JANUARI ATATOA HOTUBA HII BILA YA KUSOMA POPOTE. HOTUBA YOTE IPO KICHWANI.
- Januari anasisitiza kuwa Tanzania MPYA itajengwa na viongozi wenye fikra mpya.
- Januari ahaidi kuwa na mawaziri wasiozidi 18 tu katika baraza lake la mawaziri endapo chama chake kikimpa ridhaa ya kugombea urais kupitia CCM.
-
Januari Makamba anaorodhesha ajenda tano kuu atakazo simamia endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea na hatimae kuunda serikali.
............Update............
....Januari ahaidi kuwa serikali yake itatoa mikopo maalumu kwa vijana watakaomaliza vyuo vikuu ambao watapata changamoto ya ajila ili na wao waweze kufungua makampuni yao ili waweze kujizalishia kipato.
....Pia amesema katika serikali yake atahakikisha sekta ya nyumba ina mchango wa zaidi ya 25%, wakati sasa hivi ni chini ya 4% ikimaanisha Watanzania wengi hawana makazi. Hivyo katika uongozi wake hilo la makazi atalipa kipaumbele tofauti na ilivyo sasa.
....UVUVI, serikali yake itaanzisha mifuko maaalumu ya kukopesha wavuvi ili waweze kununua vifaa vya uvuvi ili isaidie kuboresha vipato vya wavuvi na pia kukuza sekta hiyo kwa kasi.
....UHABA WA WALIMU, serikali yake itaongeza udahili wa walimu haswa kwa masomo ya sayansi. Pia ameahidi kutatua changamoto za walimu kama vile mishahara yao kuwa duni, kukosa posho na stahiki mbalimbali. Ahaidi serikali yake kutatua kero hizo kwa kukuza na kuboresha maslahi yao.
.... RUSHWA, amesema kuwa kulizungumza na kulipigia kelele tatizo la rushwa sio njia ya kulimaliza tatizo hilo.
...ARDHI, jinsi ya kuondoa migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Serikali yake itabainisha kisheria maeneo ya kilimo, mifugo na makazi. Pia amesema wakulima na wafugaji watamiliki maeneo yao kisheria. Atatumia teknolojia mpya ya satellite kutekeleza hayo kupitia kituo maalumu kitachoundwa chini ya serikali yake. Lakini pia kituo hicho kitasaidia pia na mambo ya kiusalama.
....AFYA, kila Mtanzania lazima awe na bima ya afya, kila Mtanzania lazima apate huduma bora ya afya bila ya kujali kipato chake.
....MAJI, wakala na mfuko mpya wa maji utaanzishwa vijijini. Hapa kukazia hoja yake, ametolea mfano wa mawakala kama wa barabara (TANROADS) na wakala wa umeme vijijini (RERA) kuwa mafanikio makubwa yamepatikana kupitia uwepo wa mawakala hao. Hivyo sasa kuna haja ya kuwa wna wakala wa maji vijijini. Ahaidi ndani ya miaka kumi kusogeza hudumasafi na salama aya majikwa kaya karibu zote nchini.
....MAPATO YA SERIKALI, hapa anazungumzia namna atakavyopata fedha za kutekeleza ahadi zake. Mambo atayofanya ni yafuatayo:
1. Atahusisha sekta binafsi kwa kina zaidi ambapo serikali haina ulazima kutumia fedha zake yenyewe katika kutekeleza miradi mbalimbali.
2. Kupunguza misamaha ya kodi kufikia 1% ya pato la taifa. Ambapo serikali itaweza kupata kiasi cha kisichopungua bilioni 700 pesa za Tanzania.
3. Kupanua wigo wa kodi, hasa kwenye sekta isiyo rasmi. Serikali yake itaondoa mfumo wa sasa wa kutoza kodi kabla hata ya biashara kuanza. Pia ataweka adhabu kubwa kwa watakaokwepa kodi.
4. kuongeza ufanisi wa TRA, amenukuu rpoti ya kitaalamu iliyohitimisha kuwa TRA kama ikiongeza ufanisi wa asilimia 10% tu, itaongeza ukusanyaji wa kodi kiasi cha bilion 600 kwa mwaka.
5. Mradi wa makaa ya mawe, serikali itapata kiasi cha bilion 800 kama utafanywa kwa ufanisi zaidi.
6. Kila mwenye ardhi yenye hati atatozwa kodi stahiki, kiasi cha bilion 500 kitapatikana hilo likifanikiwa. Hapa ili afanikiwe atahakikisha kwamba wizara ya ardhi inashirikiana na sekta binafsi kupima ardhi ili kumilikisha watu wengi zaidi ili serikali iweze kupata mapato kutokana na ardhi hiyo iliyopimwa.
7. Sekta ya nyuki itatoa bilion 130 kwa mwaka kama itapewa kipaumbele.
8. Meli nyingi za kimataifa hazilipi kodi, serikali yake itarekebisha sheria ya uvuvi ya bahari kuu ili kuongeza mapata kiasi cha bilion 350 kwa mwaka.
.......Update.......
January Makamba mkuu tunakupenda sana lakini hizi ni AHADI zisizowezekana. Eleza kwa kina juu ya mtazamo wako na hali halisi.
AFYA:- Ujenzi wa Hospital za Kimataifa unatangulia bima ya Afya, huwezi kuwa na bima ya Afya wakati kuna huduma mbovu mahospitalini na ndio maana wenye uwezo wanakimbilia India kutibiwa. Mama waja wazito wanakufa ama watoto wao wakiwa na bima zao mikononi. Asilimia 60 kama sio zaidi ya wananchi wanaoishi kwa Dola moja kwa siku hawataweza kumudu gharama tanzania ni nchi maskini sio nchi tajiri. Kufuata mfumo wa Soko Huria haina maana ya Ubepari!..
ELIMU ya JUU:- Ulipokuwa naibu waziri uliwawezesha vijana kiasi gani katika ngazi hiyo na kama ilishindikana tupe sababu?
RUSHWA:- Mkakati gani ulokuwa nao kupambana na rushwa, bado ni maneno matupu
MAJI:- Asilimia kubwa ya wananchi wanatumia maji ya visimani, kutumia miradi ya TANROAD sidhani kama ni fikra yakinifu na sii maamuzi sahihi ikiwa Rushwa imetawala katika sekta hizo
Mengineyo.
1. Kuhaidi mawaziri 18 ni mfululizo wa Katiba pendekezwa isokubalika na wananchi pia ni ngumu kupita CCM kwenyewe kila mtu anaotegemea kuchukua chake Mapema na nafais zenyewe ndio hizo.
2. Kupunguza misamaha pekee haitupi picha kamili. Ni sehemu gani misamaha hiyo itaondolewa/hupunguzwa? Je, ni Miradi ya wawekezaji wa nje? NGOs au taasisi gani?
3. KODI:- Sawa utaondoa kodi kabla biashara kuanza, Je, utaweka utekelezaji gani badala yake ikiwa serikali haiwezi kukadiria pato la mfanyabiashara kihalisia?. Leo hii mashine za kodi hazionyeshi kodi ni kiasi gani kwa kila unachonunua ama kuuza ila unaambiwa tax is included.. at what Percentage unaambiwa 20% lakini haipo on record ya lisiti, jambo ambalo mfanyabiashara hakulipangia bei zake. Mimi ni muathirika wa mfumo mbovu wa kodi nchini..
4. Wafanyabiashara wangapi wanajua ili uwakilishe kodi zako ni lazima zitengenezwe na mhasibu kuweza kulinganisha kodi alizokusanya na kozi alizolipa? (Elimu ya kodi hakuna) Form za kodi hakuna, hakuna muda maalum wa kulipa ama kujaza malipo ya kodi kwa wananchi wote - Kifupi njia pekee ni kufumua mfumo mzima na kuanza Upya!
5. Mradi wa makaa ya mawe tayari upo katika mpango wa maendeleo wa taifa na umeshaanza utekelezaji wake.