Kutoka D- Hadi C-, Kisha Cheti Bandia cha Ulemavu: Aliwezaje Kufanya Kazi KenGen kwa Miaka 15?

Kutoka D- Hadi C-, Kisha Cheti Bandia cha Ulemavu: Aliwezaje Kufanya Kazi KenGen kwa Miaka 15?

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Aliingia KenGen kwa KCSE certificate bandia, akafanya kazi kwa miaka 15 na kulipwa karibu Sh14.9 milioni. Baadaye, mahakama imebaini kuwa alipata pia cheti cha ulemavu kwa njia ya udanganyifu, kilichomwezesha kupata tax exemptions kwa zaidi ya miaka minne.

Huyo ni David Mogire Nyabuti, aliyekuwa mfanyakazi wa Kenya Electricity Generating Company (KenGen), ambaye sasa amehukumiwa na Anti-Corruption Court.

Mahakama ilisikia kuwa Nyabuti alifanya KCSE mwaka 1994 katika St Paul’s Igonga Secondary School na kupata mean grade ya D-. Lakini wakati wa kutafuta kazi KenGen, aliwasilisha certificate iliyoonyesha alikuwa amepata C-, qualification iliyomwezesha kuajiriwa kama Craft Grade III.

Alifanya kazi kuanzia Agosti 2003 hadi Septemba 2018. Kinachozua swali zaidi ni namna udanganyifu huo ulivyogunduliwa: alijiuzulu baada ya wafanyakazi kuagizwa kuwasilisha original academic certificates kwa verification.

Katika kipindi hicho, mahakama ilibaini alipokea Sh14,946,118 katika mishahara na benefits kutokana na ajira aliyopata kwa qualification hiyo ya uongo.

Lakini haikuishia hapo.

Mahakama pia ilibaini kuwa alipata kwa udanganyifu disability certificate kutoka National Council for Persons with Disabilities, ambayo ilimwezesha kupata tax exemptions kati ya Julai 2014 na Septemba 2018.

Senior Principal Magistrate C. Okore alimwamuru kurejesha Sh14.946 milioni, vinginevyo atumikie kifungo cha miaka mitano. Pia alitozwa Sh900,000 kwa fraudulent acquisition of public property na Sh200,000 kwa kila moja ya counts mbili za kutumia false documents.
 

Attachments

  • 1243-image.webp
    1243-image.webp
    51.9 KB · Views: 14
  • ffaebdaa694bba7d.jpeg
    ffaebdaa694bba7d.jpeg
    49.1 KB · Views: 16
Back
Top Bottom