kumshambulia mgombea
urais kwa kiketi ya Chadema,
Edward Lowassa aliyewahi
kuwa kada wa chama hicho.
Nape alirusha makombora
yake kwa Lowassa jana
alipopewa nafasi ya
kumnadi mgombea urais wa
CCM, Dk. John Magufuli
katika viwanja vya Samora,
mjini Iringa.
Alisema Lowassa ni mwizi na
fisadi na kwamba hakuna
sehemu ambayo alipewa
kufanya kazi katika ngazi za
CCM na serikali bila kuiba.
Nape alidai kuwa Lowassa
alishindwa kukaa katika
chama cha Mapinduzi kwa
kuwa hawezi
kufugika...."Lowassa ni
Kunguru,Hafugiki." Alisema
Nape.
Katika hatua
nyingine,Nape alidai kuwa
Lowassa aliwanunua
viongozi wa ngazi za juu
wa UKAWA na CHADEMA
ili apate nafasi ya
kugombea kupitia
Chadema ambayo awali
ilikuwa ikimuita fisadi.
Katika maelezo yake,Nape
alisema mbunge wa
Iringa mjini,mchungaji
Peter Msigwa ni miongoni
mwa walionunuliwa na
Lowassa kwa shilingi
milioni 340.
Nape amekuwa akirusha
makombora kwa Lowassa
tangu alipotangaza uamuzi
wake wa kukihama chama
hicho na kujiunga
CHADEMA.
Nape aliwahi kunukuliwa
akisema kuwa amekuwa
akipambana na Lowassa
kwa miaka 12 ndani ya
CCM na kwamba mziki
wake anaufahamu
Hata hivyo, tangu
alipoanza kampeni
zake,Lowassa amekuwa
kimya bila kujibu
mashambulizi ya Nape na
viongozi wengine wa
CCM,hali inayomfanya
azidi kujipatia umaarufu
mkubwa zaidi wa kiasiasa.
Wakati Nape akitumia
muda mrefu kurusha
makombora, Lowassa yeye
alikuwa Jijini Tanga
akifanya mkutano mkubwa
wa kampeni uliolazimika
kukatishwa kutokana na
mafuriko ya wananchi
kuzidi eneo la mkutano.
YOUTUBE