Kutoka Dimba la Taifa: Taifa Stars imeifunga DR Congo goli 2 kwa nunge, katika Mchezo wa Kirafiki

Kutoka Dimba la Taifa: Taifa Stars imeifunga DR Congo goli 2 kwa nunge, katika Mchezo wa Kirafiki

Hazard CFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2015
Posts
16,627
Reaction score
38,689
Kikosi kitakachowavaa congo leo hii

FB_IMG_1522154758930.jpg


1': Mpira umeshaanza kutoka Uwanja wa Taifa

3': Msuva anachukua mpira, kwake Kapombe, piga krosi lakini kipa wa Congo anadaka

4': Kichuuya, piga shuti moja kwa guu la kushoto na mpira unakwenda nje. Stars wameanza maridadi dakika hizi za mwanzo

5': Congo wanamiliki sasa, piga pasi moja kule mbele, mpira unakwenda nje, goli kiki

6': Stars wanapata kona ya kwanza, wanaanza kwa kupasiana hapa, inapigwa krosi langoni mwa DRC lakini unapaa juu ya vichwa vya wachezaji wa Stars

7': Congo wanapata faulo pembezoni kabisa mwa eneo la hatari la Stars baada ya Banda kucheza madhambi

8': Inapigwa na kuchezwa maridadi na mabeki wa Stars, Manula anaanza na Banda, kwake Yondani

9': DRC wanauchukua, wanapasiana eneo la nyuma, piga pasi moja mbele, mpira unatoka, unarushwa kuelela Stars

10': DRC wanapata kona ya kwanza, wanapiga inaenda mpaka nje

11': Faulo tena kwenda Stars, DRC walishaanza, wanapasiana eneo la kati. Bado wanao, Kapombe unamfikia, anapia shuti kurejesha mbele

13': Mpira bado haujawa na makali kwa timu zote mbili mpaka sasa, hatari langoni mwa Stars, inapigwa krosi moja, unaokolewa

14': Mpira anao Mao,piga mbele lakini wapinzani wanaokoa. DRC wanaanza sasa nyuma, unamkuta mshambuliaji kulia mwa Uwanja huku, piga krosi lakini inakuwa mkaa. Mpira unakuwa goli kiki kuelekea DRC

15': Matokeo bado ni 0-0, kila timu inafanya jitihada za kutafuta bao la mapema

18': Issa anashindwa kupiga krosi baada ya kumtoka beki wa DRC hapa, mpira unakwenda nje

19': Banda sasa na mpira, anampasia Gadiel, Congo wanatoa. Msuva anarusha lakini inakuwa faulo. Pigwa kuelekea Stars

21': Kona ya pili inachongwa kuelekea Stars. Pigwa kona moja kubwaaa inakwenda mpaka nje ya Uwanja

22': Kichuya anapasia kwake Kapombe, anapiga krosi safi lakini inakosa wamaliziaji

23': Kibangala anatoa nje mpira, unarushwa kuelekea DRC, Kapombe amesharusha, kwake Banda sasa, anampasia Gadiel, piga huku kumtafuta Nyoni, anampasia Faisal. namna gani anapiga krosi mkaa, mpira nje

25'; Stars wanafanya shambulio kali hapa, krosi ya Gadiel Michael inapanguliwa na kipa wa DRC na kutoka nje, inakuwa kona. Kona inapigwa na kipa anadaka

26': Mpira umesimama kidogo, Issa ameumia, wakati huo Mayanga anashauriana na wachezaji wake

27': Congo wanaanza kwa kupasiana eneo la nyuma ya uwanja, kwenda huku mbele, inakuwa faulo, Mpira unachezwa kuelekea langoni mwa Stars, Banda anapata kadi ya njano

29': Offside! Mohammed Issa ameotea

31': Congo wanarusha mpira baada ya kutoka, rusha huku unatolewa tena
Namna gani hatari pale, DRC walifanya shambulio kali lakini Stars wanaonesha umahiri, wanaokoa

33': Mpira umesimama, kuna mchezaji wa Congo ameumia. Unaanza tena, Kapombe anampasia Ndemla

35': Mpira sasa anao Simon Msuva, anapiga kwake Samatta, kwake Kapombe, piga krosii, inatolewa nje, ni kona. Msuva anapasia kwake Kichuya, piga huku, kona nyingine, anapiga Msuva

37': Msuva tenaa, anapiga kichwa lakini kinakwenda pembeni kidogo ya mtambaa panya

38': Mpira ni faulo, karibu na eneo la hatari la Stars, inapigwa huku, goli kiki

39': Himid Mao anapiga pasi isiyo na malengo na kutoka nje

40': Dakika zinayoyoma Stars wanajaribu kufanya mikakati ya kupenya ngome ya DRC japo inakuwa ngumu

42': Mpira ni faulo, unapigwa kuelekea Stars

43': Hatari huku katika lango la DRC, kipa anaokoa mpira, ilikuwa kidogo Msuva acheke na nyavu

45': Manula anadaka shuti kali la mshambuliaji wa DRC, piga huku mbele, Msuva anakosa tena bahati, mpira unakwenda nje

DAKIKA 45 ZIMEMALIZIKA, ZIMEONGEZWA MBILI

45': Kipindi cha pili kimeanza. Ni lala salama ya Stars kutafuta ushindi

46': Mayanga anashauriana na benchi lake la ufundi huku mpira ukiendelea

47'; Samatta anapasia kwake Yondani, kwake Samatta tena, mabeki wa DRC wanamchezea faulo Samatta, mpira unapigwa kuelekea DRC

48': Hatarii, Samatta anamtengeneza pasi muruuua kabisa Msuva na anadondoshwa ndani ya eneo la penati boksi, Mwamuzi anasema hakuna penati.

49': Goli kiki, DRC wanaanza

50': Nyoni anacheza madhambi, mpira unapigwa kuelekea Stars, piga huku lakini DRC wanaudaka tena

51': Msuuuuva, piga shuti kali lakini linaishia kwenye nyavu za nje, ilikuwa ni shambulizi moja zuri kwa Stars

52': Mohammed Issa na mpira, pasia kwa Msuva, unamkuta kipa wa Congo anaokoa kwa kupiga shuti kali

53': DRC wanaanza eneo la nyuma

54': DRC wanakosa nafasi ya kupata bao la kwanza kufuatia shambulizi zuri, mpira unakwenda nje
Ndombe anatoka upande wa DRC, nafasi yake inachukuliwa na Junior Kabananga

56': Stars wanaanza tena eneo la ulinzi, pigwa kwake Msuva huku mbele, mabeki wa DRC wanakuwa maridadi wanacheza kuokoa mpira

57': Goli Kiki, wakati huo Manula anawaonya wachezaji wake wazidi kuwakaba DRC, wasiwaachie
Mohammed Issa ameumia, mpira umesimama kwa muda

58': DRC wako langoni mwa Stars, wanafanya jitihada za kuandika bao la kwanza, mpira unakuwa faulo, unapigwa kuelekezwa DRC

59': Mohammed Issa anatoka baada ya kuumia, Ibrahim Ajib anachukua nafasi yake

60': Mpira ni goli kiki, unapigwa kuelekea DRC, Manula anaanza taratibu na Yondan, pigwa mbele huku

61': Ajib anashindwa kutumia nafasi yake ya kwanza vizuri, baada ya kupiga shuti na kwenda nje ya goli

62': Offside, Stars wanaotoea, bado matokeo ni 0-0

63': Bahati mbaya inaiandama Stars, Msuva anakosa kuiandika tena Stars bao, mpira unamtoka miguuni na kwenda nje, Goli Kiki

64': DRC walishaanza, wanatoa nje, unarushwa kuelekea langoni kwao

65': Kelvin Yondan anao mpira eneo la nyuma huku, pasia kwake Kichuya, DRC wanauchukua, hatarii huku langoni mwa Stars inatokea piga nikupige na DRC wanakosa goli la wazi kabisa, yangekuwa mambo mengine muda huu

67': DRC na mpira, pigwa pasi moja, mabeki wa Stars wanaokoa na mpira unakwenda nje. Unarushwa huku, Manula anadaka

68': Mpira umesimama, Banda amekaa chini

70': Wachezaji wa akiba wa Stars wanapasha

71': Gadiel Michael anagangwa na madaktari baada ya kuumia mguu wakati akiokoa mpira uliokuwa unaelekea kwenye nyavu za Stars

73': Kocha Mayanga ameshindwa kukalia kiti chake, muda wote amesimama, hii ni kuhakikisha vijana wake wanapambana

74': Goooooli, Mbwana Samatta anafunga bao la kwanza kwa njia ya kichwa kufuatia krosi nzuri ya guu la kushoto kutoka kwa Shiza Kichuya, Stars 1, DRC 0

77': DRC wameshaanza, Stars wanaunyaka, piga huku mbele kwake Samatta tena, unamkuta Kichuyaaaaa, kipa anadaka, ilikuwa hatari

78': Kwenda huku mbele sasa wachezaji wa DRC na mpira, wanajaribu kutafuta bao la kusawazisha

79'; Bado DRC wana mpira

80': DRC wanapambana kupata bao hapa, Stars wanaondoka na mpira, kwake Samatta lakini DRC wanaokoa tena

82': Mpira ni goli kiki, Kipa wa DRC anaanza upya
Gadieeeel, piga shuti moja lakini linapaa juu ya lango

84': Kadi ya njano anapewa beki wa FRC baada ya kumchezea madhambi Ibrahim Ajib

85': Zimesalia dakika 5 mpira kumalizika

86': Gooooooli, Kichuyaa, anafunga bao la pili kufuatia kazi nzuri aliyotengenezewa na Samatta

87': Mabadiliko; Kichuya anatoka Uwanjani, nafasi yake inachukuliwa na Rashid Mandawa

89': Shomari Kapombe amebebwa kwenye machela kutolewa nje baada ya kuumia

DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA, ZIMEONGEZWA DAKIKA 4

91': Manula anapiga mbele huku kuwatafuta washambuliaji

92': DRC wanajaribu kupenyeza kulia mwa Uwanja walau kupata bao la kufutia machozi, faulo, mpira unapigwa kuelekea Stars

93': Unapigwa huku, Stars wanaokoa

94': Yahaya Zayd anaingia kuchukua nafasi ya Simon Msuva

FULL TIME: MPIRA UMEMALIZIKA KUTOKA UWANJA WA TAIFA, STARS 2-0 CONGO
 
Kipindi cha pili sio mbaya japo pasi za mwisho hazina ukamilifu mwema
 
Kipindi cha pili kinakaribia kuanza
 
Mbona congo ya leo ndembendembe, yaani twajipigia tu.
 
Back
Top Bottom