Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kama korona inahusishwa/ imetokana na popo, hao wanyama anaowataja inashangaza nini kama wakikutwa nayo.
La kujiuliza anaijua korona, jinsi inavyoambukizwa nk.?

Kwa sababu korona ukutani ipo, juu ya meza na viti ipo, kwenye mabasi na vya kufunguliwa milango ipo, ndio maana inashauriwa vipulizwe madawa na kufutwa, ndio maana inashauriwa watu kunawa mikono. Ambacho haelewi ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inshort mzee anakataa uwepo wa Corona Tanzania. Majibu yaliotolewa before ni ya uongo. Maabara ya taifa inatumika na mabeberu. Hivyo watu wasiwe na hofu wachape kazi!

Sent From Galaxy S20 Ultra
 
MWIGULU AZIA TOSAMAGANGA NDUGU WANANUN'GUNIKA ,HAWANA IMANI KUWA NDUGU YAO KAFA KWA CONVID19....WAZEE WANATAKA KUFANYA TAMBIKO ....
MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI PEKE YAKE ....WALIOENDA KUMCHUKUA AKAFIKA HOSPITALI AKIWA KAFARIKI USIKU HUO NI KINA NANI ????
 
Kama Leo umeona uwamuzi alio ufanya waziri wa afya utakua umeamini nilicho kwambia kwa kauli ya raisi kuwa Hadi papai kukutwa na virusi vya corona

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Nasikitika sana kwa kumpoteza Waziri wetu mpendwa wa Katiba na Sheria aliyepita, Mungu amrehemu. Still, nina faraja pia kwamba Mwigulu amerudi kazini tena, I really wanted this man back into the cabinet! Nafurahi kumuona amerudi kwa sababu mamlaka ya uteuzi ilikuwa na uwezo wa kuchukua mtu mwingine tofauti na yeye, lakini bahati hiyo imeangukia kwake tena. Hongera zake Mh. Waziri, kama Simbachawene tu vile, niliyasema humu juzi nikimuusia mtu alikuwa anajaribu kumchafua Mwigulu
 
Ukiachana na mapapai yaliyopimwa, Fenesi na Oil chafu Kuna Jambo kubwa Rais kaliongea hapa. Nanukuu...

"Nchi yetu inawaajiri kama Walimu, lakini tumeendelea kulipa mishahara bila hata wao kufundisha, zipo nchi zimeshindwa kulipa, niwathibitishie Walimu tutaendelea mpaka Shule zitakapofunguliwa na wafanyakazi wengine tutaendelea kuwalipa" - Rais John Magufuli.

Nchi ambazo zimeshaanza kukata mishahara ya wafanyakazi wake wa umma ni Uingereza wao wanalipwa asilimia 80 tu, Denmark wanalipa asilimia 75, Rwanda Pilots wamepunguzwa kazi na waliobakia Nusu mshahara umeondoka. South Korea wanalipa asilimia 70 tu ya mshahara.

Katika hili tunamoongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Share na waalimu wengine hili Jambo linawahusu.

 
Kwani hapa kwenu kakorona kameshaleta athari zozote za kiuchumi pia?. Si watu wanaendelea tu kuchapa kazi! Tena wengine wanachapia kwenye makazi yao watakakozikwa! Ofisi haitoshi hadi kazi zimehamia maskani.

Kama kweli kakorona kana kameathiri kaisi Cha kumsifia jamaa, leo idadi halisi ni ngapi, ukiondoa Ile ya mapapai, mafenesi na Mbuzi?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
hizo nchi ulizotaja hata wakupunguza 50 percent ya mishahara ya Walimu wao bado sio sawa na ya Walimu wa Bongo
 
NAKUMBUKA ROSE MUHANDO MUIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI...KUNA WIMBO MMOJA ALIWAHI KUIMBA KWAMBA UTAWABEBA KWA MBELEKO MGONGONI LAKINI WATACHANA MBELEKO...WANAZINGUA. TENDA WEMA SEPA USISUBIRI MTU AKUSIFU.....WEWE FANYA KWA WEMA TU
 
Nyie watu muwe mnaelewa kinachoongolewa kabla hamjakurupuka kuleta jamvini! Si Uingereza wala Denmark waliopunguza mishahara kwa wafanyakazi wake!

Uingereza kwa mfano, hiyo 80% sio kwamba imepunguza mishahara ya watumishi wa umma bali inalipa wafanyakazi wa sekta binafsi ambao COVID-19 imesababisha wao kukosa kazi za ujira!

Tuchukue Tanzania kwa mfano! Nasikia kuna shule binafsi zimeacha kulipa mishahara baada ya kufungwa mashule. Katka mazingira kama hayo, ndipo serikali ya UK inalipa 80% hao wafanyakazi! Na hii inatumika sana kwa wale wafanyakazi wanaolipwa kwa masaa!

Kutokana na lockdown, hawa wafanyakazi hawaendi makazini, na kwahiyo NO PAY!

Kwa suala la Denmark, soma mwenyewe hapa:-
Denmark will compensate as much as 75% of the wages for some private sector employees who face losing their jobs as the economy slows down due to the spread of the coronavirus.
Sasa unaamini mfano wako wa Magu unaendana na hao?! Huyo Magu analipa mishahara kwa kampuni ipi binafsi?!

Mkiambiwa Magufuli muongo, mnakataa!!
 
Naunga mkono hoja
 
Kwa hiyo ukiwafungia watu jioni saa 12 jioni Hadi saa 11 alfajiri, ndio inatosha kudumaza Uchumi? Vingine ni visingizio tu vya serikali
 
Wadanganye wasiofuatilia vyombo vya habari,Rwandair Senior Employees ambao wanalipwa mpk $13,000/month wanapunguziwa mshahara kwa 65% na wafanyakazi wa chini watapunguziwa salary kwa 8%.

Shule zote Rwanda zitafunguliwa Sept. mwaka huu na walimu wote wameambiwa wataendelea kulipwa mshahara wote kama kawaida mpk muda huo,walimu wa Private Schools wameambiwa kuna Stimulus Package inapelekwa huko Private Sector so watalipwa at least nusu ya salary yao.
 
Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

Powa
 
Dah!!! tumetoka mbali kumb alishawahi kuvaa nguo aina ya shift!!!
 
Wanabodi,
leo ni siku ya kimataifa ya kuadhimisha siku ya uhuru wa habari, huku Tanzania tukiwa kwenye hii vita ya kimataifa ya kupambana na janga la Corona
P
==========
View attachment 1438587
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…