Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Hivi yale mapapai niliyokula jana sijui itakuwaje ?
 
Chadema walitamani sana mambo mawili: 1. Kuwe na lockdown ili uchumi uyumbe wapate sababu ya kuikosoa serikali ya awamu ya tano. 2. Nyumba za ibada zifungwe ili watu wasimwombe Mungu na shetani apate mlango wa kuiharibu nchi yetu!
Sijui watu hawa wana ubia gani na shetani?
 
Hapo ndio tufungue macho! Nawaonea huruma waliojipeleka kupima huku wakiwa hawana dalili corona kisha wakaambiwa wana corona!
Hapa inamaanisha pia watu walioambiwa ni negative pia wanaweza wakawa positive?sasa hizi takwimu zinazotolewa sio sahihi ?ina maana inawezekana kukawa na wagonjwa wengi sana wa corona na ndio maana watu wengi sana wanazikwa usiku mpaka wizara ya Afya inasema watu wasizikwe usiku hapa wamekiri wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Business as usual as if the Late Hon Dr Mahiga was nobody to his cabinaet
 
Ujasiri tunaopewa ni mkubwa sana,ni kama ule wa Kinjekitile Ngwale kwa watu wake,lakini kama tukivuka salama,Magufuli atakuwa shujaa wa dunia. Huenda ndiye aliyenenwa na manabii. Tuwe na subira huku tukichukua tahadhari
 
Kwanza kabla hujaja kutoa maoni hapa nenda kamsikilize Rais kwanza wewe mwenyewe kwa masikio yako usisimuliwe na mtu.
Ninashaka walio wengi hawajamsikiliza Rais badala yake wanasoma nyuzi tu humu na ku comment na wengine wanasoma tu vichwa vya habari na ku comment bila hata kusoma Uzi wenyewe, hatimae wanajikuta waandika vitu vya ajabu.

Tangu hotuba ya Rais iishe mijadala imekuwa mingi kujadili kile alichokisema Rais huku ikionesha ni jinsi gani hatukumuelewa Rais.
Ukisoma kwa makini yanayo andikwa humu utakuta watu wana mlisha Rais maneno ambayo yeye hakuyasema.

Mfano, kuna watu wanasema mambo mengi kama

Biashara ya mbuzi choma, matunda n.k itaporomoka kwasababu Rais kasema vina corona.
Ajabu sana hii.!!

Mh Rais alichosema ni kwamba alikuwa na shaka na vipimo vinavyotumika kupima Corona, sasa katika kujipa uhakika na utendaji kazi wa vipimo hivyo na weledi wa wataalam wetu, wakaamua kupenyeza sample ambazo si za binadamu (lakini zenye majina ya binadamu) kwenye maabara ya taifa bila ya wataalam kujua na majibu yakaja kuwa vitu hivyo vina maambukizi ya corona.
Mafenesi,papai,oil, mbuzi, sungura,nanasi sasa hapa ndipo anaeleza shaka yake ama juu ya vipimo kuwa vinatoa majibu ya uongo, ama vipimo hivi vina maambukizi, ama vimewekewa wastani fulani kuwa kila vikipima baada ya Idadi fulani itaonyesha positive,mfano wakipima watu 20 mtu wa 21 lazima awe na maambukizi, ama kuna makosa yanafanyika kwenye upimaji, ama wataalum wetu hawajajua namna ya kutumia hivi vifaa.

Ametoa ushauri kuwa mataifa mengine pia wafanye huo uchunguzi wajiridhisha na hayo anayo yasema.

Lakini ajabu ni kwamba watu ama kwa kuto kuelewa ama kwa makusudi wanatoa taarifa tofauti kabisaa na alichosema Rais na mantiki ya uchunguzi alio ufanya.

Wengine wanahoji eti badala ya kupima watu yeye anapima mbuzi!!!

Sasa kama humu tunao jiita wasomi tumeshindwa kujua mantiki ya kauli ya Rais na uchunguzi wake je hao wengine wasio na Elimu kabisa itakuwaje??

Tutawapotosha watu wataacha kula mapapai kwa ujinga wetu tu na mihemko ya ovyo ovyo.
heti oil nayo ina corona!!!!

Lipi zuri sasa!? Kufanya uchunguzi kama huu au kukubali tu moja kwa moja na matokeo ya vipimo tuvavyoletewa?? Mnakujua viliko tengenezwa!?

Ukisoma sana maoni humu jukwaani utakuja kugundua kuwa hata Elimu tu ya namna sampuli za corona zinavyochukuliwa na jinsi zinavyopimwa walio wengi bado hawajui Elimu bado ndogo sana kwao.
Utakuta wengi wanadai ni damu ndio hutumika.

Hii tabia yetu ya kujifanya wajuaji wa mambo bila utafiti haita tusaidia wandugu.

Sasa tujiulize kosa la Rais ni lipi hasa, kufanya uchunguzi ama??

Tunaviaminije hivi vipimo kuwa viko sahihi na kumuona mjinga mwenzetu anae vifanyia uchunguzi??

Tushawahi kujiuliza ni kwanini India walivikataa hivi vifaa hasa vilivyotoka China??

Wapendwa Rais wetu ana hoja kubwa mno kwenye hili suala, tulijadili kwa jicho la tatu tusimpuuze hata kidogo kuna vitu vipo nyuma ya pazia tunatakiwa kuvijua na si kumpinga bila kutafakari anayo yasema.

Tuache kujadili kwa mihemko ya kisiasa humu.

Ila kama malengo ni kupata kiki za kisiasa tu humu basi sawa tuendelee tu kupotosha.
 
Mbaya zaidi hao hao Chadema ndo wamekuwa wa kwanza kulia lia kwa beberu wasamehewa madeni pamoja na uchumi kutoyumbishwa na corona.Yaani jamaa ni full comedy
 
Kwanza tageti ya Korona ni MAPAFU si vinginevyo, anamuingia binadamu kupitia kinywa, pua na macho pale atakapo JISHIKA na mikono iliyobeba virusi. Sasa tunda lililopasuliwa na kuchukuliwa sampuli amepenyeje huko.
Bado tuu hujaelewa! Labda Kwa viboko utaelewa, tunda limepasuliwa na robot au mikono ya mtu? Unajua Kwanini unatakiwa kunawa? Ni contamination mikononi sio? Sasa papai huwa wanatest vipi Kwa ndani?

Any away na vitasa vya milango nahisi unajua vurisi vvinafikaje huko, ni transmission through touching! Marekani familia iliteketea wakafanya research kuja kujua kumbe petts wote walikuwa contaminated, paka, kasuku, sakafu, Viatu, na ukuta wao! Huku mtu anasema anahisi sabotage wakati nahisi anajua kabisa jinsi corona virus wanavyokuwa transmitted!
 
Hv hizo sampuli za papai zilizopelekwa maabara zilikuwa kwenye damu au kwenye nini. Maana nadhani sampuli zote ziwe ni damu.

Yawezekana papai ikawa na damu pia.
Hawachukui sampuli kwenye damu! Wanachukua maji maji kwenye kuta za koo!
 
Hii nchi cjui Ina ikulu ngapi

stidy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…