Kutoka kijiweni: Kwa mwendo huu itafikia mahali tuanze kuwaombea wenzi wetu dhiki....

Kutoka kijiweni: Kwa mwendo huu itafikia mahali tuanze kuwaombea wenzi wetu dhiki....

siyo rahisi kumuacha na ulimbukeni wake maaana unakuta unakuathiri na wewe.
Ujue kuna hatua inafikia mtu anakata tamaa na kusema "Mungu nayakabidhi yote haya mikononi mwako". Ukiendelea kumfikiria sana basi utajiumiza wewe mwenyewe zaidi, usijekufa kwa presha bure. Unaendelea tu na maisha yako
 
Hahaha eti #teamrohombaya#. Ila honestly kuna watu wanajuta kwa nini wenza wao wamefanikiwa. Kwa mfano sasa hivi uncle Magu anavyotumbua mijipu kuna watu wanafunga kwa maombi wenzi wao watumbuliwe angalau wakumbuke na nyumbani. Ulimbukeni mbaya sana, ila me namuacha tu bana na Ulimbukeni wake, nastick na kujiinua binafsi.. maisha mafupi sana haya

KWELI MAFUPI LAKINI INAUMIZA KUIKUBALI HIYO HALI
 
Mi yalishanikuta hayo boy friend wangu alikuwa Hana kazi kwa muda wa mwaka mmoja nikamtunza na kumvalisha akaniomba mtaji nikampa . Chamoto nilikiona alivyoanza kupata hela tu akaanza vitimbi Mara kulala nje nikamchoka nikamtimua Yan nimekoma kuliko kumsaidia mwanaume bora watoto yatima nipate thawabu.
"masiki akipata sio msemo tu kwakweli"
 
Good morning.....
kapita kaka muuza nguo kavuta kiti kakaa tukaanza kuchagua viwalo, kama kawaida kijiwe huwa hakikauki story, story zikaanza fursa za biashara tukapewa darasa, tukahamia kwenye kilimo ana mashamba yanamlipa sana basi akashauriwa "kwanini nguo usifungue duka wife asimamie we uwe bize na kilimo"

Akaanza kama ifuatavyo nanukuu "ndugu zangu msidhani masikini akipata masaaburi hulia mbwata ni msemo tu, mke wangu ni mmoja kati ya masikini waliopata, enzi hizo hakuwa na kitu wala kazi alikua mtiifu sana kwangu, tunashauriana mambo ya maisha na biashara, tunapanga pamoja ila tangu apate kazi na kuanza biashara zake naona kaota mapembe heshima aliyokua nayo kaizika. tulipanga tufungue duka yeye awe msimamizi, nimekuja kushangaa wife ana Duka tayari ambalo amefanya sharing na mtu mwingine anaedai ni rafiki pia yupo kwenye mpango wa kufungua mradi mwingine ambao pia anashirikiana na mtu mwingine, nikiuliza namwagiwa matusi yasioelezeka, basi nimeona namie nifanye tu biashara zangu kama hivi "

Nikakumbuka jamaa mmoja ye akiwa hana kitu ni mpole kobe kasingiziwa, ila akipiga dili sasa mmmh ni matusi ni kipigo kwa mke na hali inaendelea hivo hadi aishiwe

Kwa hali hii itafikia muda sasa wa kufunga na kuombeana umasikini teh team rohombaya

PANIC AT YOUR OWN RISK!!!
 
Back
Top Bottom