Kutoka Taifa: Yanga Vs Toto African, vita ya ubingwa ama kushuka daraja!

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Klabu ya Yanga leo itavaana na Klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza kwenye uwanja wa Taifa, mchezo ambao endapo Yanga wakishinda watatangazwa ubingwa huku wanajangwani hao wakimkosa kiungo wao mshambuliaji Simon Msuva baada ya kupata majeruhi wikiendi iliyopita dhidi ya Mbeya City.

Kikosi cha Yanga
1. Beno Kakolanya
2. Hassan Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vincent Bossou
6. Thaban Kamusoko
7. Juma Mahadhi.
8. Haruna Niyonzima
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Geofrey Mwashuiya

Akiba

Deogratius Munishi
Juma Abdul
Nadir Haroub
Matheo Antony
Deusi Kaseke
Emmanuel Martin
Justine Zulu.
=======

GOOOOOOOOO Dk 81, krosi safi ya Juma Abdul, Tambwe anaruka na kupiga kichwa safi kinachotinga wavuni kama roketi
 
Jamani Simon Msuva [emoji24],get well soon.

Yanga leo wacheze kwa kiwango kama walivyocheza dhidi ya Kagera Sugar,isiwe kama kile kiwango kibovu dhidi ya Mbeya City ambacho kiukweli ile mechi tulishinda kibahati tu.

Kila la kheri Yanga,natumai leo tutaendeleza ubabe wetu kwa kuchukua kombe kwa mara nyingine mfululizo. [emoji123]
 
Watachezaj ilhal alpotok msuva gem ilyopta mpira ukaisha? Mnakufa leo
 
Hakuna kiwango miamala tuu hiyo wangekuwa na kiwango wangeonesha kimataifa
 
Hutaki kumsaidia ndgyo asishuke daraja?
 
Pengo la Msuva linaonekana wazi,jamaa anatugharimu sana.
Yanga wameshindwa kutumia nafasi zao vizuri kujipatia magoli kipindi cha kwanza,huku Toto Africans wao wamepata nafasi 3 pekee nazo wameshindwa kuzitumia vizuri.

Tusubiri kipindi cha pili kuona itakuwaje,huenda tukashuhudia mabadiliko yatakayopelekea magoli/ushindi.
 
Juma Mahadhi ni mzigo,Msuva ni muhimu sana
 
Toto Africans =Yanga B

Yanga A hawezi kumkatili Yanga B kwa sababu Yanga B akifungwa anashuka daraja

So mechi ya leo itaisha sare au Yanga A atafungwa goli moja kisha Yanga A wataenda kuwararua rarua Mbao FC.
 
Nikweli Nifah ila tunapasua hii
 
Wana Mwanza tunataka kuwaona vijana wetu Toto Africa Vpl tena mwakani, so tunawaomba wakaze kumzuia baba yao huyo hah hah
 
Unaonaje moody? Huu ni mpango kuwanusuru Toto wasishuke daraja?
Vipi tuna uhakika gani wa kumfunga mbao?
Tutamfunga Toto na tutamsaidia na mtibwa ila sio sisi Nifah tunataka ubingwa na unapatikana leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…