Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Mimi huwa najiuliza, kwa nini wakina nyerere walikuwa wadogo kuliko hawa vijana watia nia lakini hawa wengi weupe saana. Lawama nyingi tu. Ngoja aje.

akili kubwa iko nje ya systema angalia mwangosi, na wenzake wako wap?
 
Hakuwa na haja ya kusahihisha lolote lile. By the way, Januari sio wa mwisho kutoa hotuba. Watangaza nia wapo zaidi ya 25 hadi sasa.

Alichosema kwa mwenye akili atamuelewa, kwa wagonjwa wa akili ni wazi kabisa sio rahisi kuelewa zile nondo za Januari.
 
Huyu jamaa alianza kusema atatekeleza ilani ya chama ingawaje haizuii kuongeza ya kwake ambayo ndio haya anayotueleza. Kwa ahadi zake hizi zilivyo nyingi akichanganya na zilizo kwenye ilani si atakimbia nchi huyu!!!!.
 
Nampongeza hapo kwenye kujenga njia ya reli za usafiri wa ndani Dar,hapo kweli katoa idea nzuri tena sana.
 
Makamba kaongea vizuri sana ila tatizo muislam. Nchi hii kumpa muislam tena ni sawa na kuiingiza jehanamu tuliyoyaona 2005-2015 yanatosha.
 
Tatizo letu siyo yupi anaweza kumeza nondo bila kusoma...tunataka mtu akataye simamia rasilimali za taifa hili ziweze kutusukuma katika maendeleo na kutunufaisha kila mmoja kwa namna yake.

ndio maana nimesema kwa sera, sijasema anavyoenda kuzitekeleza!
huyo unautaka HAYUPO.
 
Ngoja waje watakaompa sifa kwamba ni kichwa (kwa sababu sijui katoa hotuba bila kuisoma).

Wengine watakuja na mada za kuwa 'inspired' na hotuba yake.

January Makamba si kichwa uelewa wake ni mpaka akariri sana!!
Jamaa anavitabu vingi sana, mbaya anasoma kwa kuiga ili na yeye aonekane msomi.
 
Mpaka sasa kiongozi anayefaa kutoka ccm ni Makongoro pekee, sababu yeye ndio ameonyesha kulijua tatizo la nchi hii UFISADI. Na amejitolea kupambana nalo.

January anataka kutuaminisha nchi hii imekwama sababu hatuna mipango ndio maana ahadi nyingi zisizotekelezeka hajaweka nguvu yoyote kwenye mkwamo wetu ulipo. Hana jipya kabisa na hii mipango yake yote haifui dafu mbele ya ufisadi.
 
Skype imeshindikana..... Wakaamua kutumia Telephone.
 
skype imewashinda,hahahaha tecnolojia magumashi tu
 
January Makamba mkuu tunakupenda sana lakini hizi ni AHADI zisizowezekana. Eleza kwa kina juu ya mtazamo wako na hali halisi.

AFYA:- Ujenzi wa Hospital za Kimataifa unatangulia bima ya Afya, huwezi kuwa na bima ya Afya wakati kuna huduma mbovu mahospitalini na ndio maana wenye uwezo wanakimbilia India kutibiwa. Mama waja wazito wanakufa ama watoto wao wakiwa na bima zao mikononi. Asilimia 60 kama sio zaidi ya wananchi wanaoishi kwa Dola moja kwa siku hawataweza kumudu gharama tanzania ni nchi maskini sio nchi tajiri. Kufuata mfumo wa Soko Huria haina maana ya Ubepari!..
ELIMU ya JUU:- Ulipokuwa naibu waziri uliwawezesha vijana kiasi gani katika ngazi hiyo na kama ilishindikana tupe sababu?
RUSHWA:- Mkakati gani ulokuwa nao kupambana na rushwa, bado ni maneno matupu
MAJI:- Asilimia kubwa ya wananchi wanatumia maji ya visimani, kutumia miradi ya TANROAD sidhani kama ni fikra yakinifu na sii maamuzi sahihi ikiwa Rushwa imetawala katika sekta hizo

Mengineyo.
1. Kuhaidi mawaziri 18 ni mfululizo wa Katiba pendekezwa isokubalika na wananchi pia ni ngumu kupita CCM kwenyewe kila mtu anaotegemea kuchukua chake Mapema na nafais zenyewe ndio hizo.
2. Kupunguza misamaha pekee haitupi picha kamili. Ni sehemu gani misamaha hiyo itaondolewa/hupunguzwa? Je, ni Miradi ya wawekezaji wa nje? NGOs au taasisi gani?
3. KODI:- Sawa utaondoa kodi kabla biashara kuanza, Je, utaweka utekelezaji gani badala yake ikiwa serikali haiwezi kukadiria pato la mfanyabiashara kihalisia?. Leo hii mashine za kodi hazionyeshi kodi ni kiasi gani kwa kila unachonunua ama kuuza ila unaambiwa tax is included.. at what Percentage unaambiwa 20% lakini haipo on record ya lisiti, jambo ambalo mfanyabiashara hakulipangia bei zake. Mimi ni muathirika wa mfumo mbovu wa kodi nchini..
4. Wafanyabiashara wangapi wanajua ili uwakilishe kodi zako ni lazima zitengenezwe na mhasibu kuweza kulinganisha kodi alizokusanya na kozi alizolipa? (Elimu ya kodi hakuna) Form za kodi hakuna, hakuna muda maalum wa kulipa ama kujaza malipo ya kodi kwa wananchi wote - Kifupi njia pekee ni kufumua mfumo mzima na kuanza Upya!
5. Mradi wa makaa ya mawe tayari upo katika mpango wa maendeleo wa taifa na umeshaanza utekelezaji wake.
 

Hotuba kuwa Nondo au uchafu inategemea wewe ni mtu wa aina gani. Kwangu mimi pia sikuona la kusifia maana mbele yake kuna wenzake zaidi ya 20 na hakustahili kuwa hovyo kama wenzake.

Kwa nini anahutubia wa TZ wote badala ya kusema yanayowastahili wana CCM wenzake? Sisi wengine tunaona jinsi CCM inavyovuruga nchi naye lazima anayo mambo ambayo ndani ya CCM anayatilia mashaka au kutoyaamini. Anasemaje juu ya hayo ili Wana CCM wenzake wamuone kwamba anawafaa?
 
Nikimlinganisha na Hamis Kigwangala naona huyu nimtupu kabisa.

Kigwangala walau ukimwangalia machoni alimaanisha alichosema sio huyu jamaa wa mastori.
 

Nondo wapi wewe mzee Hamza!!
nini hapo ulichokiona nondo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…