Kutoka maktaba: Hakimu aliyechunwa ngozi kwa ufisadi

Kutoka maktaba: Hakimu aliyechunwa ngozi kwa ufisadi

tushukuru sana tupo karne hii ukiguswa kidogoo unapi yoweee dunia zima inasikia..
Maweee!1 muone huyu!! Lisu yuko wapi?? unajua yaliyo mkuta?? unadhani ataandikwaje miaka ya mbele huko??.........km haitoshi muheshimiwa Nape?? je.......

Hayaaa wafanya kazi wa serikali kuachishwa km madogi bila kujali huduma zao!!........haya waziri kaenda kuapishwa matokeo yake anafukuzwa km dogi mweeee!!........

Raisi kujitungia sheria zinazo mlinda unadhani ataandikwaje huko mbele???....viongozi wezi kuiba hela wananunua mabasi tena mchana kweupeeee!!

na aliye fanya hayo kafa kifo kibaya sana ....huko mbele ataandikwaje??....Nina mengi mpaka yale ya Zanzibar,,,na aliye sababisha amesha vuta na yeye!!
 
Mchoro wa karne ya 16 unaoonyesha kuchunwa ngozi akiwa hai kwa hakimu fisadi, Sisamnes, katika mwaka wa 500BC.

Sisamnes alikuwa hakimu wa kifalme fisadi wakati wa Cambyses ll katika taifa la Uajemi. Iligundulika kuwa alichukua hongo/rushwa mahakamani na akatoa hukumu isiyo ya haki. Kwa sababu hiyo mfalme akaamuru akamatwe kwa ufisadi wake na akaamuru achunwe ngozi akiwa hai.

Kabla ya kutoa hukumu mfalme alimuuliza Sisamnes ni nani alitaka kumteua kama mrithi wake. Sisamnes, kwa uchoyo wake, alimchagua mwanawe, Otanes.

Mfalme alikubali na kumteua Otanes kuchukua nafasi ya baba yake. Baadaye alitoa hukumu na kuamuru kwamba ngozi iliyoondolewa ya Sisamnes itumike kuwamba kiti ambacho hakimu mpya angekalia kortini ili kumkumbusha madhara yanayoweza kusababishwa na ufisadi.

Otanes, katika mashauri yake, alilazimika kukumbuka daima kwamba alikuwa ameketi kwenye ngozi ya baba yake aliyeuawa. Hii ilisaidia kuhakikisha haki na usawa katika vikao vyake vyote, mijadala na hukumu

Somo la haki kwa watoa hukumu wetu.. Je umejifunza kitu hapa?

View attachment 2312625
Ha!
JamiiForums257891467.gif

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka 500 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, jaji mla rushwa aliyeitwa Susamne alihukumiwa na kuchunwa ngozi akiwa hai. Hii ilitokea wakati wa utawala wa Cambyses II wa Uajemi(Persia).

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya kugundulika kuwa alipokea rushwa mahakamani na kutoa hukumu isiyo ya haki.

Mfalme aliamuru jaji kukamatwa kwa uhalifu huo na kuchunwa ngozi akiwa hai. Lakini kwa kuwa nafasi ya ujaji ilikuwa cheo kilichorithiwa na jaji mwenyewe alikuwa kabla ya hukumu, mfalme alimpa jaji fursa ya kuteua mrithi wa kiti chake naye akamteua mwanawe anayejulikana kama Otanes.

Kisha mfalme alikubaliana na pendekezo hilo na akamteua Otanes kumrithi baba yake na kisha Otanes akatoa hukumu kwa baba yake na ngozi hiyo ikatumika kufunika kiti cha jaji mpya (Otanes) ili kila anapoketi juu yake akumbuke uovu wa ufisadi.

Otanes, kila alipokuwa akifanya maamuzi, alikumbuka kuwa daima aliishi katika ngozi ya baba yake, ambayo ilimfanya awe mwadilifu sana katika hukumu na utoaji wa adhabu.
 
Ndicho wanapaswa kufanyiwa wabunge wetu na baadhi ya viongozi wa juu
 
Mchoro wa karne ya 16 unaoonyesha kuchunwa ngozi akiwa hai kwa hakimu fisadi, Sisamnes, katika mwaka wa 500BC.

Sisamnes alikuwa hakimu wa kifalme fisadi wakati wa Cambyses ll katika taifa la Uajemi. Iligundulika kuwa alichukua hongo/rushwa mahakamani na akatoa hukumu isiyo ya haki. Kwa sababu hiyo mfalme akaamuru akamatwe kwa ufisadi wake na akaamuru achunwe ngozi akiwa hai.

Kabla ya kutoa hukumu mfalme alimuuliza Sisamnes ni nani alitaka kumteua kama mrithi wake. Sisamnes, kwa uchoyo wake, alimchagua mwanawe, Otanes.

Mfalme alikubali na kumteua Otanes kuchukua nafasi ya baba yake. Baadaye alitoa hukumu na kuamuru kwamba ngozi iliyoondolewa ya Sisamnes itumike kuwamba kiti ambacho hakimu mpya angekalia kortini ili kumkumbusha madhara yanayoweza kusababishwa na ufisadi.

Otanes, katika mashauri yake, alilazimika kukumbuka daima kwamba alikuwa ameketi kwenye ngozi ya baba yake aliyeuawa. Hii ilisaidia kuhakikisha haki na usawa katika vikao vyake vyote, mijadala na hukumu

Somo la haki kwa watoa hukumu wetu.. Je umejifunza kitu hapa?

View attachment 2312625
Hizi ni riwaya au uhalisia?

Binadamu achunwe ngozi bila ganzi halafu ayastahimili maumivu hayo mpaka zoezi litakapomalizika au walichuna ngozi huyo jaji akiwa amekwisha kufariki, yaani walichuna ngozi maiti?
 
Duuuh kabla ya Yesu, kwahiyo hata Yuda hakuogopa kusikia historia hiyo😀😀
 
Hizi ni riwaya au uhalisia?

Binadamu achunwe ngozi bila ganzi halafu ayastahimili maumivu hayo mpaka zoezi litakapomalizika au walichuna ngozi huyo jaji akiwa amekwisha kufariki, yaani walichuna ngozi maiti?
Ni simulizi sio hadithi, simulizi ni matukio halisi hadithi ni matukio ya kufikirika na kutunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom