Kutoka Ufisadi hadi Uuaji: Tuwakubalie au Tuwakatilie...?

Shida CCM iliweza kwenye kueneza uchama wake vyombo vya dora.

Kuna siku kutaibuka upingamizi ambao waliopo kwenye vyombo hivi wengine sio wapenda CCM.
 
View attachment 3518831
Na. M. M. Mwanakijiji

Mstari Umechorwa
Mstari umechorwa ardhini; wauvuke au wasiuvuke, tuvuke tu tusiuvuke. Matukio yote ya kisiasa ya mwaka huu ambayo hitimisho lake lilikuwa ni Oktoba 29 yameacha ladha yenye ukakasi kwenye ndimi za Watanzania. Kuanzia kutiwa nguvuni kwa Tundu Lissu mwanzoni mwa mwaka huu hadi mauaji ya wananchi Oktoba Watanzania wanajikuta wanalazimika kufanya uamuzi katika fikra, hisia, na mitazamo yao. Maamuzi haya yanahoji jambo moja tu; tuendelee kuwakatalia au tusalimu amri na kuwakubalia watawala wetu na kuwapa kile wanachotaka.

Wanachotaka watawala wetu ni kutokuulizwa, kutokupingwa, na kutokukataliwa. Kati ya vitu vinavyowakera na kuwatifua nyongo ni kuambiwa "hapana". Watawala wetu hawa wamejiambia katika fikra, mawazo, na maono yao kuwa wao ni zawadi ya Mungu kwa Watanzania. Wameumbwa kututawala, wamebarikiwa na uzao wao kuwa juu yetu. Hawa jamaa wanaamini kabisa kuwa bila wao Tanzania haiwezekani.

Ni Yao Si Yetu
Bahati mbaya matukio ya Oktoba 29 na baadaye yametuonesha pasi ya shaka kuwa fikra hizi zimezama katika maono yao. Unapowasikia wakisema "Tanzania ni yetu sote" kama ambavyo tumekuwa tukiwasikia siku za karibuni kiukweli wanachomaanisha ni kuwa "Tanzania ni yao yote" na sisi wengine ni wapangaji. Tunaishi na tunatakiwa kuishi kwa huruma yao na kwa hisani yao. Tumeona jinsi gani watu wanatakiwa kutoa maelezo na vitambulisho ili kuweza kwenda popote. Imefika mahali watu wanataka kuzika ndugu zao lakini bado wanatakiwa wachague nani ataenda kutoa pole na usije ukatoa pole mahali usipotakiwa kutoa pole!

Tanzania hii ni yao. Japo hili linawezekana kuwa linaonekana kama uzushi fulani, kiuhalisia kuna ukweli hapa. Tanzania hii tunayoiona leo hii ni matokeo ya asilimia 100 ya utawala wa CCM na serikali zake. Sera zote, sheria zote, kanuni zote, mipango yote ya mikakati ni mazao ya fikra za utawala wa CCM. Chochote kinachoonekana kuwa ni mafanikio na vyote vinavyoonekana ni matatizo au mapungufu vyote ni matokeo ya utawala wa CCM. Tukiona watu wanapanga foleni na madumu ya maji, watu wanahangaika na foleni barabarani n.k vyote hivi ni matokeo ya utekelezaji wa sera za kisiasa zilizoundwa na chama kimoja tu - CCM. Hakuna nafasi hata finyu ya kubebesha lawama mtu mwingine yoyote au chama kingine chochote cha kisiasa.

Wanayo Sababu ya Kuwaogopa Watanzania
Hivyo tunapowapinga na kuwakataliwa kimsingi lazima wakereke na wawe na wasiwasi. Wanatambua kuwa hawawezi kukwepa lawama. Matukio yote ya kiufisadi kuanzia kashfa kubwa ya Loliondo mwanzoni mwa miaka 1990 hadi Kashfa ya Mauaji ya Oktoba yanatudokeza jambo moja kubwa - CCM imefika mahali pabaya zaidi kama chama tawala kuliko wakati mwingine wowote; kimevuka mpaka mmoja wa hatari na tusipoangalia tunakoenda kunatisha zaidi kuliko tulikotoka.

Kutoka Ufisadi Mpaka Uuaji
Tawala zote zenye misingi ya ufisadi mwisho wake huelekea uuaji. Utawala wa Kifisadi (Corrupt Regime) inaweza kuendelea kufanya hivyo kwa muda lakini unapofika wakati wananchi wanapoanza kuamka na kukataa ufisadi hasa wanapoona unahatarisha maisha na hatima yao watawala mara zote huelekea uuaji - kutoka ufisadi hadi uuaji - from corruption to termination. Hii ilikuwa kweli kwa Adolf Hitler, Joseph Stalin, Hafidh Assad na mwanae, Augustino Pinochet, Idi Amin Dada, Jean Claude Duvalier, Slobodan Milosevic, na bila kuwasahau utawala wa Khmer Rouge wa Cambodia. Na hapa siwezi kusahau utawala wa Kamuzu Banda.

Kinachotisha na kusikitisha ni kuwa sasa hivi CCM imefika hapa na sioni namna gani inaweza kujirudisha nyuma. Hili ni kweli hasa baada yamauaji ya Oktoba. Kwa miaka mingi tumekuwa tukihangaika na kesi mbalimbali za ufisadi. Huwa tunafuatilia ripoti za CAG kila mwaka na kuona jinsi gani watu hawa wanapiga kama wana akili mbovu. Mwakani hata hivyo, ripoti ya CAG haitoonesha mauaji. Kwa sababu kutoka ufisadi na upigaji watawala ili waendelee kukaa madarakani hawana namna ila kwenda kwenye uuaji.

Tumekopeshwa Uhai Wetu
Sasa hivi, Watanzania wanaishi kwa hofu, na wanaambiwa kama kuwa wasiwe na hofu kwa sababu serikali inawalinda. Kama nilivyodokeza huko nyuma baada ya kuonja damu, hawa jamaa wameongezeka hamu. Sasa hivi, hakuna atakayekuwa salama kila mtu sasa hivi ameazima uhai wake kwa CCM. Chochote unachofikiri unacho ni kuwa umekikopa tu; wakiamua kukichukua wenye nacho - ikiwemo uhai wako - huna cha kufanya, huna pa kukimbilia na hakuna wa kumwajibisha.

Sasa hivi watu wanaishi kwa hofu; nimesoma habari ya mhadhiri ambaye inadaiwa alisema kitu darasani huko UDOM kikamkuta kitu. Sasa ni lazima ujue kuwa siyo kila "rafiki" ni rafiki kweli, na hata wale wanaoitwa "ndugu" wanaweza wasiwe ndugu kweli. Sasa hivi ni mwendo wa kusalitiana mbele kwa mbele. Ili mtu apate baraka ya watawala inabidi achongee mwingine; ukitaka mambo yako yawe vizuri usiseme lolote kuhusu maandamano, mauaji, au kuonekana kuunga mkono vyama vya upinzani.

Maadui Wajao wa Dola
Na kama kinachohofiwa kitakuwa kweli - kufutwa kwa CHADEMA - yeyote ambaye ataonekana kuunga mkono CHADEMA au kuwaonea huruma ataonekana ni adui wa dola (ENEMY OF THE STATE). Huku tunakokwenda sasa hivi usimbeze Rais, usiseme kitu kibaya, usikosoe, usijaribu kufichua uovu, na usimnyoshee kidole mtu. Sasa hivi watu watapimwa kwa jinsi gani wanaimbwa kwa sauti kubwa "tunapinga mabeberu" na watajulikana kwa jinsi gani "wanamuunga mkono mama". Yeyote atakayekuwa kinyume na CCM, Rais, na yeyote atakayeonekana anapiga sana kelele kuhusu mauaji yaliyotokea atadaiwa kuwa ni adui wa dola.

Ni kwa sababu hiyo swali hili la kufungia mwaka linaenda kubakia. Watanzania wote tunaoitwa kufanya uamuzi; kukubali kutawaliwa wapendavyo au kukataa. Je, tukubali kufumba macho na kujifanya hatukikiona kilichotokea Oktoba ili tuwe na "amani" au tuendelee kupaza sauti zetu watu wawajibishwe na wawajibike. Tunaulizwa na historia - je tutaamua kukaa kimya na kugeuza macho yetu pembeni au na sasa tutakuwa kama yule Msamaria Mwema? Tutashuka juu ya punda wa starehe zetu na kumganga yule aliyejeruhiwa na kuachwa mahututi?

Je, tutaamuwa kwa miezi na miaka ijayo kuwaacha wafanye wanalotaka kwa yeyote, popote, na kwa vyovyote bila kuulizwa? Je, gharama ya kuwanyoshea vidole na kuwataja kwa majina tutakuwa tayari kuilipa au na sisi tuamue kukaa kimya ili mambo yetu yaende vizuri.

Je, tuko tayari tuachilie CCM Tanzania iendelee kutawala hata kwa risasi kwa miaka mingine sitini ijayo? Au tuwapinge na tulipe gharama ya kupinga huko?
Mbona tarehe 9 Desemba hakufa mtu?, tatizo vijana wa Gen Z walikubali kuingizwa mkenge na kudanganywa kuhusiana na uwezo wa JWTZ, walifanya maamuzi ya kichwakichwa bila ya kujipanga kwa kina.

Haiwezekani waingie mitaani kwa kudanganywa kwamba wanajeshi wanawaunga mkono kigezo kikiwa zile video za kutengeneza za Captain Tesha. Walitakiwa wafahamu kwamba jeshi linakula kiapo kwa Mheshimiwa Rais anapoapishwa lazima akague gwaride maalum ambayo ni ishara kwamba jeshi lina utii kwa Rais.

Hiyo dhana ya ufisadi imeshakuwa kongwe, yapo mengi sana yanayofanyika ambayo kwa kuyatazama tu unaona kuwa thamani ya mradi inakwenda sambamba na pesa inayotumika. Huwezi kuzuia kwa asilimia mia moja watendaji wa serikali wasiibe pesa ya umma ni ngumu sana.
 
Ukiangalia kwa jicho kali sana CCM Mizizi yake ipo kwenye dola

Kuanzia majeshi yote na idara za usalama
Wote hao ni watiifu kwa chama na wengine ni wanachama wa CCM

Kweli nguvu ya umma inaweza angusha tawala yoyote ile lakini je
tunaenda kwa style gani?

Bila raia kuwa na chuma hatutoboi Labda tu delay tujipange kimya ila kutangaza siku kuandamama ni kosa kubwa!
Kukosea wakati wa kwenda wakati wa kurudi hayafanyiki tena makosa. Tarehe 29 October ulinzi ulikuwa umesinzia kiaina waliposhtuka mchana wakazima mtandao.

Tarehe 9 Desemba ambaye angetoka kuandamana asingerudi nyumbani akiwa anapumua.
 
Mzee mwanakijiji kuwekuweko swali la kimkakati
"Je kuwafundishe watu wetu waanze kupeperusha bendera ya Tanganyika?
 
Wananchi wanaounga mkono "the status quo" kivitendo bado ni wengi. Ndo shida ilipo. Watanzania wengi wanaoengea mabadiliko ila wenye utayari wa kutenda mabadiliko ni very few.
 
Huu Uzi umeshiba sana kwanza nikupe pongezi za dhati ndugu Mzee Mwanakijiji.

Kwa kuwa Uzi wako umekuja kwa mfumo wa swali kwamba je "tuwakubalie au tuwakatalie" kwa mtazamo wangu jibu ni rahisi kwamba tumeshawakatalia

Sasa swali la pili kujiuliza ni kwamba mwanzo tuliwakatalia kwa njia ya heri ila matokeo yake wakaua ndugu zetu maelfu bila huruma, je kwa sasa tupo tayari kuwakatalia kwa njia ya shari?
Ngoja niusome nilikuwa napita pita juu juu
 
Ukiangalia kwa jicho kali sana CCM Mizizi yake ipo kwenye dola

Kuanzia majeshi yote na idara za usalama
Wote hao ni watiifu kwa chama na wengine ni wanachama wa CCM

Kweli nguvu ya umma inaweza angusha tawala yoyote ile lakini je
tunaenda kwa style gani?

Bila raia kuwa na chuma hatutoboi Labda tu delay tujipange kimya ila kutangaza siku kuandamama ni kosa kubwa!
Ccm tunawaonea, hawana nguvu hiyo, wenye nguvu wanajulikana, ccm wao ni frontliners tu
 
Say no demonstration , protect ur life

Msikubali wananchi kudanganywa kuwa mkiandamana mtalindwa

👇🏾
 
Attachments

  • Screenshot_20251220-071210_1766204935841.jpg
    Screenshot_20251220-071210_1766204935841.jpg
    368.7 KB · Views: 14
Mfumo unatiwa adabu walichofuma wenyewe! Wananchi ni victims lakini mbegu ya damu iliyomwagwq tar 29 itazaa matunda.

Swali kwa Mzee Nyerere? Unawezaje kuunda mfumo hatari kiasi hiki kwa kutegemea busara za binadamu mmoja? Sasa ni kama hatujui tunatokaje hapa zaidi ya kutegemea karma ya damu zilizomwagwa.
 
Mbona tarehe 9 Desemba hakufa mtu?, tatizo vijana wa Gen Z walikubali kuingizwa mkenge na kudanganywa kuhusiana na uwezo wa JWTZ, walifanya maamuzi ya kichwakichwa bila ya kujipanga kwa kina.

Haiwezekani waingie mitaani kwa kudanganywa kwamba wanajeshi wanawaunga mkono kigezo kikiwa zile video za kutengeneza za Captain Tesha. Walitakiwa wafahamu kwamba jeshi linakula kiapo kwa Mheshimiwa Rais anapoapishwa lazima akague gwaride maalum ambayo ni ishara kwamba jeshi lina utii kwa Rais.

Hiyo dhana ya ufisadi imeshakuwa kongwe, yapo mengi sana yanayofanyika ambayo kwa kuyatazama tu unaona kuwa thamani ya mradi inakwenda sambamba na pesa inayotumika. Huwezi kuzuia kwa asilimia mia moja watendaji wa serikali wasiibe pesa ya umma ni ngumu sana.

Wabongo hawajajifunza vya kutosha kuhusu mbinu za civil disobedience. Wakizijua itakuwa ni disaster.

Ipo namna ya "kuikera" serikali mpaka ikubali kukaa chini na kuleta mabadiliko.
 
Ccm kwa sasa ni mhimili wa 4 wa hii nchi.
 
Wabongo hawajajifunza vya kutosha kuhusu mbinu za civil disobedience. Wakizijua itakuwa ni disaster.

Ipo namna ya "kuikera" serikali mpaka ikubali kukaa chini na kuleta mabadiliko.
Wamejifunza kutokana na kilichotokea October 29, wamepoteza ndugu zao wameiona damu inavyomwagika na umaskini unavyoweza kuingia haraka sana baada ya vita kuruhusiwa ikatawala.

Ukiona kijana bado anatamani sana maandamano mchunguze, utagundua ni msela tu hana cha kupoteza anakula kwa Baba analala kwa Mama, hana majukumu yoyote.

Sio kwamba watanzania wanaipenda sana CCM la hasha, hawataki kupoteza amani yao waliyoizoea, hawataki aina ya maisha ya mateso huku wakijua fika yamesababishwa na wajinga fulani wanaojikomba kwa mataifa ya Ulaya.
 
Ni njia gani halali wananchi wanaweza kuitumia kuitoa CCM madarakani?
 
Back
Top Bottom