carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Nimesikiliza hotuba yako ya leo. Na hapo kwenye maandamano umepotea kabisa.
Unawaweka wanaharakati mstari wa mbele kana kwamba wao ndio chanzo cha hasira ya wananchi. Hapana.
Wanaohamasisha maandamano ni CCM wenyewe. Na sio kwa maneno, bali kwa vitendo vyao vya kila siku.
Maandamano hayajaja kutoka Twitter. Yamekuja kutoka kwenye haya:
1. Kukataa mabadiliko ya sheria za uchaguzi na Tume Huru. Watu wanaomba miaka yote, jibu ni "hapana". Mnategemea nini?
2. Kuteka na kupoteza watu. Watu wanachukuliwa, wanapotea, na serikali inanyamaza.
3. Kutoa vitisho kabla ya uchaguzi. Rejea hotuba zao Lema, utanielewa. Lugha ilikuwa ya kutisha wananchi, sio ya kuomba kura.
4. Kubambikizia watu kesi. Kesi zimegeuzwa kuwa rungu la kisiasa.
5. Kukata viongozi waliopendekezwa na Halmashauri Kuu na kukosa demokrasia ndani ya chama chao. Hata mgombea wa Urais alivyopatikana, kila mtu aliona hakukuwa na demokrasia. Mkiwa hamna demokrasia ndani, mtaleta demokrasia gani nchini?
6. Wizi uliokithiri wa mali za umma. Mkataba wa bandari, mikataba ya madini, na sakata la Ngorongoro. Hizo ndizo zinawasha hasira kuliko post yoyote ya mwanaharakati.
7. Maisha ya kifahari ya viongozi na familia zao wakati Watanzania wanaogelea kwenye umasikini wa kutupwa. Tabaka mbili tofauti, nchi moja.
8. Kudharau wananchi. Mwananchi akilalamika anaambiwa ni mchochezi.
9. Vyeo vya kupeana. Ajira na vyeo vimekuwa vya familia na marafiki, sio kwa sifa.
10. Ukosefu wa ajira. Vijana wamejaa mtaani, digrii mifukoni, lakini kazi hakuna.
Sasa hapo wanaharakati wanahusikaje?