Kutoka hapo ulipotoka hadi hapo ulipo leo.

Kutoka hapo ulipotoka hadi hapo ulipo leo.

Mkwaruzo

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2011
Posts
563
Reaction score
98
Waliweza kufurahikia uzawa wako baada ya kuwafikia ukiwa salama. Ndipo hapo majukumu yaliyokuwa yanawakabili yalipowaongezekea. Hata hivyo waliweza kuweka azama ya kutaka kukufanyia yaliyo bora ili kukuwezesha kukua katika hali nzuri kiafya na kielimu licha ya shida walizokuwa wanazo.
Kutoka huko ulikotoka hadi kufikia hapo ulipo, hiyo yote ni bahati yako na unapaswa umshukuru Mungu kwani ni wengi ambao maisha yao yalikatishwa tokea wakiwa ndani ya matumbo ya mama zao. Na kati ya hao walioweza kuiona dunia, baadhi maisha yao yalikatika baada ya ya kutupwa katika mitaro au mashimo ya vyoo. Baada ya kutupwa, baadhi waliweza kuokotwa na wasamaria wema ambao waliweza kuwachukuwa na kuwalea kama watoto wao wa kuwazaa. Wote hao makosa hayakuwa yao bali yalikuwa ni ya wale waliyokuwa wanakata matunda ya yale waliyokuwa wakiyafanya.
Katika hali yoyote uliyopitia hadi kufikia hapo ulipo leo, hayo yanaweza kuwa ni machache tu kati ya yale uliyofanyiwa. Sasa inakuwaje unaweza kusahau fadhila zao kwako kwa kujiona upo umekuwa kidume wa kuyakabili maisha na hivyo kuwa na mdomo pima wa kuwajibu vile utakavyo. Ukawa huwajali wala kuwathamini na kusahau kuwa kukosa radhi zao kunaweza kuwa ndiyo mwanzo wa laana.
Kwa upande mwengine, wewe uliye mzazi/mlezi inakuwaje unamtengenezea mwanao mazingira ya kukuchukia na
kukuona mbaya bila ya sababu za msingi. Kama mzazi/mlezi tambuwa kuwa huwezi kupata heshima na upendo wa kweli kama wewe mwenyewe hujajitengenezea mazingira ya kupata vitu hivyo. Nimalize kwa kusema kuwa vyovyote vile iwavyo, sisi ni binaadamu.
Hivyo basi ni kawaida
kukoseana miongoni mwetu iwe katika familia, jamaa, marafiki au hata humu katika JF, basi ni wajibu wetu kusameheana na kuondosha tofauti kati yetu na wale tunaokoseana nao. Nami kupitia thread hii naomba msamaha kwa pale nilipowakosea.
 
Ahsante Mkwaruzo nafikiri uliyosema yanajitosheleza sana sina haja ya kuongeza hakuna kitu kizuri kama mtu kugundua kuwa amekosea na kuomba msamaha na yeye pia kujua kusamehe ili jambo kama lingekuwa ni rahisi sana miongoni mwa jamii tunayoishi tungekuwa na amani sana. Thanx nafikiri hii ni thread nzuri sana kwa kulala nayo huku nikijiuliza niliwakosea wangapi? na je nimeshawahi kuomba msamaha? na je nikiombwa msamaha huwa nasamehe? goodnight
 
Thanks my dear, Gaga. Wish U 2 gud nyt, well sleepin nd luvly swty dreamz. (Lala salama Uamke salama)
 
Hahahaha!Acha unoko mshkaji kaonyesha tu msisitizo na sio tafsiri!

we muache tu, na kama yy kaona hiyo ni tafsiri, basi hajakosea coz inaweza kuwa ni tafsiri ya lengo kwa vile zote zinapeleka ujumbe m1 ila siyo tafsiri ya neno kwa neno tu
 
Thanks my dear, Gaga. Wish U 2 gud nyt, well sleepin nd luvly swty dreamz. (Lala salama Uamke salama)

mh, yani lengo la thread limepotea kwa maneno haya. sipati picha...!
 
Back
Top Bottom