Kutoka MwanaSpoti : Mastaa walioweka vipengele vya ajabu katika mikataba yao.

Kutoka MwanaSpoti : Mastaa walioweka vipengele vya ajabu katika mikataba yao.

magnifico

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
11,075
Reaction score
24,634
PARIS, UFARANSA. MAJUZI imebainika
staa mpya wa PSG, Kylian Mbappe alitaka
viingizwe vipengele vya ajabu katika
mkataba wake wa sasa wakati alipokuwa
anahamia klabu hiyo akitokea Monaco ya
Ufaransa.
Mbappe alitaka awe mchezaji anayelipwa
zaidi klabuni hapo, lakini pia alitaka
apewe ndege yake binafsi kwa ajili ya
matumizi yake. Hayo sio madai ya
kwanza kwa mastaa wa kisasa kutaka
yaingizwe katika vipengele vya mikataba
yao.


Neymar vs Barcelona

Uhamisho wa staa wa kimataifa wa
Brazil, Neymar kutoka klabu ya Santos
kwenda Barcelona mwaka 2013
ulikumbwa na mikasa mingi pamoja na
tuhuma za rushwa. Lakini ndani ya hilo
kulikuwa na madai ya ajabu kutoka kwa
staa huyo kwenda Barcelona akidai
alihitaji marafiki zake wa karibu wawe
naye.
Neymar alitaka Barcelona ilipie gharama
za safari za marafiki zake ambao
wangemtembelea kutoka kwao, Sao Paulo
Brazil kwa ajili ya kumliwaza. Rais wa
zamani wa Barcelona, Sandro Rosell
ndiye ambaye alitoboa siri hii wakati
akiwa mahakamani kukabiliana na kesi
ya rushwa katika uhamisho wa Neymar
ambaye kwa sasa yupo PSG. Rosell
alimwambia Jaji mwendesha mashtaka
kwamba klabu hiyo iliwahi kulipa kiasi
cha Pauni 430,000 kwa ajili ya
kusafirisha kundi la marafiki zake
Neymar kwa ndege binafsi kutoka Brazil
mpaka Barcelona.


Dennis Bergkamp vs Arsenal

Wakati staa wa zamani wa Arsenal, Marc
Overmars alijulikana kama Mdachi
anayepaa, staa mwenzake wa kimataifa
wa Uholanzi, Dennis Bergkamp aliyekuwa
akikipiga naye Arsenal alijulikana kama
‘Mdachi asiyepaa’. Hii ilitokana na tabia
yake ya kutopenda kupanda ndege.
Alikuwa na hofu na ndege na hakutaka
hofu hiyo iiishie mdomoni tu. Aliamua
kuweka katika maandishi kabisa ya
mkataba wake na Arsenal kuwa
hatapanda ndege katika safari za ndege za
timu hiyo nje ya England.
Katika kitabu cha maisha yake, Bergkamp
aliweka wazi sababu za kutopanda ndege
tena na Arsenal iliheshimu mawazo yake.
“Nimewahi kupanda ndege kubwa na
ndogo, na ndogo zaidi. Wakati fulani
mara moja nikiwa na Ajax tuliwahi kupaa
juu ya Milima Etna karibu na Naples. Hali
ambayo tuliipata ilinitisha sana. Kuhusu
suala la kuruka na ndege nadhani
sitaruka tena na ndege,” alisema Berkamp
katika kitabu hicho. Kisha akaongeza:
“Katika maongezi yangu na Arsenal kama
nilisema neno ‘milioni’ basi
watanirudisha mpaka ‘mia’ kwa sababu
sipai na ndege. Na nilikubali.”


Ronaldinho vs Flamengo

Kipaji cha Ronaldinho, tabasamu lake,
uwezo wake wa kushangaza uwanjani
vilimfanya awe shujaa wa vijana wengi
waliomuona akicheza mwanzoni mwa
miaka ya 2000.
Hata hivyo, nje ya uwanja bado
Ronaldinho alikuwa na akili za ajabu
ajabu. Ni wazi Ronaldinho alipenda sana
starehe nje ya uwanja. Alitoa madai ya
kushangaza wakati aliporudi kwao Brazil
kukipiga klabu ya Flamengo akitokea AC
Milan mwaka 2011. Ronaldinho
aliwaambia Flamengo kuwa katika
mkataba wake alitaka aruhusiwe kwenda
out kujirusha katika klabu za usiku mara
mbili kwa wiki.
Kutokana na Flamengo kumhitaji sana
Ronaldinho ilikubaliana na sharti hilo
bila ya kusita.


Giuseppe Reina vs Arminia Bielefelf

Kuna mambo yanachekesha sana
linapokuja suala hili. Sikia hii. Ilikuwa
kali zaidi. Mshambuliaji wa Kijerumani,
Giuseppe Reina aliamua kwenda njia
tofauti na maombi mengi ya mkataba ya
wenzake wakati alipokuwa anahama
Klabu ya SG Wattenscheid 09 kwenda
Arminia Bielefeld hapohapo Ujerumani
mwaka 1996. Wakati akiwa katika
mazungumzo ya maslahi binafsi na timu
hiyo, Reina aliomba ajengewe nyumba
katika kila mwaka wa mkataba wake wa
miaka mitatu na klabu hiyo. Ilionekana
kama jambo zito kwa klabu hiyo lakini
kumbe ambacho Reina alisahau ni
kuelezea ukubwa wa nyumba au ubora
wa nyumba hiyo.
Arminia wakaguna na kufanya ujanja wa
ajabu. Kila mwaka walikuwa
wanamjengea nyumba nzuri ya nyasi!


Guie-Mien

Nyota wa zamani wa Timu ya Taifa ya
Congo Brazzaville alitumia akili nzuri
kuhakikisha mke wake ananufaika na
uhamisho wake kutoka Karlsruher SC
kwenda Eintracht Frankfurt mwaka 1999.
Rolf-Christel Guie-Mien alihakikisha
familia yake itaendelea kuwa bora hata
akiachana na mpira baada ya kuweka
kipengele katika mkataba wake kwamba
klabu ya Frankfurt italazimika kumpeleka
shule mkewe akasomee masomo ya upishi
wakati yeye akipiga soka katika klabu
yao.


Georg Koch vs PSV Eindhoven

Kuna wanadamu hawataki kabisa ujinga.
Huyu ni mmojawapo. Kipa wa
Kijerumani, Georg Koch mwaka 1997
aliamua kwenda nchi jirani ya Uholanzi
kukipiga katika Klabu ya PSV Eindhoven
akitokea Fortuna Düsseldorf. Moja kati ya
kipengele ambacho alikiweka klabuni
hapo ilikuwa ni kukatisha mkataba wake
endapo kama angefanyiwa vitendo vya
ubaguzi wa rangi. Ni kweli, alidumu PSV
kwa kipindi cha miezi mitatu tu kabla ya
kuvunja mkataba wake kutokana na
kufanyiwa kitendo cha ubaguzi. Alirudi
kwao Ujerumani kukipiga Klabu ya
Arminia Bielefeld akiachana na upuuzi
wa ubaguzi wa rangi wa majirani zao.
Shukrani kwa mkataba wao.


Eto’o vs Anzhi Makhachkala

Uhamisho ulioshagaza wengi huu hapa.
Wengi hawakuutarajia. Ni wakati staa wa
kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto'o
alipoamua kutua Anzhi Makhachkala ya
Russia akitokea Inter Milan ambayo
msimu mmoja uliopita ilikuwa
imechukua ubingwa wa Ulaya. Mkataba
wa staa huyu wa zamani wa Barcelona
ulikuwa mnono sana huku akiingiza zaidi
ya Pauni 20 milioni kwa mwaka. Lakini
kama vile aitoshi aliingiza kipengele cha
ajabu ndani yake.
Mkataba wa Eto’o uliweka wazi staa
huyo angekuwa anasafirishwa na ndege
binafsi kutoka Makhachkala kwenda
Moscow ambako alipendelea zaidi kuishi.
Kylian Mbappe vs PSG
Madai ya ajabu zaidi kuwahi kutolewa na
mchezaji katika zama mpya. Kwa mujibu
wa taarifa za uchunguzi wa kidaku
kutoka katika Gazeti la Der Spiegel la
Ujerumani, staa wa PSG, Kylian Mbappe
ambaye alikuwa anatakiwa na klabu
mbalimbali akiwa na Monaco inadaiwa
aliipa PSG sharti la kukodiwa ndege
binafsi kwa saa 50 kila mwaka katika
mkataba wake wa sasa.
Hata hivyo, PSG ilikataa madai hayo ya
Mbappe ingawa baadaye iligundulika
ilikubali kugharimia kiasi cha Pauni
26,000 kila mwezi kwa ajili ya
mfanyakazi wake binafsi, dereva na
mlinzi wake.
 
Mmh, Huyo jamaa kwa Yanga nadhani hata bure anacheza.Maana anaipenda hiyo klabu kuliko anavyojipenda mwenyewe.
 
Back
Top Bottom