Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

JANUARY MAKAMBA NI MBUMBUMBU WA SUALA LA GESI NCHINI

Nimemsikiliza January Makamba akizungumzia suala la gesi na manufaa yake kwa nchi.

January anasema gesi iliyopo nchini haiwezi kuwanufaisha Watanzania hata baada ya miaka 10 ijayo akimaanisha kuwa bado mapato yake yatakuwa hayajaanza kupatikana! !

Nimeshangazwa na kauli hiyo inayodhihirisha u mbumbumbu wake katika suala zima la gesi nchini.

Makamba hajui kwamba hata sasa Watanzania wameshaanza kunufaika na gesi!

Mtoa nia huyu hajui kwamba pale Mikocheni kwenye nyumba za TPDC kuna Bomba la gesi inayotumika kupikia!

Makamba hajui kuwa hata Kiwanda cha SAO HILL kilichopo Dsm kinatumia gesi!

Kijana huyu anayeomba ridhaa ya Chama chake kuiongoza nchi, hajui kwamba kuna umeme unazalishwa kwa gesi hapa nchini hususan unaotumika mikoa ya Kusini!

Hiyo ni mifano michache tu inayodhihirisha kwamba Makamba hana ufahamu wa suala hili muhimu na hivyo ninapata wasiwasi kama anafaa kwa nafasi anayoiomba.

Namshauri Makamba asikilize Hotuba ya Profesa Muhongo wakati akitangaza nia hususan kwa suala la gesi.

Profesa Muhongo alieleza kwa ufasaha, kwa kina na takwimu jinsi gesi itakavyonufaisha Taifa na Watanzania kwa ujumla. Tujifunze kutoka kwa mtaalamu huyu mzalendo.
 
Nakubaliana na wewe, ukiangalia kiundani hii ni project ya jumba kuu, just kuharibia wagombea walio serious. Hawa jamaa wanadhani hii jnchi ni ya kifalme na hawakubali yaishe. Watanzania wenzangu plaese pleae say No to third Term of Fourth regime. No to uncle. No to project ya Jumba kuu Aka Membe. Princekubali yaishe, tulia Chalinze usije kujiharibia zaidi

Huyo membe tusikubali aingie maana bdo mzee wa chalinze na familia yke wataleta shida.
 
  • Thanks
Reactions: PPM
Hii speech imejaa uongo mtupu,January acha kududanganya kabisa,Yaani Tanzania iwe kama USA kwa miaka Mitano,jamani jamani acha kutudanganya

Kwako msema kweli ni yupi? Kigwangala Membe Wassira Lowasa au Mwigulu? Mimi sio shabiki wa Makamba lkn kiukweli amejieleza vizuri sana huwezi kumlinganisha na watia nia wote waliojitokeza.
 
January atatoa milioni hamsini kwa kila kijiji,jamani Tanzania tuna vijiji vingapi?January atawezesha vyuo viweze kukopesha wanafunzi,Huku akisema kunawili kwa nchi hakutegemei kodi za mapato,bali kunategemea kuwainua watanzania.sasa hizo pesa za kugawa kama pipi atattoa wapi kama hatokusanya kodi ipasavyo?

Tanzania kuna Vijiji Elfu 12. hivyo zitahitajika bilioni mia 6, kukamilisha hilo zoezi,Amesema atazitoa kwa minajili ipi?na kutoka vyanzo vipi vya mapato?kwani haiina mantiki kutoa zaidi ya asilimia 8 ya makusanyo ya TRA kwa mwaka kwenda kwenye vijiji.
Huu ni uongo wa kipuuzi.
 
Ukiona ccm wanalalamikia serikali yao woote nitatizo kibwa.

Wameshindwa kuyafanya kama mawaziri nk sasa wanatuambia nini hawa?

-Wanatetea wezi na mafisadi popote pale

-Wakajiandikia katiba libovu na kula kodi zetu bure.

-Ndo hawahawa wanatakasa majizi ya enzi zile za EPA, KAGODA, Deep Green, Meremeta......IPTL, RICHIMOND, DOWANS,.... ESCROW NK

Hawa akina
Lowasa
Muhongo
Membe
Nyarandu
Mwiguru
Mwandosya
Magufuli
makamba
nk ndo wabunge na mawaziri pia!!! Wanaongea nini wakati Zaid ya 50yrs ya uhuru taifa likielekea mutual? Hawa ni wehu tu. Mara hii hadanganywi mtu.
 
..hawa wana-CCM wanatudanganya tu.

..huyu alikuwa mshauri wa karibu wa Raisi Kikwete.

..tena anadai yeye ndiye aliyekuwa akichukua notes za mikutano yote ya JK na watu mashuhuri kama George Bush, Bill Gates etc. Zaidi alikuwa akiandaa taarifa za ufuatiliaji wa mazungumzo kama hayo.

..sasa kwanini hakumshauri JK atekeleze walau robo ya hayo anayodai atakuja kutufanyia?

..hayo aliyoyasema yanafaa kutamkwa na mgombea ambaye siyo mwana-CCM.

NB:

..wengine wanadai watapambana na rushwa lakini miaka yote wako kwenye uongozi wamekuwa baridiiii huku ufisadi ukiendelea kila kona.

..halafu kupambana na rushwa si ni sawa na kupambana na CCM?

cc Nyani Ngabu

Hapo ndipo wanaponichanga kwa kweli wanaongea as if wao c wanaccm. Wengine ni wajumbe wa CC, ina maana CCM haina democracy kiasi hicho kiasi walikuwa hawapewi nafasi kutoa mawazo yao hayo mazuri japo kdg?
 
Nasikia Speech yake kasumup kitabu chake,itakuwa suala la gesi hakuliongelea kwenye kitabu chake,so ukilaza umemfanya asifanye kutafuta uelewa juu ya gas
 
Tanzania kuna Vijiji Elfu 12. hivyo zitahitajika bilioni mia 6, kukamilisha hilo zoezi,Amesema atazitoa kwa minajili ipi?na kutoka vyanzo vipi vya mapato?kwani haiina mantiki kutoa zaidi ya asilimia 8 ya makusanyo ya TRA kwa mwaka kwenda kwenye vijiji.
Huu ni uongo wa kipuuzi.
Eti atapunguza misamaha ya kodi,jamaa muongo sana
 
waliofanikisha ununuzi wa haya magari ndio watakaoiona Tanzania Mpya kama tulivyoshuhudia kwenye awamu ya nne.
Kwa Mtanzania aliyeshibishwa na ahadi hizi za uongo zilizoanzishwa na wakubwa na sasa bila hata aibu au woga zinatolewa na watoto wadogo na aendelee kuwapa kura ccm. Kwa wale ambao wanajua kuwa kura zao zilichakachuliwa 2010 basi jiandikisheni zaidi na kupiga kura zaidi ili hata wakichakachua washindwe!

 
Nasema through experience kuwa hatotokea rais mpya toka ndani ya chama cha CCM. Si January pekee ambaye ni muongo kwa kutoa kauli mbiu finyu na ahadi kibao kabla ya kupata urais. Kikwete alikuja na kauli mbiu nzuri ambayo watanzania bila kufikiri walimpokea kwa mbinde na kumpamba kila kona ya nchi. Miaka kumi baadaye ndani ya utawala wake, nchi na wananchi wake bado masikini vile vile na ile kauli mbiu yake mashuhuri ya "Ari mpya, nguvu mpya....maisha bora kwa kila Mtanzania," imefikia wapi? Hawa wote waliotangaza nia hawana jipya endapo wako ndani ya CCM na wamekulia humo, kwani hata wakiwa na mawazo mazuri ya kuendeleza nchi kama Kikwete before, hawatafanya chochote cha maana kwa sababu watafuata mfumo uliopo ndani ya chama chao, hivyo kuichagua tena CCM ni sawa na kujipiga kitanzi kwa miaka mingine ijayo ya mateso. Ni takriban miaka 54 sasa chini ya utawala wa TANU/CCM na hakuna cha maana walichokifanya nchi bado ipo majaribioni na viongozi wanaiba tu mali za nchi na kuwachekea waharifu huku wenzetu ambao hawana mali ghafi kama sie wanapiga hatua na kutuacha mbali. To hell with CCM na viongozi wake.

Nakumbuka Mnyika nae alikuja na ahadi tamu Ubungo za kuwa akichaguliwa tu basi tatizo la maji linaingia kwenye historia.Leo yapo wapi??


Sugu yeye aliwaahidi Mbeya kuwa japo kuwa kwa kutumia ideas zake kama ilivyokuwa malaria no more ataanzisha miradi ya mabwawa ya kufuga samaki Mbeya ili vijana wengi wajiajiri kwa kufuga samaki.

Na akaongeza kuwa akichaguliwa tu basi kila mwanafunzi wa sekondary Mbeya atapata laptop.Ni uzembe tu wa mbunge aliyekuwepo kushindwa kuja na idea za maana.

Leo miaka 5 baadae ata kiyakumbushia hawakumbushi.

Hivyo kama unaona hawa wa CCM wanaongea ndoto tatizo sio la CCM, tatizo ni watanzania, ata hao wa Upinzani wanaongea ndoto hizihizi kama hawa
 
Nasikia Speech yake kasumup kitabu chake,itakuwa suala la gesi hakuliongelea kwenye kitabu chake,so ukilaza umemfanya asifanye kutafuta uelewa juu ya gas

Victorie heshima kitu muhimu sana, ukimuita January kilaza basi akina Mbowe utawaitaje?kuna wabunge wachache sana walio kichwa kama Makamba.

Na tofauti na Makamba na wengi ata waliosoma ni kuwa wao hawasomi tena wakati Makamba anasoma kila siku.

Makamba ni kichwa, hayo ya utekelezaji ni suaka lingine lakin kwenye nadharia ukitaka idea kamuone Makamba.Huwezi kuona tofauti ya ufahamu wa Makamba ata na wanasiasa wa nchi zilizoendelea, yupo kamili na yupo updated na elimu, falsafa, ideas mbalimbali za siasa na utawala duniani.
 
Basi sawa, Makamba anajua kutiririka.
Je ataweza kuzitekeleza ahadi kwa vitendo?
Je ataweza kwenda kinyume na ilani ya CCM?
Wasifu wake kuhusu kutekeleza ahadi kwa vitendo bado haujadhihirika.
 
Wakati mwingine watu wakubali tu January leo kaja kivingine kabisa ukilinganisha na porojo za wengi wa awali this is what politics is all about maelezo na mbinu zake kinaga ubaga.

Issue labda je mbinu zenyewe ni sahihi au zinatekelezeka given the resources: lakini overall ameweka new bars in terms of the politics of policies. Aina maana mbinu zake zote are convincing to every one; over all big up January.

Nilichoona kwa Januari ni kitu cha kawaida kwa mtu yoyote ambaye ana simple exposure ya kuishi na kufuatilia siaza za dunia ya kwanza, Hakuna kipya sema kwa kibongobongo, unaweza sema watu hawajawahi ona at personal level.

Is this a bad thing?NO. It actually confirm the fact that, when keeping all factors constant, Tanzania needs to have a president who is below 45 years old and with good enough exposure and forward looking ideas.

Is January a capable person with what it takes to lead Tanzania? I still do not think so. I have always had a feeling he gets way too much help, and every time he is given an opportunity to stand by himself, he fails. The cyber-crime bill, the media bill, were supposed to be his cornerstone,his time o prove us doubters wrong. We all know how horrible that one went.

Hawa wako bize kumlaumu JK,lakini ndio walikuwa bize kumuangusha. Sasa kimtu kinakuja kutuambia kitamaliza tatizo la foleni kwa kujenga flyovers wakati kinajua kabisa hizi flyovers zimeshasainiwa kujengwa.Na pesa JICA wameshatoa. wanatueleza kuwa tatizo la ardhi litatatuliwa kwa kuwatoza kodi speculators wakati amekuwa ikulu miaka ya kutosha, JK alikuwa hamuoni?akiwa kama waziri, alishindwa nini kumshawishi waziri wa ardhi?na alikuwa na access na cabinet yote?inamaana hana ushawishi juu ya watu wasiozidi 50 tu?ataweza vipi kuwashawishi mamilioni ku-embrace policy zake?akiwa bado mbunge,alishindwa nini kuwasilisha bill yake kama makamba?haoni mwenzie Zitto anachofanya?

I will pick someone like Zitto over January Makamba any day, kwa sababu Zitto hapewi msaada, anasimama mwenyewe, and 90% of the time he walks the talk.
 
Back
Top Bottom