Kutoka CCM, heri ya sikukuu ya Pasaka

Kutoka CCM, heri ya sikukuu ya Pasaka

Baraka Mina

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2020
Posts
586
Reaction score
590
Habarini wanajamvi wenzangu, poleni na majukumu mbalimbali ya kujenga taifa.

Hakika tuendelee kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yetu na taifa letu, Mungu hatatuacha atazibariki kazi za mikono yetu. Leo baada ya majukumu nimepita kwenye mitandao ya kijamii na kukuta salamu hizi nikaone ni vema niwashirikishe watanzania wenzangu.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewatakia waumini wa dini ya Kikristo nchini pamoja na watanzania wote sherehe njema za pasaka.

Salamu hizo zimetumwa kwa watanzania kupitia kurasa na akaunti za Chama hicho Tawala na kikongwe nchini.
Ikumbukwe kwamba waumini wa dini ya Kikristo siku ya kesho jumapili (04/04/2021) wataadhimisha sikukuu ya Pasaka na siku ya jumatatu ni jumatatu ya Pasaka.

Katika salamu hizo, Chama Cha Mapinduzi kimeandika;
"Uongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wanawatakia watanzania wote sherehe njema za sikukuu ya Pasaka."

Pia kimeongeza na kuweka payana kuwa "Tuna Imani na Samia."

Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa wakipatana vema na wakipendana.

Nawatakia sherehe njema za sikukuu ya Pasaka.

IMG-20210403-WA0193.jpg
 
Attachments

  • VID-20210403-WA0145.mp4
    19.1 MB
Mbona hawajasema tuendelee kuomboleza kimya kimya wakati wa kusherekea?
 
Momba hawajasema tuendelee kuomboleza kimya kimya wakati wa kusherekea?
Maombolezo yanaendelea na leo ni siku ya 18. Kwa mujibu wa utaratibu maombolezo yalitangazwa kwa siku 21.

Na siku ya jana Chama kiliweka ujumbe huu.
"Duniani kote, sekta ya viwanda ndiyo mhimili mkuu wa kukuza uchumi, kupambana na umaskini pamoja na matatizo ya ajira."
Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
(Ufunguzi wa Bunge la 12 la Tanzania, 13 Novemba 2020.)

IMG-20210402-WA0120.jpg
 
Hatutaki unafiki si mmesema mnaomboleza hakuna sherehe ya pasaka.
 
Kuna vyama vimesahau kama tupo kipindi cha maombolezo
 
Hicho chama si ndio kimekataa...watu kusherehekea???
Hapana, sherehe za Pasaka zipo kama kawaida. Jeshi lieleza juu ya shamrashamra za matamasha.
Pia Chama Cha Mapinduzi hakijazuia. Taarifa ya Jeshi la Polisi siku ya jana ilifafanua vizuri.
Naomba ninukuu, sehemu ya taarifa iliyotolewa na David Misime -SACP, Msemaji wa Polisi.
“Jambo ambalo hatutegemei kuliona ni zile shamrashamra kubwa kama vile Matamasha na Makongamano ya Pasaka na kwa bahati nzuri wanaoyaandaa kila mwaka kwa utu wao wa Kitanzania, hekima na busara zao hatujasikia wakitangaza maandalizi ya Matamasha hayo.
Ibada za Sherehe za Pasaka kwenye Makanisa, Sherehe za Kifamilia, Hitma, Familia kuungana na kwenda kutembelea sehemu mbalimbali na kusherehekea Pasaka hakuna aliyekataza ili mradi unachofanya kinaendana na kufuata utu, busara, hekima, Sheria , kanuni na taratibu za Nchi."
 
Chama cha manunuzi gekul katambi waitara silinde moleli mdee na comp
 
Hatutaki unafiki si mmesema mnaomboleza hakuna sherehe ya pasaka.
Hapana, sherehe za Pasaka zipo kama kawaida. Taarifa ya Jeshi la Polisi siku ya jana ilifafanua vizuri.
Naomba ninukuu, sehemu ya taarifa iliyotolewa na David Misime -SACP, Msemaji wa Polisi.
“Jambo ambalo hatutegemei kuliona ni zile shamrashamra kubwa kama vile Matamasha na Makongamano ya Pasaka na kwa bahati nzuri wanaoyaandaa kila mwaka kwa utu wao wa Kitanzania, hekima na busara zao hatujasikia wakitangaza maandalizi ya Matamasha hayo.
Ibada za Sherehe za Pasaka kwenye Makanisa, Sherehe za Kifamilia, Hitma, Familia kuungana na kwenda kutembelea sehemu mbalimbali na kusherehekea Pasaka hakuna aliyekataza ili mradi unachofanya kinaendana na kufuata utu, busara, hekima, Sheria , kanuni na taratibu za Nchi."
 
Chama cha manunuzi gekul katambi waitara silinde moleli mdee na comp
Hakuna aliyenunuliwa. Viongozi hao walipaisha wazi na kuushuhudia umma sababu za msingi zenye kutosheleza akili na ufahamu kwa nini walijiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Fuatilia mahojiano yao utaona.
Tulijenge taifa letu.
 
Kwa sasa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameanza kuwashangaza.
Hawaamini, Rais anafanya kazi. Wanashangilia sana kazi njema inayofanyika baadaye wanasema ngoja tupinge. Wanashindwa kujua washike nini na waache nini.
Vyama vinatakiwa kupinga kwa hoja za msingi na zenye usahihi.
 
Umenena vyema
 
Ahsante sana yani hii sherehe jamani, huku kufa kule kufufuka.
 
Hakuna aliyenunuliwa. Viongozi hao walipaisha wazi na kuushuhudia umma sababu za msingi zenye kutosheleza akili na ufahamu kwa nini walijiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Fuatilia mahojiano yao utaona.
Tulijenge taifa letu.
Kawadanganye watoto wadogo wa kwanza waitara alipo lipwa kaenda kujenga tarime
 
Back
Top Bottom