Kutoka X ukurasa Wa Roma Kuhusu Waziri Katambi.

The Bleiz

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2012
Posts
5,143
Reaction score
13,836
Wizara ya mambo ya ndichi ina~deal na petty issues….badala ya ku~deal na vitu serious.

Waziri una deal na mashalove & Pipitilda
badala ya kulinda mipakani huko zinaingia pombe feki daily zinaenda kuua figo za maelfu ya mahomeboys na dada zetu, ajira zenyewe hamuwapi vijana wanashindwa kumudu dialysis gharama wanapoteza maisha!

Halafu hapo utasema wizara inalinda raia na mali zake!!?🤷‍♂️

Unazungumzia maadili ya kuongea lugha chafu mitandaoni, USA 🇺🇸 Rais Trump anatukanwa na raia ile F****word tena public kabisa kwenye press na raia haguswi na ndio nchi ina mahospital bora,shule na vyuo bora, umeme & maji havikatiki,barabara safi, na ajira za kutosha!!

Wewe maadili yamekusaidia nini mtu nina bachelor ya Architecture GPA 3.5 na naendesha boda tena ya mkataba mwaka wa nne huu kazi hamna, kwa siku naingiza elfu saba, utasema kuna maisha hapo?

Wewe unaekazania maadili una population ya watu milioni 70, unatangaza ajira elfu 45!!
Sasa kuna taifa hapo?

Simaanishi kama taifa tusiwe na maadili au utamaduni, lakini ni petty issues….. kundi la wale mates wangu walipaswa kuitwa hata basata tu wakamalizana nao chaap kwa, kama wazazi/walezi……easy tu, lakini sio waziri wa wizara!!

Kama tunataka kukemea maadili, tukemee maadili ya utekaji na ufisadi na mauaji ya ndugu zetu, hayo ndio maadili ya msingi na uwaite wahusika uwakemee live tuone kama tulivyoona kwa wale wasanii!!

Unaacha kuwaita askari walioua ndugu zetu october 29 uwakemee na kuwawajibisha, unamuita yule sista du anayeuza jeans, unamuita Nicole….kisa anaonyesha kifua!!?

Nini kifua babu, nchi za wenzetu unakuta striper anacheza uchi kabisa usiku club na mchana ni daktari / nurse anatibu watu na ndio ajira yake na analipa kodi na hela anayotengeneza humgusi….na ana degree kasoma na husikii kaitwa na waziri wala Mkuu wa mkoa! Dunia ndio ipo huko!!

CAG kila mwaka anasoma report wizi wa Billions of bags 💰 na huoni mtu akiwajibishwa…..sasa hayo ndio maadili ya kukemea public tena, sio mtuambie tunamalizana kwenye vikao vya kamati sijui za halmashauri…NO!!

Watu wanatekwa kiholela, wanapotea wanakufa….kila kiongozi anayehojiwa anakataa kuwa hakuna utekaji….husikii hata mmoja akikemea…..then leo wizara ya mambo ya ndani head liner unakaa kikao na GiGi money, Anko T unawakemea na mnalazimisha kabisa iwe news kubwa!!

Yani hukemei mtu anaua watu, unakuja unamkemea gigi kavaa mpasuo!?

Hivi tuna taifa kweli hapa jamani!?

Hii nchi ina maigizo sana

Soma Malu, pipytida, Dudu baya, Gigy money, Anko T, Noel na Mwijaku waitwa central station


​
 
Sijawahi kuona taifa la hovyo kama Tx
 
Roma, wabongo hawawezi kukuelewa, wao wanachotaka ni serikali ipinge Ushoga, hilo la utekaji. Mauaji, miundombinu bora, ajira, Etc, hayo sio mambo yao.

Wabongo tatizo kuu ni USHOGA, hayo mengine walaaaaa, usijipe tabu brooh, wee kula maisha huko Duniani.

Nb: Wenye Duku Duku pandeni muwezavyooo 😂😂😂😂
 
Kusudi haiambiwi pole kushindwa kwako kumudu gharama za dialysis tatizl zilotokana na pombe hili pia la kumlaumu katambi?

Tujitafakari aisee
 
Kusudi haiambiwi pole kushindwa kwako kumudu gharama za dialysis tatizl zilotokana na pombe hili pia la kumlaumu katambi?

Tujitafakari aisee
Ndugu mdau, naona umekimbilia kutoa shutuma binafsi kuhusu changamoto za kitabibu kama ugonjwa wa figo (dialysis) na matumizi ya pombe, ukihusisha maisha binafsi ya msanii Dudu Baya na hoja iliyopo mezani. Hata hivyo, kiuhalisia umechanganya mada kabisa na unamlaumu mtoa mada pasipo sababu ya msingi.
Kukusaidia kuelewa muktadha halisi wa kitaalamu na kisheria unaojadiliwa hapa:
  • Muktadha wa Habari: Hoja hapa inahusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri Patrobas Katambi kuagiza Jeshi la Polisi kumkamata msanii Dudu Baya kwa sababu ya kukataa wito wa kwenda wizarani. Dudu Baya aligoma kuhudhuria akidai hawezi kukaa meza moja na watu wanaojihusisha na masuala ya ushoga.
  • Kiini cha Hoja: Mtoa mada hapingi uwepo wa maadili, bali anahoji vipaumbele na matumizi ya rasilimali za wizara (Prioritization of National Security Assets). Wizara yenye dhamana kubwa ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao inapoweka nguvu kubwa, vikao vya dharura, na "headlines" za kitaifa kwenye migogoro ya wasanii, inazua maswali mengi ya kimsingi.
Kutazama mambo kwa jicho la kiprofeshonali, taifa linakabiliwa na changamoto kubwa za kimfumo zinazopaswa kuwa vipaumbele vya kwanza vya Wizara ya Mambo ya Ndani na serikali kwa ujumla:
  1. Ulinzi na Usalama wa Raia: Masuala ya utekaji wa raia, kupotea kwa watu, na matukio ya uvunjifu wa amani ndiyo yanayopaswa kupewa kipaumbele cha kwanza na dharura ya kiwizarani, badala ya mipasuo ya nguo au malumbano ya wasanii.
  2. Ripoti za CAG na Ufisadi: Upotevu wa mabilioni ya fedha za umma unaoripotiwa kila mwaka unapaswa kuambatana na uwajibishwaji wa dhati na wa wazi unaoonekana kwa wananchi wote, kama inavyofanyika kwa wasanii.
  3. Usimamizi wa Mipaka na Afya: Kulinda mipaka dhidi ya bidhaa hatari na feki (kama pombe feki) ambazo ndizo zinazosababisha magonjwa makubwa ikiwemo kufeli kwa figo (ambako wananchi wanashindwa kumudu gharama za dialysis), ni jukumu la msingi la kiulinzi na kiudhibiti.
  4. Kilio cha Ajira kwa Vijana Wasomi: Taifa lenye idadi kubwa ya watu lakini linatangaza nafasi chache za ajira, linazalisha changamoto kubwa ya kiuchumi. Haileti tija kiutendaji kuona kijana mwenye elimu ya juu (kama Bachelor of Architecture mwenye GPA kubwa ya 3.5) akilazimika kuendesha bodaboda kwa mkataba wa kuingiza elfu saba kwa siku, huku viongozi wakielekeza nguvu zote kwenye "maadili ya mitandaoni" badala ya maadili ya kiuchumi na maendeleo.
Nchi zilizoendelea kama Marekani zinaruhusu ukosoaji mkubwa wa viongozi, lakini zinaweka mifumo imara ya elimu, afya bora, barabara, na nishati ya uhakika. Kama wadau wa maendeleo, tunapaswa kuhoji na kushauri serikali yetu ijikite kwenye kutatua matatizo makubwa ya kimfumo yanayogusa maisha ya wananchi kila siku, kulinda rasilimali za umma, na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wetu wasomi, badala ya kushabikia maigizo ya mitandaoni.


Soma habari kwa makini na upime vipaumbele vya taifa letu kabla ya kutoa majibu mepesi kwenye hoja nzito.


 
Kielewe nilichokiandika
 
Kielewe nilichokiandika
Nieleweshe maana hakieleweki kwa mtu mwenye akili timamu. Hiyo habari uliyoiandika haipo kwenye mada wewe umeitoa wapi ama unatafuta kila njia kuwatetea hawa watu? naomba copy kipande ambacho kina sema ulichokiandika na u paste hapa labda mimi sijaisoma vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…