Kutoka Unguja: Simba S.C 5-2 Kimbunga F.C

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Leo Mnyama katakata ipasavyo kisiwani Unguja, katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya timu bora kabisa kwa sasa kisiwani Unguja.. Kimbunga F.C.

Hii ni baada ya kuondoka na ushindi mnono wa goli 5-2.. Ushindi huu uliandamana na Kimbunga cha pasi rula.. Kimbunga cha ufundi mwingi.. Kimbunga cha soka maridadi sana.. Kimbunga cha ushindi mnono.. n.k

Waliotupia kambani leo ni Ajibu [goli 2].. Danny Lyanga 1, Mgosi 1.. na la mwisho kafunga Pro, ambaye yupo katika majaribio.

Jumapili ya wiki hii Mnyama huyu huyu ambae hana masikhara kabisa kwa sasa.. atakua dimbani tena kupambana na Kombaini ya Unguja.

NOTE: Narudia tena.. 12.12.2015 Azam F.C mtatusamehe tu.. lazima tushinde, maana hakuna namna.
 
Zanzibar INA kiwango cha soka kuijenga timu imara kweli? Let's be logical comrades
 
naona simba mko vizuri sembo
 
Last edited by a moderator:
Zanzibar INA kiwango cha soka kuijenga timu imara kweli? Let's be logical comrades

Mkuu labda nikuume sikio tu.. Katika dunia hii ya sasa baada ya mazoezi mazito ya ndani na nje ya uwanja.. Timu hucheza mechi ya kirafiki na timu iliyo na kiwango cha chini zaidi yao ili kujua kama darasa limekolea.
Hivyo Mnyama kucheza mechi za majaribio Zenji si ajabu.
 
GENTA yuko wapi kusherekea ushindi huu wa wanasimba huko zenji
 
Mkuu sina data kamili.. Nikizipata nitazishusha hapa.

Yap.. Mkuu Mnyama sasa yupo vizuri.

Mnyama aka Mchangani FC ni mzuri sana kwa mechi za mchangani za majaribio! Majanga huanza pale mechi za ligi kuu zinapochezwa na hasa raundi ya pili.
 
Mnyama aka Mchangani FC ni mzuri sana kwa mechi za mchangani za majaribio! Majanga huanza pale mechi za ligi kuu zinapochezwa na hasa raundi ya pili.

Mkuu hiyo ilikua ni zamani.. Sasa hivi tupo imara zaidi.
 
Lyanga anaweza kuwa msaada mkubwa pale mbele ana kila kitu cha kuitwa mshambuliaji
 
Simba tufungieni Azam ...sisi (Yanga) ninyi ni ndugu zetu. .msituangushe kwa hilo tupo nyuma yenu
 
Simba tufungieni Azam ...sisi (Yanga) ninyi ni ndugu zetu. .msituangushe kwa hilo tupo nyuma yenu

Sijawahi kuona dua mbovu ya mwanayanga kama hii we badala uombee drow unaomba Azam apigwe, au hapo kitaani kwako hakuna mihemko ya simba? Right kama Ingekua ndio mechi ya mwisho sawa, ila kwa sasa sare ndio mpango Mzima.
 
Simba sio saiz yetu...mi nahofia Azam tu kwenye ligi
 
Inakuwaje mabeki visiki wanaruhusu goli 2 na timu ya mchangani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…