Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Perfect,Kilichonikosha kwenye hii habari ni kuwa MWAKA 1967 kuna watanzania walikuwa wameanza kukata keki aseee...
Mkuu unasema kweli?Asee hongera sana kaka maana miaka hiyo kula keki kubwa kama hiyo ilikuwa ni nadra sana.Perfect,
Kumbuka kuwa huyo aikuwa ni mtoto wa chief.
Mimi binafsi hiyo ndiyo ilikuwa ni party yangu ya kwanza kuhudhuria
maishani mwangu.
Huwa nikikutana na Chief Edward Makwaia sasa tu watu wazima
huwa tunakumbushana mengi ya utoto.
Huwa namwambia, ''Unajua Teddy wewe ndiye uliyeniingiza mimi
katika music wa James Brown nk. nk...''
Basi yeye huwa kimya.
Katika miaka ya 1960s kulikuwa na ''music craze,'' inaitwa, ''Soul Music.''
Vijana tuliingia wazimu.
Bingwa wa muziki huu alikuwa James Brown.
Baadhi yetu vijana wa Kariakoo tulichelewa kupokea muziki huu tulikuwa
bado na Elvis Presley na Cliff Richard.
Huwa simwachi Teddy nitamwambia jambo jingine ambalo mimi sikuwanalo
kabla ya kukutanane.
Basi sasa atacheka kisha atasema, ''Oh! unajua Sidney mimi nimejifunza
mengi pia kutoka kwako...''
Ninachotaka kukuambia kuwa kulikuwa na utamaduni mpya mara tu baada ya
Waingereza kuondoka ingawa mizizi ya utamaduni huu mizizi yake ni ukoloni
wa Waingereza.
Utamaduni huu uliingiza katika jamii tabaka jipya la Waafrika walionufaika kwa
kushika nafasi za Waingereza pale walipoondoka.
Wazazi wetu waliathirika na mageuzi haya mapya na sisi watoto hatukusalimika
pia.
Perfect,Mkuu unasema kweli?Asee hongera sana kaka maana miaka hiyo kula keki kubwa kama hiyo ilikuwa ni nadra sana.
Maalim Faiza,
Nami ndipo nikaona hebu nililete hili jambo Majlis.
Lakini haya yote kijana anachomwa na ule ukweli kuwa hiyo TANU
hapo kwa Hamza na Abdul ndipo kwake.
Hana jingine la kufanya ila achokonoe hata pale alipopewa jibu na
mwenye mali.
Companero,Mzee Said, maswali yangu kwako huwa nayauliza kwa nia njema ili yanisaidie kwenye utafiti wangu. Balozi Juma hadhani kama hiyo mikutano ilikuwa inafanyika kwenye nyumba yao ya Ilala Quarter maana ilikuwa ndogo sana. Pia hana uhakika kama ilifanyika kwenye ofisi ya Ilala Boma maana ilikuwa ni ya Serikali.
Kwa ufupi, sote tunakubaliana kwamba mikutano ilifanyika. Tunachotoka - ama ninachotaka mimi - kujua ni wapi hasa, nyumbani kwa Hamza, ofisini kwake au sehemu nyingine ya mafichoni huko Ilala kama Balozi anavyohisi?
Msaada tafadhali, kama nilivyosema, yote nauliza kwa nia njema - naona safari hii hata Maalim Faiza kaliona hilo.