Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Tecnolojia zaidi urongo mtupu eti anatutolea mfano Tanga leo wanavyomuangali,hao si ni wale wa mjini tu,wa vijijijini huko bumbuli hamna kitu


Lakini sio kweli kuwa wanaweza kuuliza maswali live toka walipo??
 
Nilipoanza kuangalia nikasema hakika January makamba kichwa anaongea hivi bila kusoma basi huyu ni hatari

Kumbe dume limeweka Hotuba kwwnye secreen linasoma.

.....

Tv toka ukutani jamaa akisoma
 
kule kusema tanzania mpya inamaanisha tanzania ya sasa ni kuukuu.
la kujiuliza ni nani sasa kaifanya tanzania kuchakaa na kua kuukuu km cyo chama chao kilichotufikisha hapa.na kwa yy kusema hivi inamaana kwa jicho la pili anaunga mkono kauli ya upinzani kuwa ccm imechoka.sasa km analijua hili na kuliweka km kipaumbele je asipopitushwa atatoka kwa hai wachakaza nchi? sidhani,ni mnafiki na hizi kauli nu mbinu za kuchumia tumbo
 
Kamanda kuniambia nikauze pweza ndiyo kanirarua Ahahaha mimi mbona muuza kahawa tu pweza kanikweza sana.

Kwa hiyo kamanda Chadema hawana haja na kura za wauza pweza?

Teh teh teh teh

Teh Teh Kamanda ana tekeleza sera ya chadema!
 
Vituo vya ki Olympic? Hajui walimu hawana ata nyumba, hajui maabara zenyewe ni ishu.. Yani huyu kama ni siasa za uongo Katia fora anafikiri Tanzania yote ni sinza na mbezi!
 
Ndo ukweli huo. Kuporomoka from.80 to 60 si haba
Kwa hiyo Usalama wa Taifa waliiba kura za urais tu za Ubunge na Udiwani hawakuiba? sasa mngeshinda urais mngeongozaje na wabunge 23.
 
Kwa mtazamo wangu miaka 50 baada ya uhuru sera za ccm zimeshindwa. Kina Makamba wanazungumza mipango yao lakini wakishaingia madarakani wanatakiwa watekeleze sera za chama ambazo hatupeleki kokote. Ukweli sasa nchi inahitaji sera za chama kingine
 
Na wewe unaamini mwaka 2010 Dr.Slaa alishinda urais Usalama wa Taifa wakaiba kura zake?

Mbona haieleweki kwa hiyo upo tayari kuachana na Dr.Slaa na kujiunga na Mako Nyerere safi sana.

Mbona hujajibu hoja ya Dr slaa kagombea mara ngapi Chadema? Kulinganisha na makada walafi kama lowasa, mwandosya nk
 
hilo swali la Foleni amelijibu kwenye kitabu chake alichotoa juz kati....na ndivyo anavyojibu hapo
 
Aisee..... so mawaziri 18..... katiba ilopendekezwa na chama chake kinataka mawaziri wangapi vile?
Hapo tafsiri yake ni kuwa anaiponda ile katiba yao pendekezwa ya Lumumba, iliyoandikwa na nyoka mwenye makengeza, ambayo inatoa ruksa ya zaidi ya.mawaziri 30.

Kwa January kutuambia kuwa ataunda baraza la mawaziri wasiozidi 18, maana yake anaiunga.mkono Rasimu ya Tume ya Warioba ambayo ilipendekeza mawaziri wasizidi 18.

Kwa hiyo kwa kauli yake hiyo amewaunga mkono indirect Ukawa kwa kususia BMK!
 
Huyu kijana anatoa hotuba mwishoni mwa wenzake. Kwa maana hiyo alikuwa na nafasi ya kusahihisha hotuba yake iwe bora kuliko zile za wengine.Nahisi alidhani anaweza akatoa hotuba ambayo ni philosophical kama ya Obama ambayo iligeuza muelekeo wa Wamarekani. Hii ya Makamba ni hovyo.Ni muendelezo tu wa hotuba za hovyo zilizokuwa zikitoka ikulu.

Mambo mengi aliyoyasema ni qualitative. Mtu anazungumzia kuboresha uchumi bila kusema atafanyeje. Ataongeza kipato cha taifa, bila kusema ni kwa njia ipi. Hata hivyo hayo yote ni premature. Hatuyahitaji hatua hii.

Hatua hii alihitaji kuwaeleza wana CCM wenzake ni jinsi gani atapunguza wizi na ufisadi wa viongozi wao. Alistahili atueleze jinsi gani atakifanya chama hiki cha zaidi ya miaka 30 au 50 tangu enzi za TANU, kiwe na watu wanaojitegemea badala ya watu wanaokitegemea na ndo mwanzo wa wizi wa mali ya umma. Angetueleza CCM yake itakuweje tofauti na CCM ya Kikwete, Mkapa; mwinyi na Nyerere? Tatizo eti anaona Mkapa na Kikwete ndo mfano mzuri wa uongozi na ndiko alikojifunza siasa naye anataka afanye hivyo. Shiiit!

Kwa ujumla watangaza niya wote wameshindwa kabisa kuelewa hizo hotuba zao kwamba ni kwa wana CCM. Wameishia kutoa hotuba utadhani wanaomba kura za watanzania wote. Kwa kuwa ameshindwa kusema ya maana baada ya miaka yote hii ya kuwa naibu waziri, hata akipewa nafasi ya urais, anaonekana ni mtu asiyeweza kujifunza haraka.

Moja tu, napma pongezi kwa kuonyesha niya maana hiyo inampa nafasi ya kuonekana ili rais ajaye ampe hata uwaziri.
 
Huyu jamaa maneno meeengi kama vile tapeli.

Kiongozi bora haongei kama maporomoko ya maji.
 
Inachekesha.....mara safari ya matumaini...hooooo twende na Membe, Tanzania mpya....kauli zote ni ki-ukawa tu, as hawakuwa sehemu ya serikali hii dhaifu!
 
Ngoja waje watakaompa sifa kwamba ni kichwa (kwa sababu sijui katoa hotuba bila kuisoma).

Wengine watakuja na mada za kuwa 'inspired' na hotuba yake.
 
Bora kaja ki digital zaidi inatumikaga sehemu nyingi hii njia kwenye presentations.

Naona mwenzangu ila matangazo yake yanakatakata sana leo sijui mafundi mitambo wana matatizo gani.
 
January amejipanga vizuri.
Ukizingatia yeye ni naibu wazir sayansi na teknlojia.
Ametumia tecknolojia kuwasilisha hotuba yake.

Matangazo live kutoka dar, na mikoani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…