Kutoka uwanja wa Taifa: Mechi ya Tanzania vs Nigeria leo tarehe 05/09/2015

chagga land

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2015
Posts
394
Reaction score
95
Leo ndio ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka duniani kote kuja kushuhudia manguli wa soka duniani kutoka Tanzania wakiongozwa na kocha wa makocha Charles Boniface Mkwasa master wakichuana na kikosi cha Nigeria kikiongozwa na kocha aliyezoea kufungwa Sande Olise.

Mtanange huu utavurumishwa kutoka dimba la Taifa na huku mchezo ukitarajiwa kuanza majira ya saa kumi na nusu jioni kwa majira ya Afrika Mashariki. Kama kusipokuwa na figisufigisu mechi itarushwa na AZAM TV na mimi pamoja na timu yangu tutakuletea moja kwa moja kutoka taifa kupitia tovuti inayoongoza Afrika mashariki na kati kwa kuwa na followers wengi, JamiiForums.

Stay online
=======

Full Time

Tanzania 0 - Nigeria 0

Last edited by a moderator:
dah! nimeota eti tumepigwa 2-1,sijui nikwel mungu aepushe mbali,,,,,stars tupen raha ya ushindi leo
 
I love Tanzania, mungu ibariki tz
 
Taifa stars 0 Nigeria 26. Super eagles piga hao mapimbi wakacheze kidali poo na Malinzi
 
Kila la heri Taifa Stars, fumua hao Boko haraka sana
 
Taifa stars 0 Nigeria 26. Super eagles piga hao mapimbi wakacheze kidali poo na Malinzi
Mmmmh! hivi mwenzetu ni mtanzania kweli wewe???
Kila la kheir Taifa stars, piga hao tai wa Nigeria goli 3 tu zinatosha.
 
Mmmmh! hivi mwenzetu ni mtanzania kweli wewe???
Kila la kheir Taifa stars, piga hao tai wa Nigeria goli 3 tu zinatosha.

Hapa ndipo wa tz huwa tunadanganyana, hivi kweli tz tumfunge Nigeria eti kwakuwa tu tumempa kocha mzalendo timu?!!!! tunachekesha kweli. tuwe wakweli tu hatuna uwezo huo kwa sasa.
 
Mmmmh! hivi mwenzetu ni mtanzania kweli wewe???
Kila la kheir Taifa stars, piga hao tai wa Nigeria goli 3 tu zinatosha.

Mi ni mtanzania halisi. Ila sipendi mwenendo wa hawa wanaosimamia soka letu. Kwa miaka nenda rudi hakuna chochote cha maana wanachofanya katika kukuza soka zaidi ya kutuletea magonjwa ya moyo.

Taifa stars kila siku ni kichwa cha mwendawazimu na kwakuwa ni timu yetu tunaipa moyo na kuishabikia kama vile sisi ni mabingwa. Hao wezi waliokuwa madarakani baada ya kuchukulia kutokata tamaa kwetu sisi mashabiki kama changamoto wao wanatuona mabwege na wanazidi kuendekeza ufisadi huku soka letu likiporomoka.

Nasema tena wapigwe tuuu kudadadeki hata goli elfu kumi.

FULL TIME : Kichwa cha mwendawazimu 0 - Nigeria 26
 
Leo live update mtapata hapa hatua kwa hatua jinsi timu ya kimataifa Nigeria watakavyoichabanga Li kichwa cha mwendawazimu muokota makopo a.k.a Taifa Stars magoli ya shetani.
 
Hapa ndipo wa tz huwa tunadanganyana, hivi kweli tz tumfunge Nigeria eti kwakuwa tu tumempa kocha mzalendo timu?!!!! tunachekesha kweli. tuwe wakweli tu hatuna uwezo huo kwa sasa.
Uwezo tunao wa kuwakung'uta Tai wa Nigeria tena hata goli 4 ila ninachokiona wachezaji wetu hawajitumi..
Mbona Morocco alikula za kutosha tu!
 
Naipenda Nchi yangu Lakin hatuna ubavu wa kuifunga Wanaija hao... kila la kheri T-stars ye2!
 
Unajua watu wengi awaamin.mabadiliko kisa sisiemu wako wengi ama wamekata mda uongozi bila kujua.ndan ya ccm kuna mioyo ya ukawa

leo narudi kwanduguzetu wa taifastars kwel mnapendwa mnapendeka lakini mioyoni mashabiki wanajua wazi kipigo akikwepeki tumebana sana 3-2. Else tunachezea @@@@4-2@@@!@
 
No East african nation has ever defeated Nigeria in football lol
 
No East african nation has ever defeated Nigeria in football lol
Historia peleka vyuoni, uwanjani ubabe wa timu huonekana baada ya dakika 90.
Taifa Stars 3-1 Nigeria
 
Tupigwe turudi kwenye ligi yetu ya magumashi.
Tanzania 0
Nigeria 7
 
Hapa ndipo wa tz huwa tunadanganyana, hivi kweli tz tumfunge Nigeria eti kwakuwa tu tumempa kocha mzalendo timu?!!!! tunachekesha kweli. tuwe wakweli tu hatuna uwezo huo kwa sasa.

cyber law inatakiwa ikutafune maana huna hata robo chembe ya uzalendo ya timu yako
 
Mechi itarushwa na Super Sport
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…