KUTOKA DAR ES SALAAM: Uzinduzi wa Kombe la Shirikisho Tanzania

KUTOKA DAR ES SALAAM: Uzinduzi wa Kombe la Shirikisho Tanzania

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
252
Leo kutoka Jijini Dar es Salaam, Azam Sports kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu wanazindua Kombe la Shirikisho ambalo litachezwa kuanzia msimu wa 2015/2016.




Fuatana nasi kwa taarifa zaidi...

==============================
==============================


Droo ya mashindano hayo inachezeshwa sasa, tumechelewa kidogo kuanza updates hizi...

Michuano hii itahusisha timu 64 za Ligi Kuu bara na Zanzibar, Ligi Daraja la Kwanza na timu kutoka visiwani Zanzibar kwa mgawanyo uliofafanuliwa.

Timu 16 zitatoka Ligi Kuu Bara na Zanzibar, Timu 48 zitatoka Daraja la Kwanza na Daraja la Pili kwa mgawanyo wa timu 24 kila daraja.

Mashindano yataanza mwezi Novemba mwaka huu.

Kombe linarejeshwa baada ya kutochezwa kwa muda wa miaka 13! Timu zitapewa udhamini wa shilingi milioni 3 kama nauli ikiwa inaenda kucheza ugenini, vifaa!

Waamuzi watalipwa kwa viwango vya Ligi Kuu ya Vodacom!

Kuanzia 2017, bingwa wa mashindano haya atawakilisha nchi katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2017.

Jamali Malinzi anahutubia sasa...
 

Attachments

  • fa.jpg
    fa.jpg
    14.8 KB · Views: 328
Last edited by a moderator:
Asante TFF kwa kutuongezea idadi ya makombe tunayochukua msimu 2015/2016.. Simba S.C, Nguvu Moja,
 
Rekodi Zinanionyesha Kuwa Vikombe Vyote Vinavyoanzishwa Tanzania Simba Sports Club Huwa Inavichukua.

TFF Na AZAM Kama Vipi Tupeni Tu Mapema Kikombe Chetu Hicho. Hongereni Sana AZAM Kwa Kuleta Mapinduzi Ya Michezo Nchini Tanzania. Hakika Nyie Ni Watu Wa Vitendo Na Siyo Blah Blah.
 
Rekodi Zinanionyesha Kuwa Vikombe Vyote Vinavyoanzishwa Tanzania Simba Sports Club Huwa Inavichukua. TFF Na AZAM Kama Vipi Tupeni Tu Mapema Kikombe Chetu Hicho. Hongereni Sana AZAM Kwa Kuleta Mapinduzi Ya Michezo Nchini Tanzania. Hakika Nyie Ni Watu Wa Vitendo Na Siyo Blah Blah.

Hiki siyo kikombe kipya! Wa mchangani mtaendelea kubaki hivyo daima.
 
Asante TFF kwa kutuongezea idadi ya makombe tunayochukua msimu 2015/2016.. Simba S.C, Nguvu Moja,

Mkuu sembo unachokifanya ni sawa na watoto kusimama barabarani wakingojea magari yapite, gari linapoonekana tu utasikia kila mtoto anapiga kelele 'ni langu', 'ni langu', 'ni langu'; makelele hayo hayahamishi umiliki kutoka kwa yule aliyelinunua kwenda kwa mmojawapo wa watoto hao hivyo basi kila mashindano yanapoanza mikia mnajinasibu kuwa hilo kombe ni lenu, mashindano yanapofikia mwisho mwenye kombe lake (Yanga au Azam kwa kubahatisha) anajibebea hadi kwake.

Mikia FC mtasubiri sana.
 
Last edited by a moderator:
Kombe la Maji Maji hilo

Mkuu mbona mapema sana.. umehama lini Azam?.. nadhani kasi ya Mnyama, katika mechi za kirafiki 11 zilizopita imekutisha, hivyo umeamua kutafuta mchepuko mapema, ambao ni Maji Maji.
 
Back
Top Bottom