Kutoka Mtwara katika Picha

Daaah!!!! hiyo ya mlango wa 1895 hiyo bomba sana. Love it to bits. Naheshimu sana watu wanaojua kutunza vitu na mali, haswa historical.
 
Hotel imejengwa miaka ya 1800's kwa hiyo itakuwa ni miaka hiyo hiyo!

Nadhani itakuwa mwishoni mwishoni mwa 1800. Sidhani kama ni mwanzoni mwanzoni mwa karne. Hata hivyo ni thawabu kubwa sana kutunza samani za kihistoria.
 

Jengo la Boma hotel kama linavyoonekana kwa ndani






Maeneo ya Mikindani kama yanavyoonekana toka ghorofani Boma hotel.


Fukwe za bahari ya Hindi eneo la Mikindani


Kitu kilichonishangaza ni jinsi watu wengi walivyokuwa kwenye fukwe za Mikindani wakisaka VIKORO na KUMBWA. Hawa ni aina furani ya konokono wadogo ambao niliambiwa ni mboga yao.


Barabara ndani ya eneo la Boma Hotel
 

Mikindani


Mikindani


Majengo ya kale ya Mikindani






Fukwe za Mikindani


Jamaa wako kazini hao.


Barabara hotelini Boma
 

Moja ya majengo ya kale na Hoteli ya Boma ikionekana nyuma kwa mbali!






Niliambiwa hili lilikuwa kanisa la Anglican alilolianzisha Dr Livingstone


Hii chakula ndiyo inatwa VIKOLO. Ni mboga ya wenzetu kule. Wanaisotea kuitafuta kwenye fukwe kutwa nzima!




Majengo ya kale ya Mikindani.
 
Wakuu leo naishia hapa.
Hii ni Mtwara wao wanaita Mtwara Mikindani.
Bado ninazo nyingine nyingi nategemea kuziweka baadae.
Stay tuned.
Goodnight!
 

Kwa beach zao bomba sana. Mimi nimeshafika huko mara kadhaa na huwa nafurahia sana.
 
safiiiiiii sana for your upload,this is great!!! nimezipenda picha,nakumbukka mtwara ndipo mji wangu,nimekulia pale na nimesomea pale,dah nimefurahi kuziona manake tangu nizamie huku ughaibuni sijarudisha majeshi huko .....iinaonekana mji umebadilika kiaina,ingawa baadhi ya maeneo yapo vilevile..halafu lile kanisa ni la CATHOLIC na SIO ANGLICAN, ni kwa bishop Mmole pale,nimependa kuiona migomigo kwenye mnada,iz very cool,yaani unapata nguo fresh kwa bei nzuri..yaani ningefurahi pia kuziona picha za kule soko kubwa,shangani,ligula pale kwa jionee mitaa ya chinichini,na hospitalini...ningefurahi sana..nadhani upload yako utainclude hivi vitu,tekea ma..tupo pamoja
 

Bahati mbaya majengo mengi ya kihistoria ya Mikindani yameanguka kabisa kwa kukosa usimamizi na ukarabati
 
Kwa kweli mtwara ni pazuri sana nilikuwa huko mwezi wa sita.Lakini wajihadhari wasikaribishe mafisadi maana wanaanza kupanyemelea kwa sababu ya umeme wa uhakika.Wasipoangalia patakuwa kama manzese ya Dar au Kariakoo muda si mrefu.Wataalamu wa Planning wafanye kazi yao kwa makini ili kuupanga mji.
 
Nadhani itakuwa mwishoni mwishoni mwa 1800. Sidhani kama ni mwanzoni mwanzoni mwa karne. Hata hivyo ni thawabu kubwa sana kutunza samani za kihistoria.
Umeambiwa hiyo Boma hotel yenyewe Serikali walishindwa kutunza wakapewa jeshi la polisi wakashindwa mpaka alipopewa Muingereza. Inatia huruma sana.
 
Mtwara has always been good, beautiful and unspoiled....
The sand on the beach, sugary white...
 
One of my favorite place of all time is Mikindani.

Nasikia siku hizi huwezi kupata kiwanja Mikindani wawekezaji wamenunua sehemu kubwa ya ardhi kwa aijili ya mahoteli makubwa, je hii ni kweli?
 
Picha safi sana Mkuu kazi nzuri, ila ni-comment katika ile ya pweza. Kiswahili cha kawaida, pweza ni kitoweleo au kitoweo na siyo mboga.
 
Inawezekana kwamba viwanja vingi ni vya wawekezaji wa mahotel lakini pale naona ipo hiyo moja tu ya Boma Hotel na hakuna hata hotel moja inayokuwa constructed kwenye maeneo hayo.
 
afadhali weye umeamua kuonesha mambo mazuri ya Mtwara...mwingine angekwenda kupiga picha mbayambaya na kuzileta hapa....big up mkuu
 
Pamoja na uzuri wa mkoa wao watu wa Mtwara hawajui kabisa mambo ya biashara.Sijui ni uvivu au ni kitu gani.Inabidi wajasiriamali wawahi kujichotea mipesa huko.
 
Huo ndio ukweli mwingine wa wazi wazi.
Tena si kweli kwamba serikali imepasahau bali watu tu wako nyuma kwa sababu ya ufinyu wa uelewa.
Lakini pana opportuniyt zote za biashara kubwa kubwa.
Wale wanaopenda kuwekeza nendeni katembeleeni huko muone maeneo ya kuwekeza. Pesa ipo.
Hata mbao zapatikana kwa wingi tu.
Tena njiani nimepita eneo kama kilometa 50 hivi ambazo nadhani hazijawahi kuona jembe tangu Mungu aiumbe ardhi ile. Mtu anaweza kujitosa kulima au kufuga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…