Niko hapa uwanjani naangalia mpira wa Simba SC dhidi ya Mashujaa FC. Kitu kilichonifurahisha na kunivutia ni kuona gari la Zimamoto lipo 'active' hapa uwanjani, vimulimuli vinawaka na makamanda wapo standby kabisa kwa dharura yoyote. Hongereni sana Zimamoto kwa utayari huu! 👏👏
Hata hivyo, nitumie nafasi hii kutoa ushauri wangu wa kizalendo. Utaratibu huu mzuri wa magari yetu ya zimamoto kuwa standby na kuwasha vimulimuli usiishie tu kwenye viwanja vya mipira au maeneo makubwa ya katikati ya jiji. Kuna haja kubwa ya utaratibu huu kusogezwa hadi mitaani kwetu huku uswahilini ili kupunguza muda wa kufika eneo la tukio (response time) majanga yanapotokea.
Zamani tulikuwa tunaona changamoto ya magari kufika mitaani yakiwa hayana maji (ingawa kiukweli hivi karibuni sijaona kabisa changamoto hiyo, napongeza maboresho yanayofanyika). Lakini hapa najaribu tu kukumbushia kuwa tukiongeza nguvu mitaani, tutakuwa salama zaidi.
Tuzidi kushirikiana kulinda jamii yetu. Ukiona dharura yoyote ya moto, namba ni 114.
Wacha tuendelee kumenyana uwanjani! ⚽🔥