Kutoka Kutaka Kuwa Mwandishi wa Habari na Kuishia Kuwa Mhandisi!....Je na Kwako MwanaJF ikoje Hii?

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Huenda Labda ni Mwl Wangu wa Maarifa ya Jamii aliniinfluence katika Hili.
Nilikuwa nawezea Kabisa kuigiza sauti na kutangaza Habari katika Maigizo yetu ya shule ya Msingi

Kweli nilikuwa na Nyota ya Kukubalika Maana kila mtu alionekana kuvutiwa na Mimi, nikawa maarufu saana na kila mmoja akaniita Mwandishi wa Habari, Hakika ilikuwa Faraja kubwa kwangu na ikazidi kuniongezea moyo wa kutaka kuingia katika hio career.

Nilienda kusoma shule Moja ya sekondari Mjini Moshi, wakati natoka nyumbani Arusha sikuwahi kufikiria kama katika hii nchi kuna baadhi ya shule hazifundishi Masomo ya Historia!

Ni jambo lililowahi kunivunja moyo katika kipindi changu nasoma o level, maana ndoto yangu ilikuwa nisome HKL/HGL nije kuwa Mwandishi wa Habari...Loooh kwa Bahati Mbaya sikukuta History katika Hio shule!

Kwa kuwa nilikuwa mtata wa Hesabu na Sayansi nikaamua kukomaa na masomo ya sayansi na arts sikuipenda tena maana hakuna historia na sikuona tena msingi wa masomo ya sanaa bila Historia!

Nakumbuka Nilitokea kuwa mtataa wa Somo linaitwa Engineering Science, Kila mtu akaanza kuniita Engineer, then nikawa Motivated kutaka kuja kuwa Engineer.

Safari Hii nikasema lazima nipambane hii ndoto haiwezi kufa kibudu kama ile ingine ilivokufa, kweli na Mungu si Athumani Nikafanikiwa kufaulu vema kwenda kidato cha 5 Kusoma Mchepuo wa PCM yaani Physics, Chemistry na Mathematics na kufanikiwa kufaulu kwa daraja la kwanza.

Mungu akanijalia Kufanikiwa kusoma Chuo Kikubwa Hapa Nchini Nkichukua Kozi ya Uhandisi wa Ujenzi, Japo sijutii ila kila mara nikikumbuka kwamba nilitamanigi kuwa Mwandishi wa Habari ila nilishindwa Kutimiza Hizi Ndoto Basi Najikuta Roho Inauma saana!

Je Na wewe MwanaJF ulishatamani kuwa katika Career Gani ila ukaishia kufanya Career Ingine!
 
Nilitamani sana kuwa Mwandishi wa habari kama wewe ila niliishia kusomea chuo kikuu Ualimu, ambao nao niligoma kuufanyia kazi nikaamua kufanya biashara za hapa na pale.
 
Hongera sana mkuu,tunasema hicho ndicho ulichopangiwa tena hiyo kazi unaweza ukawa freelancer no strings attached

Me napenda niwe IGP
 
Hata mimi nilipenda Kazi ya habari na nilikuwa naigiza sauti za maripota mbalimbali akiwemo Stephen Chuwa wa ITV,Na mimi nikapangiwa shule ya Ufundi mkoani Iringa kwa sasa ni mhandisi pia.
 
Huenda Labda ni Mwl Wangu wa Maarifa ya Jamii aliniinfluence katika Hili.
Nilikuwa nawezea Kabisa kuigiza sauti na kutangaza Habari katika Maigizo yetu ya shule ya Msingi

Kweli nilikuwa na Nyota ya Kukubalika Maana kila mtu alionekana kuvutiwa na Mimi, nikawa maarufu saana na kila mmoja akaniita Mwandishi wa Habari, Hakika ilikuwa Faraja kubwa kwangu na ikazidi kuniongezea moyo wa kutaka kuingia katika hio career.

Nilienda kusoma shule Moja ya sekondari Mjini Moshi, wakati natoka nyumbani Arusha sikuwahi kufikiria kama katika hii nchi kuna baadhi ya shule hazifundishi Masomo ya Historia!

Ni jambo lililowahi kunivunja moyo katika kipindi changu nasoma o level, maana ndoto yangu ilikuwa nisome HKL/HGL nije kuwa Mwandishi wa Habari...Loooh kwa Bahati Mbaya sikukuta History katika Hio shule!

Kwa kuwa nilikuwa mtata wa Hesabu na Sayansi nikaamua kukomaa na masomo ya sayansi na arts sikuipenda tena maana hakuna historia na sikuona tena msingi wa masomo ya sanaa bila Historia!

Nakumbuka Nilitokea kuwa mtataa wa Somo linaitwa Engineering Science, Kila mtu akaanza kuniita Engineer, then nikawa Motivated kutaka kuja kuwa Engineer.

Safari Hii nikasema lazima nipambane hii ndoto haiwezi kufa kibudu kama ile ingine ilivokufa, kweli na Mungu si Athumani Nikafanikiwa kufaulu vema kwenda kidato cha 5 Kusoma Mchepuo wa PCM yaani Physics, Chemistry na Mathematics na kufanikiwa kufaulu kwa daraja la kwanza.

Mungu akanijalia Kufanikiwa kusoma Chuo Kikubwa Hapa Nchini Nkichukua Kozi ya Uhandisi wa Ujenzi, Japo sijutii ila kila mara nikikumbuka kwamba nilitamanigi kuwa Mwandishi wa Habari ila nilishindwa Kutimiza Hizi Ndoto Basi Najikuta Roho Inauma saana!

Je Na wewe MwanaJF ulishatamani kuwa katika Career Gani ila ukaishia kufanya Career Ingine!

Ayse! wakati mwingine wengi huwa wanasomea wasichokipenda kutokana na sababu mbalimbali. Hilo kwa kiasi fulani ilinikuta na mimi, nikaenda kusomea kitu nisichokipenda Chuo. Nilitamani sana kusome Uchumi chuo kikuu, form IV nilipiga one kali tu, nikaenda kusoma mchepuo wangu ninaoupenda wa EGM, Six niukatoka na one ya 9 nikiwa na C ya Economics na C ya Advance Mathematics. Nika apply UDSM BA Economics ile double intake ya 2005/2006, nikambiwa nipo below cut off kwa wanaume. Roho iliniuma ile mbaya, next academic year nikaenda kusome Bachelor of Development Planning hivo hivo kibishi ingawa haipo katika moyo kabisa. kwa vile course hii ina vikozi kozi vingi vya Economics na Statistics za kutosha basi nikawa navikwangua sawasawa maana Calculus ilishakaa vizuri kichwani. basi nikatoa na ufaulu mkubwa tu, nikaingia serikali. baada ya mwaka na nusu nikapewa na scholarship na SUA kusomea MSc. Agricultural Econimics. Nashukuru kuifikia ndoto yangu ya kufanya kazi na wachumi, leo nipo ofisi kubwa nikifanya kazi na wachumi katika Klasta ya Uchumi Jumla (Macro Economics).
 
Nilitamani sana tangia nipo primary kuwa doctor but nilipofika form two tukakosa ticha wa biology nikaamua kukomaa na phyisics, chemistry na math... Hadi leo ni mhandisi umeme
 
Hata mimi nilipenda Kazi ya habari na nilikuwa naigiza sauti za maripota mbalimbali akiwemo Stephen Chuwa wa ITV,Na mimi nikapangiwa shule ya Ufundi mkoani Iringa kwa sasa ni mhandisi pia.
Hahahaa sasa Mkuu unajisikiaje
 
Ayse! wakati mwingine wengi huwa wanasomea wasichokipenda kutokana na sababu mbalimbali. Hilo kwa kiasi fulani ilinikuta na mimi, nikaenda kusomea kitu nisichokipenda Chuo. Nilitamani sana kusome Uchumi chuo kikuu, form IV nilipiga one kali tu, nikaenda kusoma mchepuo wangu ninaoupenda wa EGM, Six niukatoka na one ya 9 nikiwa na C ya Economics na C ya Advance Mathematics. Nika apply UDSM BA Economics ile double intake ya 2005/2006, nikambiwa nipo below cut off kwa wanaume. Roho iliniuma ile mbaya, next academic year nikaenda kusome Bachelor of Development Planning hivo hivo kibishi ingawa haipo katika moyo kabisa. kwa vile course hii ina vikozi kozi vingi vya Economics na Statistics za kutosha basi nikawa navikwangua sawasawa maana Calculus ilishakaa vizuri kichwani. basi nikatoa na ufaulu mkubwa tu, nikaingia serikali. baada ya mwaka na nusu nikapewa na scholarship na SUA kusomea MSc. Agricultural Econimics. Nashukuru kuifikia ndoto yangu ya kufanya kazi na wachumi, leo nipo ofisi kubwa nikifanya kazi na wachumi katika Klasta ya Uchumi Jumla (Macro Economics).
Hongera sana boss
 
Me nilitamani kua leading Graphics Designer,videographer&colorist bt vifaa vilinikwamisha nimeishia kuwa mtayarishaji wa baadhi ya Gospel tracks mnazozisikia..huko mitaani
 
Kila mtu shule ya msingi akiulizwa anataka awe nani utasikia majibu mawili tu,
Udaktari na Rubani, lkn kadri siku zinasonga kila kitu kinagoma.
Mwishoe tunajikuta kwenye hizi fani za mwendo kasi
 
Nilitamani sana kuwa daktari na nilifaulu vizuri zaidi mchepuo wa PCB ingawa kwenye kujaza fomu za mwisho nikachagua kusoma PCM kisa tu nina uoga flani wa wagonjwa,yaani mtu hata ajikate na wembe siangalii au hata mwanangu akiwa anachomwa sindano siangalii na akitoka analia natamani nilie pia.

Baada ya kusoma PCM,nikatamani sana niwe mhandisi wa umeme lakini bahati mbaya mwaka wetu ule ufaulu haukuwa mbaya sana ingawa kwangu nikakwama kwa kutofika point za kusoma hiyo course katika chuo nilichotaka,nikahamia Computer Science basi ndo hivyo tena sasa hv ni mtaalamu wa Ms Word...teh teh teh!
 
Nilipenda sana utangazaji mpira na u-Dj lkn nikakwama nafanya mengine lakini mpaka sasa nawazia nifanyeje nifikie azima yangu
 
Huenda Labda ni Mwl Wangu wa Maarifa ya Jamii aliniinfluence katika Hili.
Nilikuwa nawezea Kabisa kuigiza sauti na kutangaza Habari katika Maigizo yetu ya shule ya Msingi

Kweli nilikuwa na Nyota ya Kukubalika Maana kila mtu alionekana kuvutiwa na Mimi, nikawa maarufu saana na kila mmoja akaniita Mwandishi wa Habari, Hakika ilikuwa Faraja kubwa kwangu na ikazidi kuniongezea moyo wa kutaka kuingia katika hio career.

Nilienda kusoma shule Moja ya sekondari Mjini Moshi, wakati natoka nyumbani Arusha sikuwahi kufikiria kama katika hii nchi kuna baadhi ya shule hazifundishi Masomo ya Historia!

Ni jambo lililowahi kunivunja moyo katika kipindi changu nasoma o level, maana ndoto yangu ilikuwa nisome HKL/HGL nije kuwa Mwandishi wa Habari...Loooh kwa Bahati Mbaya sikukuta History katika Hio shule!

Kwa kuwa nilikuwa mtata wa Hesabu na Sayansi nikaamua kukomaa na masomo ya sayansi na arts sikuipenda tena maana hakuna historia na sikuona tena msingi wa masomo ya sanaa bila Historia!

Nakumbuka Nilitokea kuwa mtataa wa Somo linaitwa Engineering Science, Kila mtu akaanza kuniita Engineer, then nikawa Motivated kutaka kuja kuwa Engineer.

Safari Hii nikasema lazima nipambane hii ndoto haiwezi kufa kibudu kama ile ingine ilivokufa, kweli na Mungu si Athumani Nikafanikiwa kufaulu vema kwenda kidato cha 5 Kusoma Mchepuo wa PCM yaani Physics, Chemistry na Mathematics na kufanikiwa kufaulu kwa daraja la kwanza.

Mungu akanijalia Kufanikiwa kusoma Chuo Kikubwa Hapa Nchini Nkichukua Kozi ya Uhandisi wa Ujenzi, Japo sijutii ila kila mara nikikumbuka kwamba nilitamanigi kuwa Mwandishi wa Habari ila nilishindwa Kutimiza Hizi Ndoto Basi Najikuta Roho Inauma saana!

Je Na wewe MwanaJF ulishatamani kuwa katika Career Gani ila ukaishia kufanya Career Ingine!
Wewe ulisoma Moshi Tech. Japo umekwepa kusema hilo wazi.

Mimi nilisoma Tanga Tech, Umenikumbusha somo la Engineering Science
 
Mimi moyo wangu ulikuwa ni kusoma computer science vitisho vya watu na vilinifanya nijiingize kuapply kozi za afya tcu wakanitupa first round ...second round nikajikuta nipo SUA nasomea vitu ambavyo sikuwahi kufikiria maishani mwangu ila kwakuwa nilipata mkopo nikaona siyo mbaya kwa wakat huo
 
Back
Top Bottom