Kutoka Tunduru: Wakulima wa Korosho wapokea zaidi ya Sh. Milioni 500

Hizo bilioni 800 ziliwafikia wakulima au wafanyabiashara wa kati?Sasa hivi bilioni zitawafikia walengwa na kuwaacha watu wa kati.
 
Mafisadi kama wewe ndiyo mnalalamika kafeli kwa kuwa amewabana kwenye ufisadi wenu!! Badilikeni acha ufisadi mkuu la sivyo hutaonekana uraiani.
Vp umeenda kubangua koro-show

Ova
 
Hizo bilioni 800 ziliwafikia wakulima au wafanyabiashara wa kati?Sasa hivi bilioni zitawafikia walengwa na kuwaacha watu wa kati.
Nenda tunduru hko ukajioneee Hali halisi usikalie kupata habari za kusikilizaaaa

Ova
 
Nenda tunduru hko ukajioneee Hali halisi usikalie kupata habari za kusikilizaaaa

Ova
ITV wapo Tunduru na wametuletea hali halisi ikiwemo madiwani wa upinzani walioshikwa katika kutapeli wakulima.
 
Sio kila muda upost kitu,tsh 500 million ni sawa na wamenunua tani 152 tu.Sasa sielewi unajaribu kuwaeleza nini watanzania juu ya hatma ya zaidi ya tani 200,000 za mavuno ya korosho.
FYI Korosho zitanunuliwa zote. Wewe Tuliza mshono bado haujapona vizuri.
 
million 500 kati ya billion 600...au billion 2 kati ya billion 600.. si mwaka utaisha hawajamaliza kununua?
gervase
Mwaka utaisha kwa mahesabu gani?
By the way mwaka umebaki wiki chache sana!
 
Kakurupuka huyo Lumumba akidhani mil500 ni pesa nyingi sana.

Hta hajui kuwa kuna tani ngapi za korosho
Wakurupukaji ni nyie...Hii ni taarifa ya Tunduru tu tena kwa siku chache tu bado maeneo mengine.
Serikali itanunua Tani zote tena kwa bei ya 3300
 
x = 500,000,000/3,300 = 151,515 = ~151 Tones

Nakukumbusha kuna Tani laki 221.

% ya walionunua = 151/221,000 = 0.068%

Zero Brains wa Lumumba wanapenda namba lakini hawajui hesabu.
Mkuu, hyo umeambiwa kwa Tunduru area.. Sio maeneo yote na wala sio tani zote 220,000 ziko huko Tunduru
 
Wakurupukaji ni nyie...Hii ni taarifa ya Tunduru tu tena kwa siku chache tu bado maeneo mengine.
Serikali itanunua Tani zote tena kwa bei ya 3300
Waambie hao.. Yaan kuna mijitu humu wao wamekalia kuharibu ilimradi nyoyo zao zifurahi..
Utadhan kama wana angalau kilo 1 ya korosho
 
Huna TV wewe?Hali ya kibiashara kwa wana Kangomba lazima iwe mbaya Serikali imeamua kuwalinda wakulima wake.
Hela walizopewa na Jeshi hawazitumii? Sioni mabadiliko hayo milioni 500 hali ile ile
 
Mkuu Inawezakana Unachokiongea Ni Sahihi, Lakini Tunaomba Utuambie Ni Chama Gani Cha Msingi Kilichopokea Hiyo Hela??
Mana Malipo Yote Ya Wakulima Hulipwa Kulingana Na Chama Cha Msingi Kilichopokea Korosho....!!
Wakulima wanalipwa direct kwenye account zao...huwa hamsikilizagi hotuba?
 
hesabu huwaga hazidanganyi....

malipo haya ni 0.08% tu ya thamani ya korosho yote iliyochukuliwa na majeshi ya serekali. haya malipo yamefanyika ndani ya siku 10.

kwa ulipaji katika speed hii, itachukua siku 12,500 (au miaka 34) kuwalipa wakulima wote.

poleni wakulima. tukutane 2020.
 
Korosho yote iliyochukuliwa huko Tunduru ni kiasi gani?
 
Wakulima wa kahawa wana kilio kikubwa kuliko wa korosho, msijifanye vipofu na msidanganyike na hatua hizi zilizojaa SIASA nyingi ndani yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…