Kutoka maktaba ya Juma Mwapachu: Barua ya baba yake kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere 1949

Kutoka maktaba ya Juma Mwapachu: Barua ya baba yake kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere 1949

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074

Barua ya Hamza Mwapachu kwa Julius Nyerere 1949


Hamza Kibwana Mwapachu

Balozi Hamza Mwapachu ameiweka hadharani barua ya baba yake Hamza Kibwana Mwapachu (1913 – 1962) aliyomwandikia Julius Nyerere mwaka wa 1949.

Barua hii sasa karibu itafikia miaka 70.

Sababu ya kuiweka barua hii nadhani ni kutaka kulizindua taifa kuhusu kupotoshwa kwa historia ya wananchi wa Tanganyika katika kujikomboa kutoka makucha ya ukoloni wa Waingereza.

Kumekuwa na tatizo kubwa sana katika kutafiti na kuiandika kwa sawa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Takriban yote yaliyoandikwa kuhusu historia hii yamemtaja Julius Nyerere peke yake kiasi cha kufanya iaminike kuwa kabla yake hapakuwa na wanasiasa wala hapakuwapo na juhudi zozote za kutaka kuikomboa Tanganyika kutoka katika ukoloni.

Mwelekeo huu uneifanya nchi ikose mashujaa wake.

Jambo la kusikitisha ni kuwa na pale inapojaribiwa ingawa kwa kuchelewa kuwaenzi mashujaa waliopambana na ukoloni maswali mengi hujitokeza ambayo hakuna awezaye kuyajibu kwa uhakika na kwa ithibati ya kuaminika.

Mathalan inawezekanaje ikatolewa Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa Abdulwahid na Ally Sykes, ndugu wawili waliokuwa kati ya waasisi 17 wa TANU ukawaacha waasisi wengine kama Saadan Abdul Kandoro na Japhet Kirilo kwa kuwataja wachache.

Itoshe tu kueleza kuwa medali hizi zimetolewa kwa kuchelewa miaka 50.

Ally Sykes kapokea medali yake akiwa katika miaka yake ya mwisho wa maisha yake,akiwa mgonjwa, miaka miwili kabla ya kifo chake mwaka 2013.

Lakini swali linakuja vipi utawapa medali mashujaa hawa wa uhuru usimpe medali Hamza Mwapachu ambae ushahidi wa historia unaonyesha kuwa ndiyo alikuwa, ‘’mentor,’’ wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Abdul Sykes na mwalimu wao hawa wote waliokuja kudai uhuru katika nafasi zao tofauti na baada ya uhuru kupatikana wakaja kuwa viongozi wa Tanganyika huru?

Dr. Vedasto Kyaruzi alipatapo kumwambia Juma Mwapachu kuwa kama si mpango walioweka Hamza Mwapachu na Abdul Sykes Tanganyika isingepata uhuru mwaka wa 1961.

Dr. Kyaruzi akaongeza kwa kumwambia Juma kuwa kule Nansio kisiwani alikopelekwa baba yake na Waingereza ile ilikuwa jela kumtia kizuizini kumzuia asishiriki katika siasa.

Wazalendo hawa ndiyo waliochora ramani ya njia ipi ichukuliwe kuidai Tanganyika na kuitoa katika mikono ya Wiangereza kwa salama.

Kwa wale waliokuwapo katika ‘’circle,’’ ile ya kupambana na Waingereza hakuna ambae hakuwa anajua kuwa Hamza Mwapachu ndiye aliyekuwa akisukuma mambo nyuma ya pazia iwe yuko Nansio au Rungwe sehemu za mbali alizotupwa na wakoloni ili asiwasumbue kwa kumtoa karibu na miji mikuu ambako ndiko yalipokuwa mashina ya kupinga ukoloni.

Mtafiti yeyote katika historia ya uhuru wa Tanganyika kama atakuwa makini hatoweza kumuepuka Hamza Mwapachu kwani ni vigumu kumtaja Julius Nyerere usimtaje Hamza Mwapachu.

Barua hii ya iliyoandikwa na Hamza Mwapachu kwa Julius Nyerere kwanza imedhihirisha ule ukweli kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika ipo katika vichwa vya watu na wengi wao wameshatangulia mbele ya haki,

Halikadhalika nyaraka nyingi za kipindi kile zipo mikononi kwa watu binafsi.

Barua hii ya Hamza Mwapachu kwa Nyerere imethibitisha ukweli huu na pia imefungua mlango kuwawezesha watafiti kuchungulia ndani kusoma na kufahamu nini Hamza alikuwa anasema kumwambia Nyerere.

Barua hiyo ni matokeo ya barua ambayo Nyerere alimwandikia Mwapachu kuhusu mambo muhimu waliyozungumza siku za nyuma.

Mwapachu anaandika na anasema kuwa hakutia katika maandishi kwa ajili ya kumbukumbu yale mazungumzo yao.

Baada ya kuandika haya Mwapachu anaorodhesha moja baada ya jingine katika yale waliyozungumza kama ifuatavyo:

1. Trusteeship as compared to Protectorate and Mandate
2. White Paper 191
3. White Settlement in Tanganyika

Ukurasa wa kwanza wa barua hiyo ya kurasa tatu unaonyesha mambo manane lakini nimeweka kwa leo hayo matatu hapo juu nayo ni Udhamini wa Tanganyika chini ya Waingereza, Mjadala wa East African High Commission na Ukazi wa Wazungu Tanganyika.

Haya yalikuwa mambo mazito, makubwa na ya kuzungumzwa kwa siri sana baina ya Waafrika.
Inawezekana vipi historia kama hii ikaachiwa ipotee hivi hivi tu?

Barua hii ni muhimu sana na kwa haraka ikawekwa katika Makumbusho ya Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo na naamini katika Maktaba ya Juma Mwapachu yapo mengi sana achilia hayo aliyohifadhi kichwani kwake.
 
Kweli tanganyika imetoka mbali n vijana w nyakati zile wamefichwa kwa bahati mbaya au maksudi na historia yake.
 
Wapigania Uhuru wengi naona ni waislamu(sina mrengo wa kidini But truth be told) lakin cha kushangaza baba wa Taifa mkiristo,aise hawa jamaa janja janja kama Mataifa yao yanavyosadifu,mf;USA,ISRAEL,RUSIA nk.
Sijawaza nimewaziwa.
 
Daah wanaume wa dar wakipindi hicho walikua na akili za kufanya mambo makubwa kama haya ila wa siku hizi wangeishia kuandikia hio karatasi "mistari/vina".
 
Umepotea sana Mzee Mohamed Said!Tunashukuru
 
Mzee Mohamed Said salute!...mzee wangu napenda kukufahamisha kuwa historia siku zote haisemi yale yote yaliyopata kutokea,sio historia ya Tanganyika tu yenye upungufu wa matukio,bali historia za mataifa mengi duniani hazijakamilika kwa 100%,kuna changamoto nyingi zilizopelekea hali hii,mojawapo zikiwa kukosekana kwa njia bora za uhifadhi wa kumbukumbu na uzito/umuhimu wa kumbukumbu kwa mtunza kumbukumbu...sasa ni jukumu lako kukusanya historia iliyopotea na kuileta kwa jamii lakini sio kulaumu kama vile layman asiyejua historia inapatikana kwa njia zipi.
 
Mzee Mohamed Said salute!...mzee wangu napenda kukufahamisha kuwa historia siku zote haisemi yale yote yaliyopata kutokea,sio historia ya Tanganyika tu yenye upungufu wa matukio,bali historia za mataifa mengi duniani hazijakamilika kwa 100%,kuna changamoto nyingi zilizopelekea hali hii,mojawapo zikiwa kukosekana kwa njia bora za uhifadhi wa kumbukumbu na uzito/umuhimu wa kumbukumbu kwa mtunza kumbukumbu...sasa ni jukumu lako kukusanya historia iliyopotea na kuileta kwa jamii lakini sio kulaumu kama vile layman asiyejua historia inapatikana kwa njia zipi.
Wise...
Nimelaumu kitu gani na nimemlaumu nani?
 
Wapigania Uhuru wengi naona ni waislamu(sina mrengo wa kidini But truth be told) lakin cha kushangaza baba wa Taifa mkiristo,aise hawa jamaa janja janja kama Mataifa yao yanavyosadifu,mf;USA,ISRAEL,RUSIA nk.
Sijawaza nimewaziwae.
thA goD,
Katika video hii nimeleza vipi Mwalimu Nyerere alichaguliwa kuchukua
uongozi wa TAA mwaka wa 1953 na mwaka wa 1954 TANU ikaasisiwa na
Mwalimu Nyerere akawa rais wake.

Abdul Sykes
alisafiri hadi Nansio, Ukerewe kuonana na Hamza Mwapachu
akifuatana na Ally Mwinyi Tambwe na huko ndipo ulipopita uamuzi wa
kumtia Mwalimu Nyerere katika uongozi:

 
Nani abebeshwe lawama kwa kukosekana kwa maandiko haya
 
Mohammed nakupa hongera Sana kwa kutufungulia pazia la historia uliyofichwa.

This what I call THE LOST HISTORY OF TANGANYIKA.

Ningependa uandike KITABU kuhusu historia tusiyoifaahamu ya TANGANYIKA
Hydom,
Kitabu ni hicho toleo la kwanza Kiingereza 1998.

upload_2018-4-17_19-31-1.png


Toleo la kwanza Kiswahili 2002

upload_2018-4-17_19-44-49.png


Toleo la pili Kiswahili na Kiingereza 2014

upload_2018-4-17_19-35-42.png
 
Nani abebeshwe lawama kwa kukosekana kwa maandiko haya
DJ,
Soma kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza matatizo yaliyotokea
ilipotakiwa kuandikwa kwa historia ya TANU mara baada ya
uhuru mwaka wa 1961
 
Hawa waasisi Wa TANU walimuamini nyerere na kumkabidhi kijiti cha uongozi
Je mwl alilipa shukrani au hakulipa kwa maoni yako
 
Hawa waasisi Wa TANU walimuamini nyerere na kumkabidhi kijiti cha uongozi
Je mwl alilipa shukrani au hakulipa kwa maoni yako
DJ,
Sheikh Hassan bin Ameir
alikuwa katika darsa zake kuna maswali na majibu.

Baadhi ya wanafunzi wake walikuwa wakimuuliza maswali ya kumtega ili akijibu
swali kwa namna ambayo atakuwa ameridhisha, ''school of thought,'' ya pande
zilizokuwa zinakinzana katika suala hilo atakuwa yeye kama Mufti kauli yake
ichukuliwe ndiyo jibu la sawa.

Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa akitoa jibu hili.

Alikuwa akisema kuwaambia wanafunzi wake wasome na majibu ya maswali yao
watayapata katika kusoma.

Nami nakuambia isome historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika majibu yote
utayakuta humo.
 
Sasa mkuu wewe umeisoma historia ya Tanganyika na Mimi pia nimeisoma na kwa kuwa vitabu vyenye ithibati ya serikali kutumika shuleni na vyuoni havijawatambua wengi Wa waasisi vipi vitaonyesha uhusiano wao na mwl!?
Ndo maana nikakuuliza wewe malenga unidadavulie.
 
Back
Top Bottom