Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,786
Kauli Mbiu Kuu Ya Kongamano Hilo.
Wanawake Wanaweza,Waliweza Na Wanaendelea Kuweza.
Mwezeshaji:Ndg.Humphrey Polepole
Hakika Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimepata Katibu Wa NEC Itikadi Na Uenezi Mwenye Uwezo Mkubwa Mno Katika Kujieleza,Kuelezea,Kufafanua, kuelimisha na KUSHEREHESHA.
Hakika Kipawa Chake Kikubwa na Uzalendo Mkuu Alionao Unajieleza Kila Uchao.
Akinogesha Kongamano hili la GIRL POWER CONFERENCE 2020,ndg.Humphrey Polepole Aliwaalika Mabinti na Wanawake Wa Kitanzania Ambao Wamekuwa Chachu Ya Kupigiwa Mfano Kwa Wanawake Na Mabinti Waliothubutu nchini Kwetu Tanzania.
Mkononi nikiwa na kinywaji changu Pendwa cha Al Kasus Nililifuatilia tukio lile nyuma ya Seti Yangu Ya Televisheni nyumbani kwangu na Kuguswa Juu Ya vile Vipawa Mujarabu vya Wanawake Wa Kitanzania Ambao ni nadra kufafanuliwa katika makongamano "AILA" ya Hili.
Makongamano ya namna hii yakiendelea kuandaliwa na kurushwa hewani kila mwaka,ni hakika yatawapa CHACHU Wadogo zetu wa kike,wapwa zetu,vitoto vyetu vya kike vinavyokua,WAJITAMBUE,WAJIAMINI,WAUONE UWEZO WAO MKUBWA WALIOPEWA NA MUNGU MUUMBA.
Makongamano ya NGUVU ZA MTOTO WA KIKE,yataendelea kuwa TAA IMULIKAYO kwa Mabinti wa Kitanzania waone kuwa UHUNI,STAREHE ZA KUPITILIZA,KUJIUZA a.k.a KUDANGA,UMAARUFU KOKO MITANDAONI,uvivu,njia za mkato,kupendelewa,kubebwa,ni Mambo yanayoweza kuepukika wakiamua kujiepusha kwa usalama wao na wa taifa letu pendwa.
Mgeni Rasmi Makamu Wa Rais Mh.mama Samia Suluhu Hassan Aliwakumbusha wahudhuriaji ambao wengi wao ni Rika la wasichana kuwa waamue kujitambua wabadilike,watangulize NIDHAMU,heshima,Adabu na kujichunga ili waweze kuzifikia na kuzitimiza NDOTO ZAO.
Kwa nyakati tofauti ndg.Humphrey Polepole aliburudisha masikio ya wasikilizaji alipowahoji Kamanda Mstaafu Wa Jeshi La Wananchi Wa Tanzania(JWTZ) Meja Jenerali Mstaafu Mama Madawili akiambatana na Mkuu Wa Askari Polisi Wanawake Nchini aliye pia Mkuu Wa Dawati La Jinsia SCP Kamishna Mary Nziku,Kamanda Mkuu Wa Uhandisi na Lojistiki Jeshini Brigedia Jenerali Kodi na Ambaye ndiye Afisa Mwanamke Mwenye Cheo Cha Juu kuliko wote waliopo bado Katika Utumishi.
Ikumbukwe huyu Meja Jenerali mstaafu Madawili ndiye aliyekuwa anamuINSPIRE Brigedia Jenerali Kodi Mpaka Kufikia Hapo Alipo.
Mama Madawili aliwakumbusha wahudhuriaji juu ya UMUHIMU wa kutunza AMANI YA NCHI,akiwaeleza ya KUWA AMANI HII TULIYONAYO imetengenezwa kwa muda mrefu mno na kuipoteza ni Jambo jepesi tu.
Alieleza kuwa amani huweza kupotea kwa sababu za migongano ya KIKABILA,KIDINI NA KISIASA.
Aliwaasa waendelee "kuiengaenga" kwa faida ya kila Mmoja wetu akiwashangaa wanaosema wao kuwa "kukinukisha" huwa ni heri pale ambapo matakwa yao binafsi yanakuwa MSAMBWENI kinyume Cha matarajio Yao.
Katika Panel Alikuwepo Katibu Mkuu Dr. Zainab Chaula Ambaye Kwa Unyenyekevu Mkubwa Alijibu Maswali Ya Humphrey Polepole na kutukumbusha kuwa ndiye aliyekuwa GREDA la ujengwaji wa hospitali za Wilaya, Vituo Vya Afya na Zahanati Zilizojazana Chini Ya Awamu Hii ya Kutukuka ya Mh.Rais John Magufuli.Hakika Wanawake Wanaweza,na Dr.Zainab Chaula Amewadhihirishia Wadogo Zetu wa kike Ambao Kutwa Wanaona Maisha ni Yale tu Ya INSTAGRAM, kupata views YouTube tu na kutaka kuishi maisha ya Kina Giggy Money na ya baadhi ya wasanii wetu ambao wengi wao hawaishi maisha asili(faking life).
Katika kongamano Hilo walikuwepo Madaktari Bingwa wawili ambao ni Vijana Wa Kike Wanaofanya Kazi Hospitali ya Taifa Ya Muhimbili,mmoja akiwa kitengo Cha Magonjwa ya ndani(internal medicine) na mwingine akiwa ni daktari pekee wa Kike Anayepasua Moyo Na Mishipa Ya Damu Mwilini(Cardiovascular Surgeon)pale JKCI iliyo Chini ya Prof.Mohamed Janabi.Akinadada Hawa Waliwatia Hamasa Ndugu Na Wadogo zao wa kike kwa kule "KUTOBOA"na kuvumilia mengi ya kimaisha kuweza kusoma na kufika hapo WAKIWA na umri mdogo kabisa.
Huyu Daktari Mpasuaji Wa Moyo, Aliamua kwenda tena kusoma nchini Urusi Miaka 5 mengine kufanikisha ndoto zake kuntu baada ya kuwa amefanya kazi pale MAPOKEZI ya Muhimbili akiwa na shahada yake ya Kwanza aliyoipata Pale Chuo Cha Taifa Cha Tiba Muhimbili(MUHAS) baada ya Kupambana miaka 5 na mwaka mmoja wa VITENDO(internship)Kabla ya kupata leseni yake ya kututibu watanzania.
Hii Yote Inadhihirisha kuwa Mtoto Wa Kike Akiamua ANAWEZA kuyafanya makubwa ZAIDI yetu tunywao Al Kasus Kwenye Maskani na vijiwe vyetu Uswahilini,kucheza michezo ya Bao,Draft,Keram,KuBET, na Ile Tabia Yetu kuu Ya Kugonga Faru John Kwa Kwenda Mbele ambako watoto wa KIUME na sisi Kaka zao ndiyo Mambo tuyafanyayo Kwa Wingi Zama hizi.
Mbali na hao niliowataja Hapo Juu Alikuwepo Mwanamke Kijana Wa Miaka 32 Aitwaye Miss Bomani ambaye kwa miaka 9 MFULULIZO toka 2011 amekuwa ni rubani wa kurusha ndege za hapa nchini kuanzia mashirika madogo mpaka muda huu akihudumu ATCL kwa kuendesha ndege kubwa DREAMLINER.Dada huyu pamoja na ulimbwende wake na kuwa mke na mama wa watoto wawili hakukata tamaa kufika hapo alipo na Hili hapa liwasukume Wadogo zetu wa kike wakitanzania walioko shule za msingi,sekondari,vyuo vya Kati,vyuo vikuu,wanaopata na wasiopata bumu"tamu"kutoka HESLB Kama hisani ya Serikali Yao iliyodhamiria kwa moyo mweupe kuwainua waipuuze hii michezo ya KUTUMIKATUMIKA HOVYO KINGONO na masponsa kwa AJILI eti ya kupata hela za kununua Vijora na Wigi,hakika haya ni Mambo ya kuachwa kufanywa na kuyakomesha Mara moja kwani wao Wana thamani kubwa ZAIDI ya hayo mambo ya "kifulafula" "kizwazwa"na "kindwanye".
Sambamba na huyo rubani wetu Alikuwepo pia Profesa wa Kike Mdogo Nchini Kuliko Wote Jina nimelisahau ambaye katika umri wa miaka 41 ya Uhai wake ameshakusanya SHAHADA 3,akizamia katika masuala ya maendeleo ya fedha uchumi na UWEKEZAJI.
Dada Yetu Shilole Shishibebe naye aliwapagawisha wahudhuriaji kwa kuwaeleza uthubutu wake katika maisha, toka safari yake kutoka Igunga,muziki,na upambanaji wake bila ya kuchoka ili kufikia Malengo YAKE ya ujasiriamali wa kupigiwa mfano.
Alikuwepo binti mdogo mwanamuziki wa kike mwenye miaka 17 na akiwa na ndoto za kuwa daktari wa binadamu siku za mbele.Binti Huyu anauwezo mkubwa wa kuimba na kupiga VYOMBO vya muziki mbalimbali.Binti huyo amejitolea kufundisha wasichana wenzake nao waufahamu muziki vile anavyoufahamu yeye.
Hakika Kongamano lile lilinisisimua mno kwa kuona kuwa hii serikali yetu ya awamu ya 5 ikidhamiria kuwapa SHIME watoto wa kike popote walipo kwa Kuwakumbusha kuwa WANAWEZA KUFIKA WANAKOTAKA.
Mtoto wa Kike Wa Kitanzania Akiamua Kwa Dhati Ya Nafsi yake hahitaji Tena KUWEZESHWA ili aweze bali aamue tu, na Akiamua ANAWEZA,ALIWEZA NA ATAENDELEA KUWEZA.
Viva Tanzania,
Siempre Siempre Watoto Wa Kike.
Hasta la Victoria- Girl Power Conference 2020.
Aluta Continua.
Ndimi Kaka Yenu,
Muuza Al Kasus,
Jumbe Brown,
Tandale Kwa Mtogole.
02/08/20