumi na vyote vinatumia muda mwingi kwenye malumbano bnadala ya kusema watafanya nini kwenye utawala wao.
Mkuu wangu, kwanza ninataka kuamini kuwa wewe ni mbongo mwenzangu, maana haiwezekani ukawa mbongo ukashindwa kujua kuwa kustaafu mapema kwa Mahita, ex-Police Chief, hoja ilianzia NEC na baadaye CC, kwamba Mbilinyi waziri wa zamani wa hazina hoja ya kumpuzisha ilianzia NEC, kwamba majuzi kujiuzulu kwa Lowassa na mawaziri watatu, hoja zimetokea NEC na CC, I mean kamati ya CCM ya ulinzi na usalama kazi yake ni nini? kamati ya uchumi ya CCM kazi yake ni nini?
Ni pamoja na kufuatilia ishus za uchumi za taifa, kukutana na gavana na waziri at their call, kwa hiyo kama kuna ishu wanatakiwa kuifikisha kwenye NEC, ni lazima wawaite waziri na gavana, ili kuwasilisha their side of the professional story inayowakilishwa na kamati kwa NEC, bunge hufanya hivyo pia kumbuka kuwa hiyo professional Nduulu ameipata baada ya kuchaguliwa na rais, ambaye ni mwenyekiti wa CCM, ambaye taifa tumempa nafasi kisheria kutekeleza sera za CCM, ikiwa ni pamoja na sekta ya uchumi,
Hivi kweli haya yanahitaji kuwa professor kuelewa, hivi mkuu kweli unaaamini kuwa mkuu wa majeshi na wa polisi sasa hivi hawako Butiama tayari!
Mkuu, Ndulu ni mtendaji wa sirikali, na si mtendaji wa CCM!
Mkuu Nyangumi,
Ninakuheshimu kuwa ni kichwa, Gavana wa BOT na waziri wa hazina ni watekelezaji wa sera za CCM on uchumi side, nashangaa sana kuwa ulikuwa hulijui hilo, maana ushindi wa CCM kwenye uchaguzi wa wabunge na rais, maana yake ni moja tu nayo ni CCM kuwa na mandate ya wananchi kutekeleza sera walizoziahidi kwenye kampeni, sasa sera hizo zitatekelezwa na nani? Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM, akiwatumia wasaidizi wake wanaotambulika kisheria, who are they? ni pamoja na waziri wa hazina pamoja gavana wa BOT, sera za CCM zinatengenezwa na nani NEC,
Sasa kweli unasema kumuita gavana na waziri wa hazina NEC, ambao ndio watengenezaji wa sera zetu za taifa ni uhuni na ukosefu wa akili? are you serious? Maana nina wasi wasi watu wenye akili nyingi wakiisoma hii topic watashindwa kuelewa exactly nani mwenye uhuni na ukosefu wa akili mkuu,
Halafu, hivi ni kweli ilibidi utumie haya maneno very low kuwa-describe NEC ambao wameamua kuwaita watekelezaji wa sera zao kwa taifa?
I am very dis-appointed mkuu!
Mkulu wangu Bubu,
CCM wangekuwa na nia mbaya naye, wasingesema kuwa wanaenda naye, wanayotaka kufanya naye huko sio lazima ingesubiri Butiama, halafu next time upinzani wakikutana mwiteni ni haki yenu kisheria kama mlikuwa hamjui, atakuja tu, akikataa then tutamkoma nyani hapa,
ila kwa sasa yeye kwenda huko NEC, kwa watengeneza sera zetu za taifa, ukweli ni kwamba hoja yenu ni hafifu kama hakuna kabisaa!
Wito kwa watanzania wenzangu,mimi nimejifunza somo kubwa sana kwa watu wa Musoma na hii ndio inatakiwa hadi pale 20010,CCM tuwalambishe mchanga kwanza ndio adabu itawasogea vinginevyo watatufanya malofa hadi siku ya mwisho.
Watu wa musoma nawapa BIG UP kubwa.