Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Mchoro wa karne ya 16 unaoonyesha kuchunwa ngozi akiwa hai kwa hakimu fisadi, Sisamnes, katika mwaka wa 500BC.
Sisamnes alikuwa hakimu wa kifalme fisadi wakati wa Cambyses ll katika taifa la Uajemi. Iligundulika kuwa alichukua hongo/rushwa mahakamani na akatoa hukumu isiyo ya haki. Kwa sababu hiyo mfalme akaamuru akamatwe kwa ufisadi wake na akaamuru achunwe ngozi akiwa hai.
Kabla ya kutoa hukumu mfalme alimuuliza Sisamnes ni nani alitaka kumteua kama mrithi wake. Sisamnes, kwa uchoyo wake, alimchagua mwanawe, Otanes.
Mfalme alikubali na kumteua Otanes kuchukua nafasi ya baba yake. Baadaye alitoa hukumu na kuamuru kwamba ngozi iliyoondolewa ya Sisamnes itumike kuwamba kiti ambacho hakimu mpya angekalia kortini ili kumkumbusha madhara yanayoweza kusababishwa na ufisadi.
Otanes, katika mashauri yake, alilazimika kukumbuka daima kwamba alikuwa ameketi kwenye ngozi ya baba yake aliyeuawa. Hii ilisaidia kuhakikisha haki na usawa katika vikao vyake vyote, mijadala na hukumu
Somo la haki kwa watoa hukumu wetu.. Je umejifunza kitu hapa?