Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kwa hiyo hapa tunakamuliwa pesa? Anyway Paschal anakebehi kusema ikulu ya chato,hayupo serious kwa namna wengi mnavyomchukulia,jifunzeni kumsoma vizuri
Hapo lazima serikali imeilipa familia ya Magufuli. 😂😂😂
 
NITATUMA NDEGE MADAGASCAR KULETA DAWA INAYOTAJWA KUTIBU CORONA-RAIS JOHN MAGUFULI.

Leo 13:15pm 03/05/2020

Kurunzi langu leo limeidaka hotuba ya Mh Rais John Pombe Magufuli wakati akimuapisha Mh Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria,

Tukiendelea kufuata haya tunayoelekezwa na Wataalam wetu wa Afya,

1.Serikali imesema epuka mkusanyiko
2. Fanya social distancing(kaa mita moja au mbili unapoongea na mwenzako)
3. Vaa barakoa
4. Nawa mikono na maji tiririka na sabuni kila wakati
5. Tumia sanitizer
6. Epuka safari zisizo za lazima
7. Muombe MUNGU wako
8. Chapa kazi ili uishi,usife njaa
9.Jifukize

Huku tukiendelea na utaratibu wa Wiki ya Nyungu,tukijifukiza utaratibu ambao upo tangu na tangu kwenye makabila mbalimbali, weka sufuria au chungu chako jikoni, washa jiko, maji yachemke, weka majani ya mti unayoyajua wewe yalete harufu nzuri,yasiwe mengi sana,jifunike na blanketi au shuka, kaa dakika tano au kumi ukivuta ule mvuke taratibu kwa kutumia pua na mdogo,toka jasho kweli kweli hapo utakuwa umekiua kirusi,

Mh Rais John Magufuli yuko tayari kutuma ndege kwenda Madagascar kuleta dawa inayotajwa kutibu virusi vya korona, hapa anamanisha yuko tayari kufanya chochote chema kwa Wananchi wake,hii ni habari njema sana,sio Mh Mbowe aliyesema tutume Ndege yetu iende China kufuata barakoa,

Ndugu zangu kama mnamfuatilia habari,Nchi nyingi kama Marekani, Uingereza,Canada wamelalamika baadhi ya vifaa kama barakoa fake pamoja na vipimo kutoka China vinatoa false positive na false negative,Lakini Mh Mbowe alisema tutume ndege iende huko kuchukua barakoa,

Hiki kinachotokea leo kwenye maabara zetu za fenesi,kwale,mbuzi na papai kukutwa na corona ni hatua za kuthibitisha kwamba vitu tunavyoletewa labda vina virusi vya corona au sampuli za kuchanganyia zina virusi,

Lazima kuchukua hatua hata kwenye dawa yoyote itakayoingia kwenye bohari yetu ya dawa ya Taifa,maana hakuna mtu nje ya Tanzania anaetutakia mema kwa kutumia Watanzania wachache wasio Waaminifu.

Mh Rais John Magufuli ametumia weledi wake wa Sayansi kuonyesha dhahiri udhaifu wa baadhi ya wataalamu katika maabara kwa kushindwa kutoa majibu sahihi ya sampuli wanazopelekewa na badala yake amegundua mpaka papai,ndege aina ya Kwale,mbuzi nao wana korona , hapa anamanisha sio kila mtu anayefariki ni corona na sio kila sampuli inayopimwa ni kweli corona,

Kwa kifupi,Hotuba ya Mh Rais akiongelea Mapambano ya corona imeshiba sawasawa,yenye kutia moyo,yenye mengi yenye weledi na intelijensia, nimemsikiliza mwanzo hadi mwisho, kuna mengi ya kujifunza kwenye ile hotuba, kutokurupuka kutumia akili na tahadhari zitolewazo na Wizara ya Afya.

Katika hotuba yake Mh Rais ameonesha kusikitishwa na jinsi watu wanaofariki na corona wanavyoshughulikiwa akitolea mfano tukio la Marehemu Mkuu wa Wilaya,Dc Evod Mmanda,

Mh Rais ameshangaa kwa nini hakupelekwa kwao Moshi,akitolea mfano wahudumu wa wagonjwa wa corona wanavaa PPE yaani mavazi rasmi ya kujikinga na corona,

Kwa nini hawakumvalisha Marehemu mavazi hayo na kuvalisha watu watakampeleka Marehemu kuzimwa nyumbani kwao Mkoani Moshi!

Hapa anaonesha kushangazwa hata wananchi wanavyofanyiwa kwa wapendwa wao wanaozikwa wasipopataka.

Nimemsoma Rais John Magufuli na kutambua kuwa ni mtu mwenye huruma sana hata kuogopa damu ya mtu,Mh Rais Magufuli ana hofu ya Mungu sana,

Rais John Magufuli ana imani ya kuweza kuamisha mlima, anamuamini Mungu sana, hawezi kumaliza hotuba yake bila kutaja neno la Mungu,na anawapenda sana Watumishi wa Mungu wa imani zote na amekuwa akiwashirikisha kila jambo linalohusu Taifa la Tanzania,

Katika kila vita basi lazima kwanza uishinde kwenye imani baada ya hapo ndio utaishinda katika ulimwengu wa kawaida, Rejea Daudi na Goliath,

Ukirejea Musa na Farao,Waisrael walivyofika Bahari ya Shamu na hakuna njia, Mungu alimuuliza una nini mkononi,Musa akajibu,Nina fimbo,Mungu akamwambia piga bahari itagawanyika nanyi mtapita hapo,hili ni zao la imani,usipokuwa na imani utabisha na utakufa,

Mungu alimwambia Baba yetu Ibrahim,"Hata akiwepo mtu mmoja mcha Mungu katika nchi ya Sodoma na Gomola basi sitaichoma moto"

Mwenyezi Mungu ni suala la imani na itakusaidia kupitia imani,Niwaambie ndugu zangu Watanzania,Isssue ya imani na kusali,acha kila mtu afanye sawa sawa na imani kwa Mungu Mwenyezi,

Rejea Shadrack,Meshack na Abelinego alitupwa kwenye moto kwa kukataa kuabudu sanamu lakini baada ya kutupwa kwenye moto walionekana wapo sita badala ya watatu,watu walianza kupiga Kelele baada ya kuona moto hauwaunguzi,walikuwa na imani kwa Mwenyezi Mungu nae akawatuma Malaika watatu wawalinde wasiungue na moto,

Rejea Daniel kwenye biblia alitupwa kwenye shimo lenye Simba wakali lakini Simba walimlinda badala ya kumla,Simba walimfanya rafiki yao,hii ni pale tu utakapokuwa na imani kubwa kwa Mwenyezi Mungu.

Wapo watu wanatembea na hawakanyagi chini,lakini wewe ukiwaangalia utaona wanakanyaga chini,

Watu awa ambao ni kama terrestrial wao kiuhalisia "nothing can touch them" for they are not of this World,

Sasa unapobishana na mtu ambaye ni mwamini kwa maana ya believer, you should be very careful,For it takes the level of faith you have plus your relationship with God almighty.

Rais John Magufuli ni mtu mwenye huruma sana, ni Protocol za taasisi ya Urais na protokali na majukumu ya Walinzi na Wasaidizi wake tu ndio zinambana ila kama sio hizo basi bajeti yake na ya Ikulu ingeishia kutoa misaada kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu maana anaweza akatoa msaada hata senti yake ya mwisho ya kula,

Tumeona katika ziara zake kabla ya corona akiwa anapita kugawa misaada pamoja na kutuma wasaidizi wake kutoa misaada kwa watu mbalimbali!

Wasaidizi wake wanambana kwa sababu wanajua udhaifu wake kuwa ana huruma sana na akionana na watu wenye shida ni lazima awasaidie kabla hajaendelea mbele na Safari yake,

Rais John Magufuli ni mtu mwenye kusamehe na kusahau, si wengi ambao ukiwakosea wanaweza kusahau labda wakusamehe tu lakini sio kusahau, yeye akishakusamehe anasahau na anakuamini tena kama mwanzo, mfano mzuri ni Mwigulu,Nape, January,na wengine wengi!

Rais John Magufuli ni mtu anayependa maendeleo yenye matokeo si maendeleo ya Kitakwimu ndio maana ukitembea Tanzania sasa hivi utatambua kuwa kuna mambo mengi yanafanyika, utakiri kuwa Serikali ipo kazini!

Nashindwa kumuelezea zaidi lakini itoshe tu kusema kuwa ni mtu mwenye kariba ya kipekee sana!na kwa hakika tumepata Rais mwema sana mwenye mapenzi ya dhati kwa Taifa lake la Tanzania,Mwenyezi Mungu ambariki sana,

Baada ya kusikiliza kwa makini hotuba ya Rais Magufuli nimefarijika sana, bado tunaye rubani imara na mwenye ueledi mkubwa bila kusahau ucha Mungu wake, ingawa pia nimegundua kuwa bado tunayo safari ndefu katika kuweka sawa baadhi ya mifumo yetu kuelekea katika ndoto ya kuwa na Tanzania tunayoitaka.

Hotuba muhimu iliyokuja kwa wakati muhimu kwa jambo muhimu, Hotuba ambayo imeleta matumaini kwa waliokufa moyo ktk kipindi hiki. Kura yangu haikupotea bure, hii ndio thamani ya kura yangu. Mungu mlinde, mpiganie, muongoze na kumtunza Rais wetu, kipenzi chetu John Pombe Joseph Magufuli,

Nitoe rai kwa ndugu zetu wa Madagascar kama wanataka kuisaidia Africa mara moja wamruhusu huyu *Dr. Jérôme Munyangi Wa Nkola* mgunduzi wa dawa ya corona ya Madagascar afanye workshop na wataalam wa Utafiti kama yeye Rais wa Madagascar alivyohutubia Marais wa Afrika,

Aeleze Wataalam wa Utafiti waingie maabara wa Afya wa Afrika njia ya kuchanganya hayo majani ya *Tetradenia riparia* ambayo yapo Afrika nzima na yamekuwa yakitumia kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo changamoto za mafua makali na upumuaji.

Hii habari kila mmoja kuagiza Madagascar wakati majani yapo Afrika nzima itafanya hitaji ama demand kuwa kubwa >kulinganisha na upatikanaji kwa maana ya Supply,

Hili lisijekutupeleka mwisho kwa waafrika wengi wa kawaida kukosa uwezo wa kununua na kutumia lakini utaalam jinsi ya kuichanganya ukiwekwa wazi utawasaidia waafrika wengi sana kokote walipo sababu majani haya yapo kote Afrika,

Kule Rwanda wanaita *_Umuravumba_* wanaitumia kutibu magonjwa mbalimbali miaka mingi yakiwemo yanayohusiana na mafua, homa kali..

Mti huo kama nilisikia vizuri kwa kiingereza unaitwa Tetradenia riparia,ambao kwa kiluguru ni mti wa chango kwa watoto,kule vunjo wanauita iyombo, kibosho wanaita ikingi,Machame ikingili,Wapare mrumbavasi, kimasai olmakingi,kihaya kashwagara,tunahitaji Dr Jerome ahutubie wataalam barani Afrika na watengeneze dawa hiyo,

Tatizo letu Afrika tulijikita kuepuka maambukizi tu huku tukisubiria Ulaya,Marekani,Western Countries watutafutie dawa.

Wakati hao western countries hawana mitishamba ya kutosha huko kwao kufanya Utafiti hivyo wanakuja huku kwetu Afrika ndio wanafanya Utafiti kisha ndio wanatupa dawa wakati dawa hizo kama hii imekuwa ikitumiwa miaka mingi pamoja na kinga mbalimbali ikiwemo kujifukiza,

Ahsante Rais John Magufuli,kwa hotuba yenye kutuma nguvu katika Mapambano ya corona,hotuba yenye kutia moyo,yenye mengi yenye weledi na intelijensia, nimekusikiliza mwanzo hadi mwisho, nimepata mengi ya kujifunza kwenye hotuba,kama kutokurupuka,kutumia akili na tahadhari zitolewazo na Wizara ya Afya.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
 
Angetuambia kwanza kwenye hivyo hivyo vifaa kwanini kuna watu wamekutwa positive na wengine negative? kwanini wote wasiwe positive? Majuzi tu waziri Ummy kasema watu zaidi ya 600 wameruhusiwa kutoka karantini baada ya kupimwa negative.

Anataka tumuamini yeye kuzidi maabara je yeye anawaamini vipi aliowatuma? je ni kweli ana uhakika vitu vyote vilivyopimwa viko positive wakati katumia neno baadhi? Rais anayependa kulalamika lalamika baada ya kuchukua hatua nani achukue hatua?

Vitu vingine tusipoteze muda rais anapenda kuambiwa anachotaka kusikia ndio maana anaowatuma wanamlisha pipi na kukaa pembeni wanamchora tu kama walivyofanya kwenye makinikia tri200+ na kwenye korosho kuleta kampuni hewa ya wakenya.
 
Kwa ninavyofahamu mimi machine mpya kabla haijaanza kutumika kupima wagonjwa hufanyiwa VALIDATION, hii hufanywa kwa kutumia known positive samples, na known negative samples.
Positive zinatakiwa ziwe positive na Negative ziwe negative. Hii ina-prove sensitivity na specificity ya machine husika.

Pia quality control zitoe results kama zinavyopaswa kutoa, kuna random error na specific errors kwenye machines na hata chemical reagents na pia kuna human errors hivyo vyote vinatakiwa kuwa vineangaliwa kabla human testing hazijafanyika.
Kama wao walipewa machines na wakaanza kupima human tests basi walichemka.
Science ina taratibu zake na zinapaswa kufuatwa, kama makosa yapo yarekebishwe siyo kudhalilisha wataalam wake hadharani.
 
Umeenda mbali sana rafiki. Maiga was no more a threat to even his beautiful wife. He was toothless. Fitina ya nini Sasa? Ni sawa na Mrema au Cheyo wa Leo. Hizo condom zimetepeta ndugu.
You only know too little........Yule ni mtu nyeti sn amehudumu awamu zote.......he has a lot to be a huge threat to any one......Usijidanganye mkuu hizi ni sirikali tu za dunia
 
Jiulize na wewe pia mana nanasi limekutwa positive pia kumbuka.
Basi tusiegemee upande mmoja,tujue kwamba kumbe waliopimwa wakakutwa hawana na walioambiwa wamepona na kuruhusiwa inawezekana hawajapona,na ili kwenda mbele zaidi ni kwamba takwimu zote walizokuwa wanatupa waziri mkuu na waziri wa afya ni batili na wao inabidi wajitafakari ikiwezekana wajiuzulu kwa kutoa takwimu ambazo haziaminiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikia NIMR wametoa michanganyiko aina 3 ya nyungu, mbona hatuipati humu, hebu tupieni bhana kabla hatujasukutua hiyo ya kutoka madagascar...
 
Na Nani kakuambia kuwa Rais wetu hafanyi kazi? Kutoa maelekezo siyo kazi? Kuteua mawaziri siyo kazi? Kuapisha waziri siyo kazi? Hata
kama haumpendi lakini macho unayo na masikio unayo! Unamwona na kumsikia akifanya kazi!
 
Time will tell,
Tanzania ikiangamia kama marekani kwa vifo na maambukizi,ndo tutajua nani juha na shetani na nani mwerevu na Malaika.
Ombeni hilo lisitokee hapa kwetu,lakini naona kama itakuwa muujiza.
Amen
 
Hivi kumbe Chato kuna Ikulu? Nimeuliza Kuna Ikulu??
Kweni hujui kua Chato ni sehemu ya mkoa wa Geita,kuna mkoa usuokua na Ikulu?

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…