Kutoka uboss hadi umachinga

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Inasikitisha sana wadau lakini ndio katika kupambana na maisha si lelemama.

Ni hivi baada ya kelele za muda mrefu za maboss wetu wenye asili ya Asia.

Nimejipanga 2020 niachane nayo na nitafute vya kwangu. Hii ni baada ya uvumilivu wa hali ya juu ya vichambo vya hawa raia ukizingatia hali ya soko la ajira na jinamizi la kitaa haswa sisi wenye familia ila sasa enough is enough.

Bahati mbaya sikuwekeza maji zaidi ya hizi milioni mbili na kwakuwa mimi ndio nitavunja mkataba basi sitegemei kupata termination benefit yoyote na Ile pesa ya NSSF naimani sitoweza ipata kwani tunaikopesha serikali yetu itujengee flyovers.

Baada ya kutafakari biashara nyingi zinazoweza nipatia cash kwa haraka nikapendekeza biashara ya kuuza nguo sokoni mfano Tandika na the like.

Sikumshirikisha mke wangu naimani atanirudisha nyuma yaani hii ni one man army.

Ninachoomba ni sapoti kutoka kwenu wadau maana sijajua undani hasa wa hii biashara. Mkinipatia uzoefu wa kutosha mtakuwa mmenisaidia.

Nawasilisha.
 
Mtaji wa kwanza wa biashara ni elimu ya hiyo biashara, tafuta elimu yake kwanza, kama ukiweza tafuta aliefanikiwa kwenye hiyo biashara (aliyefanikiwa kweli sio watu wa hadithi hadithi) akuongoze.

Kuwekeza kwenye biashara usiyoijua ni kupoteza na sio kuwekeza. Mtaji wako mkubwa ni elimu ya hiyo biashara na elimu haina faida kwa kuijua tu bali kuifanya hiyo elimu.
 
Pole na hongera mkuu, inashauriwa sana kufanya kile unachokipenda, cha kufanya pamoja na maoni ya wadau wa hapa nenda huko sokoni tafuta mtu atakaekupa taarifa sahihi.
Japo wengi ni wachoyo wa kutoa taarifa lakini huta kosa.

Pia jaribu kufikiria na biashara ya kuzunguka kwenye minada, nasikia biashara huwa inatoka sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ankol,

Nakupongeza kabisa katika kuchukua hii hatua uliyoichukua, usijali swahili yangu sio poa lakini utanielewa hivyo hivyo.

hii ni hatua ya kihistoria katika maisha yako umechukua,kabla sijakupa ushaui wowote, niketaka nikupe kisa moja kilichotokea katika taifa fulani, mtu moja alienda kufanya interview ya kazi ya janitor, yaani kazi ya kufagia, sasa alipoulizwa maswali akaanguka ile interview, so wingine akachukuliwa, sasa huyu jamaa akawa hana lolote la kufanya.

alikuwa na dola 200 pekee, akaamua kwenda shambani fulani akanunua masaduku kadhaa ya tomato, akaenda akauza, ikaisha, akarudi kanunua tena kauza hivyo hivyo, sasa akajuana na wateja wengi kazi au orders zikawa nyingi, jamaa akaaza kukodisa pick up kweda nayo mashambani kununua tomatoes na kisa kusuply to customers, to cut a long story short , huyu jamaa sasa ako na viwada vya kuprocess tomatoes na mihela nyingi ajabu, na mambo mengi sana kaa biashara zingine.

Swali je kaa angefaulu ile interview bado angekuwa mufagiaji wa ofisi, lakini sasa anaweza inunua ile kamupuni ambayo ilimuyima ajira, my point is this, you will never realise your potential untill you take the first step into the UNKNOWN, sasa tuje kwa swala alo mkuu, my first advice to you, never be in a hurry to make profit, never enter into a bussiness which you dont fully understand, do your research very well, never listen to every tom, dick and harry, and aslo there are some nuggets of wisdom as far as biashara is concerned you can never learn them till YOU ARE IN THERE SIR,

usiwe na haraka , kuwa maakini, weigh every adive, and in everything PUT GOD FIRST, wish you all the best happy xmas and blessed new yea sir
 
Do it brother safari moja huanzisha nyingine
wish you good lucky, ila kua makini na madalali kwenye hayo masoko ya nguo.
 
Wazo zuri sana hili. Ushauri wangu usiache kwanza kazi. Hela uliyo nayo anzisha biashara ukiwa unasubiri uone inayokwenda. Ukiona inakwenda vizuri ndo uache. Ukiacha sasa hivi ghafla itakusumbua kisaikolojia. Unaweza sema hata mkeo aanze kusimamia ukimfuatilia kwa ukaribu.

Usiache kazi hadi uone mwelekeo unaendaje
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee. Biashara ina changamoto nyingi, inaweza isikup return hata kwa mwezi mzima. Usifadhaike na haya maneno bali, jiandae na hali.

Kubwa kuwa na utambuzi wa maisha mapya utayokuwa nayo. Utambuzi huo pia ukurudishe kufanya tafiti ya biashara yako, ina hitaji mtaji wa kiasi gani, pesa ngapi zitatumika kusapoti biashara hiyo, kiasi gani niwe nacho ili maisha ya nyumbani na family kusiyumbe yumbe.

Then kaaa chini, ukipata hesabu yake, angalia fungu ulilo nalo, kam halitoshi weka malengo then make ukiwa na maono yako. Maono ndio ramani itayongoza, tabia zako, matumizi, rafiki zako n. K

Lakini kubwa zaidi mshirikishe mkeo, sidhani kama yeye ni kiazi hivo, kam uliweza kumshawishi ukaishi naye ili unaweza pia.

Kuna baraka kutoka kwa mke pia, jenga naye mipango, maan nyumbani kwako kukiyumba, hutoishi kwa raha na planz utaziua tu.

Moderate utayo mwambia kama waona ni muoga but mjuze, JUST MWAMBIE UNA PLAN NA NDOTO ZAKO, YA KUJENGA CHA KWAKO, SIO KUFANIKISHA NDOTO ZA WENGINE KWA UJILA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mtoa mada huu ushauri uzingatie Sana tena sana vinginevyo utakuja kutoa ushuhuda mwingine wa mateso.
Kwa sisi wazoefu wa hayo mambo tunaona mbeleni what will happen.
Watu huwa hawaachi kazi kizembe hivyo eti kwa ajili ya kutegemea biashara isiyo na guarantee.
Halafu Kama unajua ukiacha kazi mwenyewe huwezi kupata nssf yako huoni hyo ni hasara nyingine.
Sasa wenzako wakongwe huwa hatuachi kazi kwa staili hyo bali huwa tunafanya timing ili muajiri atuachishe mwenyewe.
Yaani unamfanyia visa Hadi anakuchoka na kukuachisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…