Huyu kijana anatoa hotuba mwishoni mwa wenzake. Kwa maana hiyo alikuwa na nafasi ya kusahihisha hotuba yake iwe bora kuliko zile za wengine.Nahisi alidhani anaweza akatoa hotuba ambayo ni philosophical kama ya Obama ambayo iligeuza muelekeo wa Wamarekani. Hii ya Makamba ni hovyo.Ni muendelezo tu wa hotuba za hovyo zilizokuwa zikitoka ikulu.
Mambo mengi aliyoyasema ni qualitative. Mtu anazungumzia kuboresha uchumi bila kusema atafanyeje. Ataongeza kipato cha taifa, bila kusema ni kwa njia ipi. Hata hivyo hayo yote ni premature. Hatuyahitaji hatua hii.
Hatua hii alihitaji kuwaeleza wana CCM wenzake ni jinsi gani atapunguza wizi na ufisadi wa viongozi wao. Alistahili atueleze jinsi gani atakifanya chama hiki cha zaidi ya miaka 30 au 50 tangu enzi za TANU, kiwe na watu wanaojitegemea badala ya watu wanaokitegemea na ndo mwanzo wa wizi wa mali ya umma. Angetueleza CCM yake itakuweje tofauti na CCM ya Kikwete, Mkapa; mwinyi na Nyerere? Tatizo eti anaona Mkapa na Kikwete ndo mfano mzuri wa uongozi na ndiko alikojifunza siasa naye anataka afanye hivyo. Shiiit!
Kwa ujumla watangaza niya wote wameshindwa kabisa kuelewa hizo hotuba zao kwamba ni kwa wana CCM. Wameishia kutoa hotuba utadhani wanaomba kura za watanzania wote. Kwa kuwa ameshindwa kusema ya maana baada ya miaka yote hii ya kuwa naibu waziri, hata akipewa nafasi ya urais, anaonekana ni mtu asiyeweza kujifunza haraka.
Moja tu, napma pongezi kwa kuonyesha niya maana hiyo inampa nafasi ya kuonekana ili rais ajaye ampe hata uwaziri.