Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aise Ina lipa sana hasa hapa dsmBiashara ya miwa juice inalipa, ahsanteni
Dah maisha yana Siri kubwa aiseKuna story katikati itaendlea kuwa siri yake bruz ila ili ufanikiwe lazima uanze na kitu then mambo yatajipa umo umo ndani yake ata ukienda kwa mganga upate utajiri utaambiwa anzisha biashara yoyote . Chempa akiminywa vizuri atatoa maelezo yalinyooka utajiri una siri nyingi
🙌🏻🙌🏻🙌🏻Kwa kweli mkuu ni vyema nipambane na ka njia kangu kwa upande wangu kwenda kuuza juice ya miwa hapanaAnza na wewe ufike huko. Binadamu sehemu kubwa ya maisha yake husema uongo hasa kinapofika kipengele cha mafanikio ya maisha yake
NakaziaMotivesheno spika embu tupumzisheni kwanza
Ni kweli mkuu, wapo wataopinga Ila ukweli ndiyo huo.....Aise Ina lipa sana hasa hapa dsm
Hahahahahaaaumeonaakwanini usirithi goli lake la juice ya miwa?
Kauze miwa uone kama utatoboa?.kuna vitu vingine kwenye biashara huwezi kuviona ni mwenye biashara tu ndiyo huwa anajua anavyofanya ili kukuza biashara yake.Anakuwa anaonekana kwenye biashara hii kumbe baishara kamili anayofanya ni nyingine kabisaWadau habari za saa hizi ningependa Leo tusambaziane mawili matatu kuhusu biashara ambazo haziku dhaniwa lakini zimetoa watu.
Aisee wakuu kuna wakati mwingine maisha yanakufundisha kwamba mafanikio hayachagui kazi, bali ni juhudi, uvumilivu, na akili ya kibiashara. Mimi na Chempa tulianza maisha tukiwa na ndoto kubwa, dah! lakini hatukuwa na kitu kabisa. Chempa bhana, nyumbani kwao ni Rombo, Kilimanjaro, lakini kutokana na hali ngumu ya maisha, aliamua kufungasha virago na kuja Dar es Salaam kupambana. Hakukuwa na pa kuanzia, hakukuwa na msaada wowote, lakini jamaa alikuwa na kitu kimoja – moyo wa simba na akili ya kupambana.
Alipoingia hapa Mzizima bhana, hakuwa na mtaji mkubwa wa kuanzisha biashara ya maana, lakini hakuwa na muda wa kulalamika. Alianza maisha ya kuhustler kinoko, akifanya vibarua vya hapa na pale huku akili yake ikiwa kwenye kitu kimoja – kutoka kwenye lindi la umaskini. Ndipo siku moja akaamua kujaribu bahati kwenye biashara ya juice ya miwa bhana. Alianza kwa mtaji mdogo, lakini alikuwa na uthubutu wa hali ya juu. Alijua kwamba biashara yoyote inawezekana ikiwa mtu ataweka bidii na akili ndani yake.
Miaka kadhaa ilipita na Chempa alikuwa amegeuza biashara yake ya juice ya miwa kuwa chanzo cha mamilioni. Hapo Kawe, kwa siku moja jamaa alikuwa analaza kati ya laki mbili mpaka laki tatu! Nilikuwa naangalia biashara yake na sikuamini macho yangu – mtu aliyekuwa hana chochote sasa alikuwa anapiga pesa ya maana kwa kazi ambayo watu wengi wangeidharau. Watu walimuona akisimama na mashine yake ya kusaga miwa, lakini hawakujua kwamba nyuma ya biashara hiyo, kulikuwa na mpango mzito wa kupiga hatua kubwa zaidi maishani.
Chempa hakuridhika na mafanikio ya juice ya miwa pekee. Alianza kuweka akiba na kupanua mawazo yake ya biashara. Alianza kusafiri mara kwa mara kuelekea Iringa na Mafinga, akitafuta fursa nyingine kubwa zaidi. Ndipo alipoingia kwenye biashara ya mbao, na hapo ndipo maisha yake yalibadilika kabisa. Leo hii, jamaa ana Scania zaidi ya 100 zinazobeba mbao, na amekuwa mmoja wa wachezaji wakubwa kwenye sekta hiyo. Wakati nikiwa Dar namkumbuka Chempa yule wa juice ya miwa, leo hii yupo Mafinga na Makambako akisimamia miradi yake mikubwa.
Siku moja nikiwa na marafiki tunapiga stori kuhusu watu waliotoboa kwa biashara za ajabu, nikaamua kumtaja Chempa. Jamaa mmoja akanicheka na kusema, "We unataka kuniambia yule aliyetoka kuuza juice ya miwa sasa anaweza kunituma nikamnunulie hata ugoro sokoni?" Nikamuangalia tu nikacheka, maana sikujua kama anatania au anamaanisha. Ukweli ni kwamba maisha hayachagui kazi – yanachagua juhudi, bidii, na nidhamu.
Kwa kweli Chempa amenifundisha jambo moja kubwa maishani – hakuna biashara ndogo, kuna akili ndogo za kuona biashara kama ndogo!
Je ni biashara gani mdau ambayo hukudhania kama inaweza kumtoa mtu mtu it has been like a miracle Yani imemtoa mtu?
Aise ni kweli sometimes huwa hivyo japo biashara nyingi ndogo hufanya vizuriKauze miwa uone kama utatoboa?.kuna vitu vingine kwenye biashara huwezi kuviona ni mwenye biashara tu ndiyo huwa anajua anavyofanya ili kukuza biashara yake.Anakuwa anaonekana kwenye biashara hii kumbe baishara kamili anayofanya ni nyingine kabisa
Waaapiii? Mishe gani?🙌🏻🙌🏻🙌🏻Sasa hivi napiga mishe zingine mkuu
Kwa kweli aisee.. au atuunganishe na tajiri moja kwa moja maana tu Natafuta AjiraMotivesheno spika embu tupumzisheni kwanza
Bahati ya mwenzio???kwanini usirithi goli lake la juice ya miwa?