Huu uzi ni wa mwaka 2009 miaka kama 11 hivi iliyopita. Wakati huo Mtwara ilikua inachipukia kuja juu. Leo siyo haba japo kumedidimia tena baada ya mambo ya gesi kupoa kabisa.
Kama mdau au wadau ikiwemo mleta mada akienda tena anaweza kuwa na picha nyingi na nzuri kuliko hizo. Kwa sasa anaweza kupata BNN ROYAL Hote,Cashewnut Hotel,LUWA EVERGREEN HOTEL,TIFFANY DIAMOND HOTEL,KIWANDA CHA DANGOTE, Vinu vya kuchakata Gesi kwa ajili ya Mtwara kule Kilambo,KIWANDA CHA CHEMICAL ZA WATAFUTA GESI,BUSTANI/MANDHARI NZURI PALE MZUNGUKO MNARANI,TAA ZA KUONGOZA MAGARI PALE BIMA(ingawa siyo issue sana,ila kwa kuwa ipo miji haina hata moja,nasi nayo siyo haba) nk nk nk.
Tutashukuru kama mtu atajitolea kuziweka humu.
Hii itasaidia kuwaelimisha watu ambao hawajafika Mtwara wapate elimu ya nini hasa kipo Mtwara
Ni matumaini tutapata mwendelezo wa picha kati ya zile za mwaka 2009 na leo hii 2021.
Enzi hizo Mashujaa Park, Tilla Park hazikua nzuri kama leo, hakukua na Naf Beach, Tiffany, BNN Royal, Shangan Apartments, Chuno road, Dangote, Luwa Evergreen, Shooters nk
Sent using
Jamii Forums mobile app