Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Vyama vyote haviwapi nafasi vijana wagombea wa CUF ni Maalim Seif na Lipumba,ukija CHADEMA ni Dr Slaa hawa wote wameshafikisha miaka 60.Bado mfumo wa vyama vya siasa za Tanzania hauwapi nafasi vijana kugombea nafasi nyeti

Nadhani si Tanzania tu hata nchi zilizoendelea,kama ikitokea inakuwa Mara chache siyo kwamba wame set the standard,angalia akina Angela Merkel
 
Kakodi mengi sana kwa kweli naona yamejaa hapa UDOM na wanafunzi wanazidi kumiminika kuingia kwenye gari.

Nchi hii ni shidaaaaa!!!!!

nao wanahaki ya kusikiliza. Alichofanya ni kufacilitate tu watu wafike. Hakuna aliyelazimishwa..
 
Heshima iwe kwenu wadau.

Baada ya kumsikiliza mtangaza nia namba 3 kutoka CCM ndugu Mwigulu Nchemba nimeingiwa na wasiwasi kidogo.

Kwa wale waliofuatilia na kumsikiliza mh. naibu waziri mtagundua kuwa Mwigulu alikuwa anaongea kama vile yeye si sehemu ya serikali.

Lakini cha ajabu zaidi mtakumbuka kuwa Hoja alizokuwa anaziongelea leo ni zile zile zilizokuwa zikiongelewa na wapinzani bungeni na yeye kuamka kuzipinga kwa kuwakejeli.

Kwa lugha nyepesi tunaweza sema kuwa Mwigulu katumia hoja za wapinzani kujinadi wakati ndye aliyekuwa mstari wa mbele kuzicrash hadi akasifiwa na Mwenyekiti wa chama na kupewa unaibu katibu mkuu bara pamoja na unaibu waziri kwa hiyo kazi.

Kwa lugha yepesi Mwigulu Nchemba tunaweza kumuita Chichidodo (Ndege mnafiki anayechukia kinyesi wakati chakula chake kinatokana na kinyesi)

Na hapa ndipo ninapopata wasiwasi kujua hasa nimwamini Mwigulu Nchemba yupi?!

1) Yule aliyekuwa anazipinga hoja za wapinzani?!

Au

2) Huyu aliyetumia hoja za wapinzani kutangaza nia?!
Mwigulu si ndie aliechana nakala ya budget ya waziri kivuli wa fedha bungeni!kwamba haina kitu kinachoweza tekelezeka?Lakini leo hii katumia maneno yaleyale yaliokuwa kwenye hotuba ile kwamba ndio vipaumbele vyake?Wonders shall never end in TZ wacha movie iendelee...
 
Kwa hiyo kila jema likiongelewa na CCM ni idea ya upinzani?

Mwigulu ni jembe na ni kiboko ya upinzani, lazima mpanick..

Hufuatilii Siasa Za Nchini Mkuu. Mwigulu Leo Alikuwa UKAWA kwa hotuba yake. Amerudia Yaleyale Yanayosemwa Na Wapinzani, Hasa Katika Bunge Hili La Bajeti.
 
sawa kaka. unajua nimekulia arusha na sifa za huyo baba nilikuwa nikizisikia nikiwa mdogo kuwa "...mtoto wa nyerere mlevi sana.....hajiheshimu ...hapendezi kuitwa mtoto wa JK..." lakini kipindi kile akagombea kwa tiketi ya nccr akapata kwa sababu aligombea kwa chama cha jembe la wakati huo - mrema. baada ya nccr kupoteza umaarufu na yeye akapotea kwenye masikio yangu. wenzie kama kina mbatia baada ya kupoteza ubunge kutokana na kudhoofika kwa chama bado waliendelea kuwa active mpaka leo wapo na legacy yao inaonekana. Sasa huyu makongoro ananitia shaka kidogo. Anajitokeza wakati wa mgao tu? uongozi wa mwigulu niliuona toka tukiwa chuo ila hakuwa maarufu kama kina zitto na msando, ila nilipomuona anapanda kisiasa ndo nikasema kumbe yule kaka alikuwa serious na siasa??

Mwigulu ana faida ya kutokuwa kwenye uongozi kwa muda mrefu kwa hiyo nguo yake itakuwa na matobo kidogo ukilinganisha na hao wagombea wengine akiwemo makongoro. nakubali tayari nina prejudice kwa makongoro. kama anafaa kuwa rais basi na mimi awamu ijayo natangaza nia.

Aaaaah haya bana (hapo kwa red), tia nia tu wapiga debe wako tupo for free

BTW mi naangalia uwezo wa mtu siangalie hizo personals kama kunywa pombe, manake kama kunywa karibia wote wanakunywa pombe. Uhuru kenyatta anakunywa balaa lakini ndo rais wa kenya sasa, mzee warioba kajijengea heshima sana nchi hii lakini alikuwa mnywaji balaa enzi zile akiwa PM wa mzee ruksa
 
Ukiona wanakodi watu kwa kuwasafurisha jua ndio mwisho wao umewadilia hizo ela wezitoa wapi na watazirudishaje? Huu ndio mwaka wa kufanya maamuzi magumu kwa kuachana na chama cha wachumia tumbo kila mtu apambane kuelimisha jamii ikifika october tuwapumzishe CCM

Sio kila mtanzania ni maskini kama ulivyo wewe...
 
nadiriki kusema hujachambua vizuri....hotuba iliyokuwa nampangilio na wasilishaji mzuri ni ya wasira......huyu nchemba anashika namba mbili kisha yule wa tamasha la jana hata namba tatu hashiki..siwezi kumuweka namba tatu hafai nafasi hiyo

Sorry ,hivi ya wasira ilikuwa hotuba au historia zaidi ya udhoefu?
 
Hufuatilii Siasa Za Nchini Mkuu. Mwigulu Leo Alikuwa UKAWA kwa hotuba yake. Amerudia Yaleyale Yanayosemwa Na Wapinzani, Hasa Katika Bunge Hili La Bajeti.
Nikikuambia kua hayo ya kuhusu viwda vya nguo niliishayaongelea miaka mitatu iliyopita utaniambia wakisema sawa na mimi wanakosea kwa sababu nimewahi kuyasema?
 
Mwigulu ni mtu nae mwamini kuliko mtu yoyote, nikimwangalia kwa kimoyo naona anastahili % 100, nikimwangalia kimacho ni mtu ambae anania ya dhati kuijenga Tanzania tunayoitaka wananchi wa Tanzania. Binafsi nimekuwa nikimwangalia bungeni ni mtu ambae kwenye swala la wananchi ata kama limetoka upinzani nilimwona akiunga hoja kwa mwili na kimoyoni hata kama alikuwa pengine kimya. Kwenye ukweli tuwe wakweli Mwigulu anastahili kwa %100 kuwa Raisi wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania. Mungu akubariki usonge mbele.. haya ni maoni yangu na mtazamo wangu, na endapo akipitishwa na CCM ntampigia kampeni kwa jamii inayonizunguka kwa sababu nina ushawishi. Narudia tena Mungu akubariki ndugu Mwigulu.

Multiple IDs at work!
 
Mwigulu kaongea unafiki mtupu, akiwa kama kiongozi wa chama na waziri maana yake mawaze yake yangeweza tekelezwa maana anshiriki baraza la mawaziri na mjumbe wa kamati kuu inayopanga ilani ya chama chao
 
Nimesikiliza vizuri na kwa umakini mkubwa hotuba za watangaza nia wote wanne wa CCM kwa kweli mtangaza nia aliyetoa hotuba nzuri na yenye ubora zaidi ni Mzee Wasira. Mwigulu kaongea vizuri sana lakini hotuba yake haifikii ubora wa hotuba ya Mzee Wasira. EL ni wakuhurumia maana ni kama mtoto.
 
Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa akili wa akili waliotangaza nia za kugombea ccm wote pamoja na kutumia vyombo vya habari vingi sijaona jipya kwani ni zile hoja za upinzani wana hoja nyepesi nyepesi lakini wameshindwa kuzifanyie kazi wakiwa madarakani wanasubiri mpaka wawe maraisi huu usanii tupu.ndani ya ccm hakuna jipya wala mabadiliko yoyote.CCM ENDELEENI NA SAFARI ZENU ZA HUZUNI ZA KUIMALIZA CCM.
VOTE FOR UKAWA
 
Tuache utani, na ushawishi Mwigulu hafai kwa lolote, hata uwaziri wenyewe unampwaya. Ni mtu hatari kwa umoja wa kitaifa: mtu ambaye yuko tayari hata kuua, ambaye hamuungi mkono. Kumbuka mauaji ya Arusha alipokuwa ameweka kambi, na kupoteza majimbo yote. Kwa ushauri wangu, Mwigulu apewe nafasi zaidi ya kuchunguzwa, atajifunua wazi jinsi alivyo.
Kwa maoni yangu anafaa kuwa jasusi, ajiuunge nao kama bado.
Watu tunaridhika tu akituimbiwa wimbo wake kuwa katoka familia maskini, kwani nani hakutoka huko?
Yupo ndani ya serikali iliyotufukarisha, na inaendelea kufukarisha anafanya nini cha msingi isipokuwa kutuhadaa na hadithi zake kuwa katoka familia maskini?
Tatizo tunasahau haraka.

Tulia unyolewe wewe
 
Sera ipi ya upinzani aliyotumia? Huyu ndio jembe la ccm hana makundi na anauwezo wa kukemea jambo lolote baya bila aibu
 
Back
Top Bottom