Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Salaam Tanzania na kooote ulimwenguni, Karibu sana....! Naaaaam...!
Ile patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL, inaendelea kuvurumishwa leo Jumatano Oktoba 23, 2019 majira ya saa 11:00 jioni, kunako uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni wanawakaribisha wana Lamba lamba Azam FC.
Mchezo wa leo unatakuwa na ushindani mkali sana, hasa ukizingatia kwamba Simba SC ambao wenye ubora wa viwango uwanjani, wakiwa na utamaduni wa kuandikisha ushindi kwa asilimia 100% huku wakiwa wameshinda michezo yote, wanakutana na Azam FC ambayo nayo haijapoteza mchezo wowote kwenye VPL, lakini ina kumbukumbu ya kuchapwa na Simba SC katika Ngao ya Jamii msimu huu wa 2018/2019.
Wapenda kandanda, mnaombwa kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa tayari kushuhudia mtanange huo, ambao unatarajiwa kuwa mkali na wakusisimua kwa muda wote..!
Nani kuibuka na Ushinda, Simba SC ama Azam FC?
•••••=================•••••••••
MATOKEO YA VPL;
Simba SC imeibuka na ushindi wa bao moja kwa bila, kwa kuichapa Azam FC, kwenye uwanja wa Taifa, bao safi la kichwa likiwekwa kimiani na Meddie Kagere baada ya majalo bomba ya Kahata kunako dakika ya 49' ya mchezo huu wa VPL
Kwa matokeo hayo Simba SC wanaendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa VPL wakiwa na alama 15 kwa kucheza michezo 5.
FT: Simba SC 1-0 Azam FC..Hongera Simba SC NguvuMoja.