Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,904
- 1,064
- Thread starter
-
- #61
Kwa hiyo sahiv utakuwa na 80 sio?Bahati mbaya mimi ni mzee wa miaka 70 na nina kora ya kichungaji shingoni! hivo vibinti vidogo vyote vilikuwa vinanikimbia. Nisingeweza kupata picha zao.
Admin mbona picha hazifunguki?
Hii ndio barabara inatokea Lindi kuja Mtwara!
Magomeni Mnadani. Ni lini vijana hawa watajengewa soko zuri kwa ajili ya biashara yao? Ebu fikiri akitokea mwehu mmoja wa kuwasha moto vibanda hivi je hasara kiasi gani itawapata vijana hawa?
Nilifurahi kuona hair cutting Salon za chini ya mwembe. Vijana mnaona? msisingizie mgao wa umeme kazi mtindo mmoja hata kama hakuna umeme. Angalia jamaa anazo mpaka uniform zake na wateja wake!
Vijana wamejiajiri kuuza hata maji mitaani.
Mibuyu inapendezesha mandhali.
Hii ni sehemu ya mbele ya Boma Hotel. Hotel hii iko Mikindani. Mikindani ni eneo lililosheheni majengo ya zamani sana(Maghofu). Hapa palikuwa ni makazi ya waarabu na palikuwa na soko la utumwa kabla halijasambalatishwa na Dr Livingstone. Na majengo ya hii hotel inasemekana yalijengwa miaka ya 1890's na zamani ilikuwa ghofu baada ya serikali kushindwa kuiweka katika hali ya kutumika. Niliambiwa kuwa iliwahi kuwa hata chini ya umiliki wa jeshi la Polisi lakini nao walishindwa kulikarabati jengo na serikali ikampa mwekezaji toka Uingereza ambaye kalitengeneza vizuri sana. Ni hotel kubwa kwa Mtwara.
Hiki kifaa ni sehemu ya mizinga iliyokuwa ikitumika katika vita ya wajerumani na waingereza na kimeifadhiwa pale nje ya hotel ya Boma kama ukumbusho kwa kuwa sehemu hiyo ilitumika katika vita hiyo.
Hii kitu ipo kweli pale Chikongola hadi leo? Mkuu ndo nasikia leolazima tukubali kuwa toka enzi za mwalimu mikoa ya kusini iliachwa nyuma kimaendeleo makusudi hususan mtwara kwa kisingizio eti cha vita ya msumbiji ikawa haiendelezwi zaidi ya kuwa na makambi na vituo vingi vya wapigania uhuru,ukibahatika kufika nachingwea nenda farm 17 ukajionee jumba la Samora Machel lingeweza hamishwa nadhani lingeletwa Dar liwe makumbusho,nilisoma mtwara miaka ile ya sabini kila shule ya msingi ilikuwa na Handaki nakumbuka hayati mwalimu Nyerere alitembelea mtwara akaingia ktk handaki letu shule ya msingi chikongola.Amini usiamini vijana wa rika lile toka Kusini hasa Mtwara tuliiva kisiasa na kimapinduzi ndiyo hawa akina john komba ,nchimbi na wengine wengi walioibuliwa na marehemu mzee mnauye acha masihara tulikuwa mahodari wa kuzama ktk mahandaki ndege ikipita shule nzima inabaki tupu,tumecheza paredi na kuimba nyimbo za kimapinduzi siku hizi hawawezi,ila tuliachwa watupu
Hii dude ilianzishwa miaka 13 iliyopita. Muanzisha uzi hatujui hali yake ila abarikiwe sana. Bahati mbaya picha nyi gi ziliziwekwa miaka hiyo hazifunguki tena. Kwa sasa twaongeza Kutoka Mtwara katika Video:Maeneo mengi ya mipakani na hasa ambako kulikuwa na vita vya ukombozi wa nchi jirani na Tanzania minara ya jinsi hii imejengwa kama kumbukumbu ya wapiganaji wetu. Kama inavyoonyesha mnara huu uliopo uwanja wa mashujaa Mtwara.
Baba huyu amepozi na Samaki wake akitoka kuvua. Angalia na wakina mama wale mbele yake nao wanatoka kutafuta samaki hasa kwa ajili ya biashara. Samaki Mtwara ni wengi na biashara hii inafanyika kwa wingi na hasa wakina mama wanaouza samaki wa kukaanga. Mkoa una utajiri mkubwa wa samaki.
Mibuyu ni miti inayoupendezesha mji huu wa Mtwara kwani imetapakaa kila mahali.
Uvuvi ni sehemu ya maisha ya watu wa Mtwara. Lakini hapana viwanda vya Samaki kama vile vilivyojazana Kanda ya ziwa. Kwa nini?
Kama kawaida usafiri wa Bajaj ndio usafiri wa kutumainiwa na wakazi wa mji wa Mtwara. Hakuna daladala kama za Daresalaam.