Kutoka Mtwara katika Picha

Asante kwa kunikosoa hapo maana mwalimu wangu wa kiswahili alikufa nikiwa darasa la kwanza nikabaki na mwalimu wangu wa Kigogo.
 
Mtwara looks beautiful. Kwa ujumla jamani nchi yetu ni nzuri na inavutia kwa sana tu.
 
asante sana mkuu na hongera kwa kudondosha hizi picha,
yaani zimenirudisha mwaka mmoja nyuma niliokuwa huko,imekuwa nio bonge la flashback kwangu
asante sana mkuu
 
asante kwa kutuonyesha maeneo ya kwetu mkuu,lakini siyo kweli kwamba Mtwara hakuna daladala labda ulikwenda miaka ya nyuma sana takriban miaka 8 mpaka 10 sasa tangu daladala zianze Mt.
 
Aah!!Safi sana mkuu picha zinavutia kwa ambaye hajafika mikindani inafanana na bagamoyo hata ki historia na majengo yake utayapata na kilwa kivinje na kisiwani au zenji,tatizo ni kwamba serikali haikutilia mkazo kuwekeza ktk nyanja ya utalii kama ilivyo Bagamoyo labda kwa vile ni karibu na DSM na mambo ya miundombinu na upatikanaji wa umeme wa uhakika.Lakini hivi sasa kila kitu kipo tena hapo mikindani kuna chanzo cha maji baridi kuliko mfano,zamani kulikuwa na kiwanda cha cocacola lakini wakafunga sijui kwa nini sasa wanapata shida ya ku-inport toka Dar.Nadhani sasa ni changamoto kwa wadau wa sekta ya utalii kuchangamkia fursa ya kuwekeza ktk fukwe hizo,pia wenyeji waache kuharibu mazalia ya samaki kwa kuendekeza uvuvi wa mabomu na baruti mmeharibu sana pwani za mikindani mkangala sudi mpaka msangamkuu
 
mkuu hiyo boma hoteli ni kiboko,ukiingia humo ndani huwezijua kama upo ktk gofu lenye takriban miaka 100 ilyopita an kama hujala samaki wenye ladha nenda uonje samaki wa mikindani hata wale wa Nangurukuru utawasahau,na siku hizi wadau wamestaarabika wamechimba vyoo hata karibu na fukwe
 
lazima tukubali kuwa toka enzi za mwalimu mikoa ya kusini iliachwa nyuma kimaendeleo makusudi hususan mtwara kwa kisingizio eti cha vita ya msumbiji ikawa haiendelezwi zaidi ya kuwa na makambi na vituo vingi vya wapigania uhuru,ukibahatika kufika nachingwea nenda farm 17 ukajionee jumba la Samora Machel lingeweza hamishwa nadhani lingeletwa Dar liwe makumbusho,nilisoma mtwara miaka ile ya sabini kila shule ya msingi ilikuwa na Handaki nakumbuka hayati mwalimu Nyerere alitembelea mtwara akaingia ktk handaki letu shule ya msingi chikongola.Amini usiamini vijana wa rika lile toka Kusini hasa Mtwara tuliiva kisiasa na kimapinduzi ndiyo hawa akina john komba ,nchimbi na wengine wengi walioibuliwa na marehemu mzee mnauye acha masihara tulikuwa mahodari wa kuzama ktk mahandaki ndege ikipita shule nzima inabaki tupu,tumecheza paredi na kuimba nyimbo za kimapinduzi siku hizi hawawezi,ila tuliachwa watupu
 
Nimempenda yule samaki mkubwa kwenye tenga, tafadhali ukija dar niletee samaki sio picha
 
Ni kweli kabisa fursa zipo nyingi sana, kilimo ,uvuvi,na biashara nyingine nyingi tu. Tatizo kubwa bado liko kwenye usafiri, mabasi ni mengi sasa hivi lakini hakuna bei maalumu ya nauli kwani zimekuwa zikibadilika badilika sana sijui hawa sumatra wanafanya nini
 
Mbona bei si mbaya sana?
Usafiri wa basi ni sh 18 elfu tu Mtwara to Dar!
Ebu fikiri mtu anayesafiri toka Bukoba Kwanda Dar analipa 60 elfu!
Barabara si mbaya sana maana sehemu kubwa ni lami na ndogo ni chafu lakini inatengenezwa.
 
tafadhali leta na picha za akina dada wa makamo (19 - 30) kutoka Mtwara. Waombe ridhaa wasepe kwenye ukumbi wa jamii. πŸ™‚
Inabidi apate ruksa kutoka kwa kaka ao kwanza, si kwa kulazimisha
 
KIle kipande kati ya daraja la Mkapa na Somanga, ambacho kilikuwa hakina lami ndio kilikuwa kinabadilisha sana viwango vya nauli. Hivi sasa kinatengenezwa na kitakapokamilia njia yote itakuwa full mkeka na naamini bei itapungua na haitobadilikabadilika
 

Usafiri wa kwenda Mtwara sasa hivi ni mzuri na mabasi ni mengi na mazuri, tatizo kubwa mabasi yote yanaondoka ubungo saa 12 asubuhi. Tunaomba mamlaka zinazohusika zipange utaratibu wa mabasi kupishana kuondoka, ili kwamba liwepo basi la mwisho kuondoka dar saa 5 au saa 6 mchana.
 
Wadau bado nina picha naandaa lakini nasikitika kuwa nimejikuta nimepoteza picha nyingi sana. It was a techinical problem. Natamani kulia na naona machozi yanaanza kudondoka........ kwa sababu picha ni sehemu yangu ya maisha😱
 
Wadau bado nina picha naandaa lakini nasikitika kuwa nimejikuta nimepoteza picha nyingi sana. It was a techinical problem. Natamani kulia na naona machozi yanaanza kudondoka........ kwa sababu picha ni sehemu yangu ya maisha😱
MF asante sana kwa picha nzuri, umenifanya nijisikie niko kwetu japokuwa niko mbali nako. Picha zinafurahisha sana. Shukrani pia kwa waliochangia mawazo, yamenipa mtazamo tofauti na awali.
Pole kwa hizo zilizopotea, jipe moyo - there is always a reason for every event.
Ubarikiwe MF!
 
Wakuu naendelea na zoezi la kuonyesha picha zaidi za Mtwara ingawa kwa kweli nimepoteza nyingi!


Huu ni moja ya sehemu za ibada pale Mikindani............jengo liko kati kati ya majengo yale ya zamani. Sikuwahi kujua lina umri ganiπŸ˜€


Hili linasemekana liliwahi kuwa kanisa la Anglikan lililojengwa na Livingstone. Bado lina hali nzuri na linatumika kama ofisi na maduka.




Watalii pia wapo kule Mtwara. Mikindani inatembelewa na wazungu kujionea jinsi waarabu na wajerumani walivyoishi pale. Je watanzania tunajali utalii wa ndani? Jiulize katika nchi yetu nzuri hii umeshawahi kutembelea vivutio vipi?


Wakina bibi wao wanatoka beach kutafuta vitoweo.
 




Wakina mama wakiwa na ndoo zao zikiwa zimefurika aina fulani ya konokono wao wanaita VIKOLO na KUMBWA ambacho ni kitoweo chao. Naona kila mmoja wao kajaza ndoo yake na bila shaka wanakwenda tafuta wateja. Sikuwahi kuonja kitu hii lakini wale wenyeji wa Mtwara twambieni, je ni watamu hao konokono?




Kwenye ufukwe huu utaona watu wengi sana! Si watalii hawa, hapana ni wenyeji tu wa Mikindani hawa na wanatafuta kitoweo (VIKOLO). Naweza kusema ni njia nyingine ya uvuvi!


Hili ni eneo la ufukwe pale Mikindani. Nilipiga picha hii nikiwa nimesimama kando ya barabara itokayo Lindi, ina maana ufukwe umekingwa na barabara au niseme barabara inapita ufukweni kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…