Kutoka kofia ya barghashia ya Nyerere 1964 hadi msalaba wa William Lukuvi 2014

Kutoka kofia ya barghashia ya Nyerere 1964 hadi msalaba wa William Lukuvi 2014

Mimi unishangaza sana dini inapotumika kuonyesha kuwa ilipigania uhuru wa Tanganyika. Nina hakika wahusika waliokuwa mstari wa mbele katika kudai uhuru wetu hawakusukumwa na dini zao bali nafsi zao kwa kuona udhalimu wa ukoloni. Ingekuwa ni dini ndiyo zilifanya hivyo, nafikiri sasa tungekuwa na tatizo kubwa. Tume one mataifa ambayo dini zimetumika kudai haki au uhuru, matunda yake yako dhairi!
 
Mashaalah, unazidi kutuelimisha mwalim wetu. ALLAH akuzidishie Kheri kwa ELIMU yako isiyo na mipaka.
Ukweli utasimama sikuzote, waliokuwa wanakupinga Leo wanaanza kuthibitisha kauli zako na KUNUKUU maneno yako.
Tumeoana na kusikia mengi Kwenye bunge la katiba na bado naamini tutaonana na kusikia mengi zaidi.
 
Jasusi Mag3 nguruvi MWANAKIjiji Son of Alaska njooni huku Mohamed Said ameshaanza kumwaga pumba anaitaji kusahishwa

Hoja hujibiwa kwa hoja...Binafsi nakuona wewe ndo mwenye Pumba hapa... Hukumsikia Lukuvi? wewe uliona maneno yake yako sawa?...Fikiria kwanza kabla ya kuandika Mkuu... I wish ungefikiria kwanza kabla ya kuandika badala ya kuandika ndipo uanze kufikiria kama ufanyavyo sasa..
 
Mzee Mohamed Said wewe ni mmanyema wa Kigoma kwa akina abakorakamo. Mahaba uliyonayo kwa Zanzibar yanatoka wapi? Pambana Tanganyika yako Irudi.

Wewe vipi laumu Maalim Mohamed Said yeye kusemea mambo ya Zanzibar kwa sababu yeye penda Tanganyika. Wewe kama taka Tanganyika rudi basi pigania free sovereign Zanzibar. Impossible Tanganyika to annex Zanzibar and call it Tanganyika. You learn history from him sio that been cooked at Pengo's Altart and Chuo ya Kivukoni.
gombesugu bhai
 
Last edited by a moderator:
Mimi unishangaza sana dini inapotumika kuonyesha kuwa ilipigania uhuru wa Tanganyika. Nina hakika wahusika waliokuwa mstari wa mbele katika kudai uhuru wetu hawakusukumwa na dini zao bali nafsi zao kwa kuona udhalimu wa ukoloni. Ingekuwa ni dini ndiyo zilifanya hivyo, nafikiri sasa tungekuwa na tatizo kubwa. Tume one mataifa ambayo dini zimetumika kudai haki au uhuru, matunda yake yako dhairi!
The bottom line ni kwanini historia yao imepotezwa? Kwanini michango yao haienziwi? Kwanini tusikubaliane na Lisu kuwa Nchi hii imejengwa katika misingi ya Uwongo?...Jipange uje upya Mkuu...
 
Wewe vipi laumu Maalim Mohamed Said yeye kusemea mambo ya Zanzibar kwa sababu yeye penda Tanganyika. Wewe kama taka Tanganyika rudi basi pigania free sovereign Zanzibar. Impossible Tanganyika to annex Zanzibar and call it Tanganyika. You learn history from him sio that been cooked at Pengo's Altart and Chuo ya Kivukoni.
gombesugu bhai
hahahahaha JF ni zaidi ya burudani... Shukran sana Punjab Singh, Jamaa umempa darasa tosha ...
 
Mheshimiwa Mohammed Said, nimekuwa nikijifunza mambo mengi sana kupitia vitabu na makala zako mbalimbali, ni miongoni mwa wasomi wachache sana wenye kujua ukweli na kuusema bila kuficha, umewafungua na kuwatoa usingizi watu wengi sana hapa nchini juu ya historia halisi ya Tanganyika na mchango wa wazee wa kiislaam katika kudai uhuru.
Baada ya mwalimu nyerere kukaribishwa kwenye chama cha TAA na kina ABDUL SYKES, malipo aliyowalipa wale wazee ni kufuta historia zao, kufuta taasisi yao ya EAMWS, na kuwaundia waislaam BAKWATA inayowatafuna waislaam mpaka leo.
kama Nyerere asingefanya yote haya LUKUVI asingethubutu kutamka maneno yale pale bungeni! ametamka yale kwa ujasiri kwa sababu mfumo aliotengeneza NYERERE una mruhusu.
 
Mi naona mleta mada kosa ni kuvaa misalaba wa dhahabu uyo nyerere ingemkuta zama hizi mbona angevaa tu
 
Wewe vipi laumu Maalim Mohamed Said yeye kusemea mambo ya Zanzibar kwa sababu yeye penda Tanganyika. Wewe kama taka Tanganyika rudi basi pigania free sovereign Zanzibar. Impossible Tanganyika to annex Zanzibar and call it Tanganyika. You learn history from him sio that been cooked at Pengo's Altart and Chuo ya Kivukoni.
gombesugu bhai
Acha kujifanya mhindi wewe gaidi
 
Nchi hii inanuka udini, ubaguzi wa rangi, ukabila, ukanda na baya zaidi viongozi waandamizi Serikalini wameanza chokochoko kwa kuchochea maovu hayo ndani ya majumba ya kuabudia! bilashaka Profesa Lipumba yuko sawa kuliona hili kwa kututahadharisha wa TZ tuwe macho na kundi lenye mrengo wa Kiinterehamo!!
 
Binafsi sijashangazwa na kauli ama maneno aliyoyatoa Ndugu Lukuvi,isipokuwa nimepata faraja kwa wale Waislamu waliokuwa na mashaka kuwa hakuna Udini nchini.kwa sasa mashaka Yao yamepungua kama si kuondoka kuwa(Udini upo na ni mkubwa sana.) Udini ambao inafikia mpaka kwenye mashirika ambayo serikali ina hisa zake na inakubali pesa kwenda kanisani(CRDB NI Mfano mzuri) kwani ni nani asiyejua kuwa hata bungeni baada ya bunge wabunge wakristo hukaa na kupanga mikakati yao mizito ya kipi kipite? Mwisho Nikushukuru sana ndugu Lukuvi kwa kuendelea kutukumbusha wajibu wetu sisi waislamu tujue nini cha kufanya.

N:B
ingelikuwa maneno hayo aliyotamka Lukuvi angetamka muislamu,bila Shaka kiti cha uwaziri angelinyang'anywa mara moja.lakini Hili kwa kuwa kasema mtu wa kanisa basi tuendelee kuona jamaa akipeta japo hana hata elimu ya kiivyo."Mods wakiona hivi basi Uzi hatukai wataufanyia Kila hila utoke.
 
Huwa unapenda kutumia vitu vidogo vidogo ambavyo vipo visible ili kujenga hoja yako, kwa lengo la ku capture attention ya majority wenye ufinyu wa kupambanua mambo.
Kama hapa unapojaribu kuoanisha Uisilam na balaghashia. Balaghashia ni moja ya mavazi ya kichwani ya kitamaduni maeneo ya arabuni. Ukiwa huko ni sehemu ya maisha ya kawaida sana kuona watu wanaenda kanisani wakiwa wamevaa baraghashia na kanzu.
Hata hapo Zanzibar utakuta wanaweka wamevaa hijab na wanaendakusali kanisani. Inawawezekana una hoja nzuri unataka kuijenga na kuiwasilisha lakini tabia ya kuokoteza tuvitu hutu tudogo twenye mafungamano na tamaduni za watu kwa lengo la kujigeuza 'centre of gravity' inakupunguzia maksi mbele ya watu wafuatiliaji na makini.
Otherwise huwa nakusifu kwa tabia ya kupenda kuandika.
 
Hivi umri wa wastani wa maisha ya mtanzania ni miaka mingapi?
 
Wanaukumbi,Imekuwaje leo Uislam wa Zanzibar unakuwa neno miaka 50 baada ya muungano? Kuna kitu hapa hakisemwi kwa kuwa kinatisha. Dunia nzima hivi sasa Uislam unakuja juu na huu ni ukweli usiopingika. Hapa kwetu Tanganyika Uislam umechukua sura nyingine pia. Kuna kitu Ulaya na Marekani wanakifahamu nacho ni ''Militant Islam.'' Hili ni somo tosha linalojitegemea lakini hapa hatuwezi kuingia ndani ila itoshe tu kusema kuwa kuna Waislam wananyanyua silaha kuilinda dini yao. Kama hivyo ni sawa au si sawa hilo tuwaachie maulamaa waamue. Ili mtu aweze kuelewa kwa nini leo uhusiano kati ya Zanzibar na Tanganyika umefika hapa ulilipofika ni muhimu sana akaijua historia ya kweli ya muungano. Vinginevyo mtu atakuwa anatapatapa hana mahali pa kushika.Mwaka 1964 wakati Tanganyika inaungana na Zanzibar, Tanganyikahaikuwa kama hivi sasa ilivyo. Suala la ''udini'' halikuwapo katika siasa za Tanganyika. Uislam ulikuwa umetumika vilivyo kupigania uhuru wa Tanganyika bila ya kuuathiri Ukristo na hakuna aiyekuwa hajui nguvu ya Uislam. Nyerere mwenyewe aliingia madarakani mwaka 1961 na kuishika nchi akiwa amekaa juu ya mabega ya Waislam. Siasa zilizotamalaki wakati ule zilikuwa siasa za uzalendo wa Kiafrika. Dini katika uendeshaji wa nchi haikuwa na nafasi. Hii leo mambo yamebadilika sana.Uislam Tanganyika ulianza kupigwa vita vya chini kwa chini mara baada ya uhuru hatimaye kufika mwaka 1968 vita hii ilikuwa ishafika kileleni katika mgogoro wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na kuundwa kwa BAKWATA. Si siri tena kuwa Nyerere na Kanisa Katoliki walihusika sana na hatimae nguvu ya Waislam katika siasa za Tanganyika zikapotea kabisa pamoja na historia ya Uislam katika kupigania uhuru wa Tangayika. Hadi leo mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika historia yao imefutwa. Imekuwa mwiko hata kuwataja katika vitabu vya historia.Hivi sasa hisia za Uislam katika nchi yetu zinafukuta chini kwa chini na ndiyo maana tumekuwa na mauaji ya Mwembechai, Picha ya Ndege, na Kilindi na vijiji vya pembezoni mwake hivi karibuni na majuma mawili yalopita tu Waislam wamingiliwa msikitini (staili ya Mwembechai) na kupigwa na polisi. Kesi za masheikh zimekuwa maarufu Zanzibar na Tanganyika. Shuhudia hapa JF hamaki za kidini na wakati mwingine matusi baina ya Waislam wa Wakristo. Hizi ni dalili tosha kuwa mambo si shwari tena. Kitu cha kushangaza ni kuwa viongozi wetu wanajifanya hakunajambo, tuna amani. Hii leo Zanzibar Karume akitajwa baadhi ya watu wanamlaani na halikadhalika Tanganyika Nyerere akitajwa baadhi ya Waislam wanamlaani. CCM Zanzibar katika chaguzi zote toka 1995 wamekuwa wakishindwa na hili linafahamika dunia nzima. Zanzibar wanachukua serikali kwa mtutu wa bunduki. Kitu cha kujiuliza ni hiki. Ni nani hawa wanaowanyima CCM Zanzibar kura? Jibu ni kuwa hawa ni wananchi na wengi wao wamezaliwa baada ya mapinduzi. Wazanzibari asilimia 99 ni Waislam. Hii asilimia 99 leo inajua kuwa nchi yao imeungana na Tanganyika mbayo viongozi walioshika madaraka ni Wakristo na wana chuki kubwa na Uislam. Wazanzibari hawajasahau sakata pale walipojiunga na Organisation of Islamic Conference (IOC) mwaka 1993 na wala hawajasahau Aboud Jumbe alivyotolewa madarakani Dodoma kwa kuidai Zanzibar. Viongozi wa leo wa Tanganyika hawa hawapendezi Zanzibar kama walivyopendeza kwa wazee wao wakati wa muungano mwaka wa 1964. Viongozi hawa ndiyo hawa katika kundi la akina William Lukuvi wanaoingia kanisani na bila hofu kusema kuwa hawataki kuiona Zanzibar inakuwa nchi ya Kiislam. William Lukuvi alipopewa nafasi ndani ya Bunge Maalum la Katiba kujieleza bila hofu na kwa kibri cha hali ya juu akarudia maneno yale yale na kusema yeye si mnafiki atasema kile kilicho katika nafsi yake kuwa hawawezi kuiachia Zanzibar iwe huru isimamishe Uislam. Ile picha iliyozoeleka Zanzibar na Tanganyika hapo zamani ya kuwaona Karume na Nyerere wote wamevaa kofia za mkono (kofia za Kiislam) leo haipo. Labda kitu cha kujiuliza leo ni kwa nini Nyerere aliacha kuvaa barghaishia iliyokuwa ikimkaa vyema? Viongozi wa Tanganyika leo wanaingia Zanzibar wamening'iniza misalabamizito ya dhahabu shingoni. Ilikuwa Wazanzibari watanabahi siku nyingi sana. Naomba nihitimishe kwa kunukuu maneno ya Dk. Harith Ghassany katika kitabu chake maarufu kuhusu Zanzibar, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru’’: ‘’Inavoonyesha, bado haijawadhihirikia Tanganyika watawala kuwa baada ya miaka 50 kuwa ipo haja kubwa kwa Tanganyika kuubadilisha mtizamo wake juu ya Zanzibar na kuupinduwa msimamo mkongwe wa kuinyanganya na kuinyima Zanzibar haki zake kwa kukhofia kuwa ikiwachiwa huru Zanzibar itakuwa ni tatizo la kimataifa kwa Tanganyika. Au Zanzibar itakuja kutumiliwa au kutumika kama ni mlango wa kuuingiza ubeberu wa Kiarabu na wa Kiislamu Tanganyika na Afrika ya Mashariki na ya Kati. Wako wengi wenye kuhadaika na udogo wa Zanzibar ingawa athari zake wanaziona lakini wameamuwa kuukataa ukweli huo. Anasema Jalaluddin Rumi “Yatizame macho yako. Ni madogo lakini yana uwezo wa kuyaona mambo makubwa.”
Umeanza kwa kutukumbusha kuwa kuna waislamu wanaobeba silaha kutetea dini yao. Kwa unafik mkubwa unajifanya kuwaachia wengine waamue kama wako sawa au la. Kwangu mimi naamini kuwa mtu yeyote anayeshindwa kukemea uovu yuko upande wake. Mtu yeyote anayepata kigugumizi kulaani matendo ya wakina Al Shaabab na Boko Haram, anawaunga mkono. Kwenye hili hatuna haja ya kuwasubiri hao maulamaa watuambie uko upande gani maana ni dhahiri utafurahi ikifika siku waislamu wenzako humu nchini wakibeba silaha kupigana na unachokiita mfumo kristu.Umelalamikia yale unayoona maovu yanayoendelea kufanywa na makafir dhidi ya waislamu. Umepandisha jazba ukifikiria kiburi cha Kafir kama Lukuvi kutamka bayana kuwa anahofia serikali ya kiislamu Zanzibar. Katika yote haya, hata mahali pamoja hukuwataja wakina Father Evaristus Mushi, Pastor Mathew Kachira, Joseph Mwang'amba,Sheikh Fadhil Soraga, Katie Gee na Kirstie Trup ambao ama wamepoteza maisha yao au kuharibiwa viungo vyao mwaka jana kisiwani Zanzibar. Bila shaka kwako wewe hawa ni "collateral damage" katika vita ya kulinda dini ya kiislamu. Kwako wewe hawa ni malipo tosha kwa wale waliopoteza maisha Mwembechai na Pemba! Bila shaka ukiwa na wenzako unawapongeza wale wote walionyanyua silaha zao na chupa zao za tindikali katika kulinda dini yao ya Uislamu.

Huyu binti amekosea alipoita hayo maandiko yako kuwa pumba. Maandiko yako ni zaidi ya pumba, ni maovu na yaliyojaa chuki na uchochezi dhidi ya wasio dini yako. Na ili tusikuchanganye na hao makafir wanaodai Tanganyika yako, unatukumbusha kuwa wazazi wako hawakutoka Tanganyika. Ndio maana hausiti kupandikiza sumu hapa maana una mahali pa kukimbilia! Uzuri tu ni kuwa watu waovu kama wewe kila siku wanashindwa. Hizi jitihada zako zitawafurahisha wafuasi wako humu ndani lakini wengi watakukwepa kama ukoma.

Amandla.......
 
naona ww umeahikiwa mawazo..na hao unao waita....mbona ww mvivu wa kuchambia mambo....inamaana hao ndo walokishikia msimamo.....nadhan...kwa mtindo huu kunabaadhi ya mambo yako ww na mkeo huwa unawaita watu wakusaidie pia au kama hujaoa huenda ukafanya hivyo.....acha uvivu na ututusa wa kufikir...jenga hoja nasio kuomba msaada na kukejel......u better stay calm
 
Mimi unishangaza sana dini inapotumika kuonyesha kuwa ilipigania uhuru wa Tanganyika. Nina hakika wahusika waliokuwa mstari wa mbele katika kudai uhuru wetu hawakusukumwa na dini zao bali nafsi zao kwa kuona udhalimu wa ukoloni. Ingekuwa ni dini ndiyo zilifanya hivyo, nafikiri sasa tungekuwa na tatizo kubwa. Tume one mataifa ambayo dini zimetumika kudai haki au uhuru, matunda yake yako dhairi!

Umeongea jambo nene sana. Mtoa mada ni mchochezi tu kama hao anaowapinga. Waliosaidia kudai uhuru hawakudai sababu wao ni wa dini fulani.Kama ni suala la kidini kwanini wamtangulize wa dini tofauti? Hawakuwa na mwenzao? Udini ni upofu na uhaba wa busara hata mtu uwe mzee wa miaka mia na mwenye ngozi yenye magaga.
 
Mzee Said, Salaam.

Naomba nikushukuru kwa michango yako kuhusu muungano.
Mimi binafsi nashukuru kwa kuweza kunifungua sana juu ya masuala ya nchi ya Tanganyika.

Tatizo watu awana positive minds wana bisha pasipo kuwa na facts wakieleweshwa wanakimbili "m-dini"....
 
Back
Top Bottom