Mzee Said, maswali yangu kwako huwa nayauliza kwa nia njema ili yanisaidie kwenye utafiti wangu. Balozi Juma hadhani kama hiyo mikutano ilikuwa inafanyika kwenye nyumba yao ya Ilala Quarter maana ilikuwa ndogo sana. Pia hana uhakika kama ilifanyika kwenye ofisi ya Ilala Boma maana ilikuwa ni ya Serikali.
Kwa ufupi, sote tunakubaliana kwamba mikutano ilifanyika. Tunachotoka - ama ninachotaka mimi - kujua ni wapi hasa, nyumbani kwa Hamza, ofisini kwake au sehemu nyingine ya mafichoni huko Ilala kama Balozi anavyohisi?
Msaada tafadhali, kama nilivyosema, yote nauliza kwa nia njema - naona safari hii hata Maalim Faiza kaliona hilo.
Companero,
Nijuavyo mimi na nimeandika kwingi kuwa mikutano ikifanyika Ilala Welfare Centre.
Mimi sijapata kusema ikifanyika nyumbani kwa
Hamza Mwapachu.
Wala mimi sijasema mikutano ilikuwa ikifanyika Ilala Boma.
Mikutano mingine ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa
Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na
Sikukuu.
Hii nyumba naifahamu vizuri sana ni nyumba yenye nafasi na hadhi kwa wakati ule.
Katika
Nyaraka za Sykes nimekuta dondoo za mkutano wa Tanganyika African
Government Servants Asociation (TAGSA) uliofanyika hapa uliohudhuriwa na
Ally Sykes, Thomas Marealle, Rashid Kawawa, Stephen Mhando, Othman
Chande na
Leonard Bakuname.
(
Ally Sykes TAGSA Honorary Secretary, to The Honourable Chief Secretary to the
Government; Ref. No. 1/52/3 10 January, 1952).
Sasa huyu aliyeniambia kuwa wakifanya mikutano nyumbani kwa
Abdul Sykes ndiye
huyu aliyeniambia kuwa mikutano mingine wakifanya Ilala Welfare Centre.
Kuna mikutano mingine ikifanyika Mtaa wa Pemba lakini sikuweza kujua khasa ni
katika nyumba ipi ingawa nahisi inaweza ikawa kwa
Maalim Sakina Biti Arab.
Ninaloweza kusema ni kuwa mkutano muhimu uliohudhuriwa na
Sheikh Hassan bin
Amir, Sheikh Abdallah Chaurembo, Sheikh Nurdin Hussein, Rajab Diwani
ulifanyika usiku hapo Mtaa wa Pemba na ni katika mkutano huu ndipo
Sheikh
Hassan bin Amir alieleza umuhimu wa kufuta ''symbols'' zote za Uislam katika TANU ili
TANU iepukane na haiba ya kuwa ni chama cha Waislam.
Nyumba ya
Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu ni hiyo hapo chini ingawa
imefanyiwa mabadiliko kidogo kwa kuwekwa milango ya maduka katika miaka
ya 1980s: