Kutoka dimba la Taifa: Simba SC watakata! Wairarua Singida Utd goli 4 kwa nunge, wajikita kileleni kwa alama mbili zaidi

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Baada ya uwanja wa Taifa kufungwa kwa kipindi, leo unafunguliwa kwa Simba kuikaribisha moja ya timu kali kwa sasa, Singida Utd. Azam ambao watakuwa na mechi ya mapema leo dhidi ya majimaji wanaombea Simba adondoshe mfupa wa point ili akishike kilele.

KIKOSI CHA SINGIDA DHIDI YA SIMBA LEO…
Peter Manyika Jr; Michael Rusheshangoga, Shafiq Batambuze, Kennedy Wilson, Maliki Antiri, Mudathiri Yahya, Deus Kaseke, Tafadzwa Kutinyu, Lubinda Mundia, Kambale Gentil, Kigi Makasi

SUB:
Ally Mustapha, Miraj Adam, Salum Chuku, Salum Kipaga, Kenny Ally, Elimwisia Sumbi Yusuph Kagoma,


KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA SINGIDA LEO;
Aishi Manula, Nicholas Gyan, Eresto Nyoni, Asante Kwasi, Juko Mushidi, Jonas Mkude, Jems Kotei, Mzamiru Yasin, Mwinyi Kazimoto, John Boco, Shiza Kichuya

WACHEZAJI WA AKIBA
Emanuel Mseja, Said Hamis, Mohamed Ibrahim, Mothes Kitandu, Emanuel Okwi, Mohamed Husen


Tega macho yako kujua kitachojiri uwanja wa Taifa, mitaa ya Chang'ombe, Dar es Salaam. Kuanzi mishale ya saa kumi jioni (10:00)
===============================

UPDATES:


01' Mechi imeanza kwa kasi na Singida wanakuwa wa kwanza kufika katika goli la Simba na mpira uliopigwa na Kambale unakuwa goal kick

03' Goooooooaaaaaaal - Kichuya anaipatia Simba goal
Kichuya anaruka na kupiga tik tak mbele ya Rushenshagoga na kuandika bao la kwanza kwa Simba

05' Simba wanashambulia tena, Manyika anatoka anachelewa Batambuzi anawahi na kuokoa
08' Simba wanaonekana kupadhibiti katikati ya uwanja zaidi na kuwapa wakati mgumu viungo wa Singida akiwemo Kutinyu
10' Bocco anautokea mpira vizuri mabeki Singida wakidhani ameotea
12' Gyan yuko chini baada ya kupigwa teke na Makasi wakati akijaribu kuuwahi mpira

22' Mabadiliko ya mapema: Ndemla ameingia kuchukua nafasi ya Kazimoto upande wa Simba.

25' Goooooaaaaaal. Asante Kwasi anaipachikia Simba bao la pili.
Ndemla anatoa pasi safi kwa Kwasi, anaweka kifuani na kuandika bao la pili kwa Simba

26' Simba wanagongeana vizuri tena, Ndemla anaingia vizuri lakini Manyika anatokea kwa ustadi mkubwa na kudaka.
34' Krosi safi ya Kichuya Bocco anaruka na kuachia mkwaju karibu goal kick
35' Kichuya anaingia vizuri ndani ya 18, anawekwa chini hapa, mwamuzi anasema twende mbele
39' Mpira unaonekana kuchezwa katikati ya uwanja zaidi na Simba bado wanazidi kutawala huku wakikaba kwa nguvu sana
41' Kaseke anajaribu kuachia mkwaju mkali hapa, Manula anadaka kwa ulaini kabisa
43' Kambale anajaribu mkwaju mkali hapa, anaokoa Mkude

45+3' Kipyenga kinapulizwa kuashiria mapumziko, Simba SC 2-0 Singida UTD.

45' Mpira umeanza na Simba wamefika katika eneo Kichuya anachia mkwaju mdhaifu, wa kitoto kabisa
48' Pasi nzuri ya Ndemla, Kichuya anauwahi na kuachia mkwaju mkuubwa, unakuwa nje pale
51' Manula anafanya kazi ya ziada, anatoka na kuokoa vizuri dhidi ya Lubinda. Yuko chini akitibiwa. Alienda nje ya 18 na kuokoa mpira uliokuwa kima cha mbuzi kwa kichwa, akajigonga kwenye goti la Lubinda
54' Kadi ya njano inakwenda kwa Rusheshangoga wa Singida United kwa kucheza kindava
59' Kambale anapokea pasi ya Kutinyu amaachia mkwaju mkali kabisa lakini Manula anadaka kimakini kabisa
62' Salum Chuku anaingia kuchukua nafasi ya Kigi Makasi upande wa Singida. Wakati huohuo Simba wanamnyanyua Okwi kwenye benchi aende kupasha misuli
65' Emmanuel Okwi anaingia kuchukua nafasi ya Muzamiru Yassin
69' Okwi anajaribu kuingia lakini Singida wako makini hapa
71' Batambuzi anajaribu vizuri kabisa hapa kutoka mbali Manula anauona
74' Shiza Kichuya peke yake akiwa amebaki na goli, baada ya pasi nzuri ya Okwi anatoa mpira njeeeee, alibaki yeye na goli pale. Muamuzi wa Pembeni pia anasema Kichuya ulikuwa umeotea

76' Goooooooooaaal - Okwi anawaandikia Simba goal la tatu
Pasi nzuri ya Kichuya, Okwi anaingia anamchekecha begi moja aliyebaki naye na kuachia mkwaju wa chinichini uliomshinda Manyika Jr na kuandika bao la tatu kwa Simba

79'
Mabadiliko kwa Singida: Anatoka Kutinyu na nafasi yake inachukuliwa na Kagoma

82' Goooooooooooooooooooooooaallll - Okwi anaandika goal la pili kwake leo na la nne kwa Simba.
Okwi alipenyezewa pasi safi kutoka kwa Ndemla, akatoka nayo kumpiga chenga kipa na kubaki yeye na nyavu na kufunga goli kirahisi kabisa pale.

84' Kotei yuko chini anaugulia maumivu baada ya kugongwa na Mudathiri
86' Okwi anatoka vizuri kabisa lakini mwamuzi anasema, Okwi ulishaotea
88' Simba wanamtoa Kotei na nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Ibrahim
90' Simba wagonga pasi tu kwa sasa katikati hapa. Dakika 3 za nyongeza hapa

Mpira umekwisha. Simba anaibuka kidedea kwa kushida goli 4 dhidi ya Singida United. Wamejikita kileleni sasa
===================

Tukutane Kaitaba - Kagera, Jumatatu ya tarehe 22/01/2018
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…