Mzee Mag3,
Sasa hujioni kwa attitude kama hii unakua umejifungia ndani ya box lako pekee!?...yaani unaogopa kuchomoka humo ndani ya comfort zone yako,au!?
Kwahiyo unataka kutuaminisha yakua watu takriban woote ambao weye unawapa chance ya kufanza nao majadiliano ya kitaaluma au hata ya kawaida...ni wale tu wenye mitazamo amma fikra zishabihianazo na zako!? Daah!
Sasa weye kama unadai yakua huyu Maalim Mohamed Said, ati ni "mtu hatari" sana kwa "Taifa lenu"!?...pia ni mtu "anaesababisha" migongano ndani ya nchi na shutuma nyanginezo kadhaa...ambazo mpaka kesho hamuwezi/mmeshindwa kuzithibitisha!? Je unakhis hivi kumkimbia na huku ati kususia kufanza nae mijadala ndo itaepusha hizo "hatari",mnazodai analeta hapo nchini!?
Kwanini msifanze ile positive engangement, which may lead into meaningful/constructive discussion with logical arguments,au!?
Mie binafsi nakhis weye kuamua kungia mitini, au kujaribu kumbeza mtu mzima na Mwanataaluma mwanzio Maalim Mohamed Said...basi hiyo yako ni irresponsible attitude na huna uzalendo asilan!...yaani unakimbia wajibu wako kwa Taifa,au!?
Tafadhali rejea hapa jamvini...njoo uje kuzungumza masuala yanayokhusu mustakabala wa Taifa na Wananchi wangine!
Hao Waislam au huyo Maalim Mohamed Said...ndo wenzenu hapo nchini hata mkifanza lolote/chochote...watabaki tu kuwa miongoni mwa Watanzania wenzenu! Sasa badili dasturi na uanze some sort of reconciliation and/or positive engagement with Maalim Mohamed Said!?
Hivi kama nyinyi Watanzania wenzetu ambao ndo wasomi wa Taifa hili na ndio tegemeo letu, yaani mnashindwa hata kuwa-flexible and tolerable to each other!?.... Je sisi Wananchi/Watanzania wenzenu wa hali ya chini tulio wengi, khasa sisi tulio huku vijijini na bila ya elimu ya kutosha!...je tufanze nini,jamani!? Daah!
Natumai utanifahamu japo kiduchu...na utaacha kusikiza hawa watoto waduchu hapa jamvini wenye kukuzidishia farka na migongano!
Ahsanta sana.