Kutoka Kutaka Kuwa Mwandishi wa Habari na Kuishia Kuwa Mhandisi!....Je na Kwako MwanaJF ikoje Hii?

Kutoka Kutaka Kuwa Mwandishi wa Habari na Kuishia Kuwa Mhandisi!....Je na Kwako MwanaJF ikoje Hii?

Nilitamani sana kuwa katibu mkuu wizara ya fedha.

Saa hizi nalima majaruba ya mpunga huku mpanda
 
Nilitamani sana kuwa katibu mkuu wizara ya fedha.

Saa hizi nalima majaruba ya mpunga huku mpanda
 
Huenda Labda ni Mwl Wangu wa Maarifa ya Jamii aliniinfluence katika Hili.
Nilikuwa nawezea Kabisa kuigiza sauti na kutangaza Habari katika Maigizo yetu ya shule ya Msingi

Kweli nilikuwa na Nyota ya Kukubalika Maana kila mtu alionekana kuvutiwa na Mimi, nikawa maarufu saana na kila mmoja akaniita Mwandishi wa Habari, Hakika ilikuwa Faraja kubwa kwangu na ikazidi kuniongezea moyo wa kutaka kuingia katika hio career.

Nilienda kusoma shule Moja ya sekondari Mjini Moshi, wakati natoka nyumbani Arusha sikuwahi kufikiria kama katika hii nchi kuna baadhi ya shule hazifundishi Masomo ya Historia!

Ni jambo lililowahi kunivunja moyo katika kipindi changu nasoma o level, maana ndoto yangu ilikuwa nisome HKL/HGL nije kuwa Mwandishi wa Habari...Loooh kwa Bahati Mbaya sikukuta History katika Hio shule!

Kwa kuwa nilikuwa mtata wa Hesabu na Sayansi nikaamua kukomaa na masomo ya sayansi na arts sikuipenda tena maana hakuna historia na sikuona tena msingi wa masomo ya sanaa bila Historia!

Nakumbuka Nilitokea kuwa mtataa wa Somo linaitwa Engineering Science, Kila mtu akaanza kuniita Engineer, then nikawa Motivated kutaka kuja kuwa Engineer.

Safari Hii nikasema lazima nipambane hii ndoto haiwezi kufa kibudu kama ile ingine ilivokufa, kweli na Mungu si Athumani Nikafanikiwa kufaulu vema kwenda kidato cha 5 Kusoma Mchepuo wa PCM yaani Physics, Chemistry na Mathematics na kufanikiwa kufaulu kwa daraja la kwanza.

Mungu akanijalia Kufanikiwa kusoma Chuo Kikubwa Hapa Nchini Nkichukua Kozi ya Uhandisi wa Ujenzi, Japo sijutii ila kila mara nikikumbuka kwamba nilitamanigi kuwa Mwandishi wa Habari ila nilishindwa Kutimiza Hizi Ndoto Basi Najikuta Roho Inauma saana!

Je Na wewe MwanaJF ulishatamani kuwa katika Career Gani ila ukaishia kufanya Career Ingine!
Ulimaliza mwaka gan pale Mo tech?
 
Mimi nilitamani kuwa kama Dr shika ila sasa nimebaki kubet tu
 
Dah....Nilipenda sana mambo ya uchawi na ufugaji majini.....nimejikuta naishia kuwa mpigakura tu[emoji13] [emoji87]
Hahaha[emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16]nimecheka Sana Mkuu Hope Ndoto Yako Itatimia
 
Naamini kwa sababu bado nipo hai ndoto yangu itatimia tu japo vikwazo vingi ila ipo siku sita kata tamaa kama Dr. Shika aliepata umaarufu enzi za uzee wake.
 
Naamini kwa sababu bado nipo hai ndoto yangu itatimia tu japo vikwazo vingi ila ipo siku sita kata tamaa kama Dr. Shika aliepata umaarufu enzi za uzee wake.
Amini Mkuu, Nothing is imposible!
 
Back
Top Bottom