Kutoka X ukurasa Wa Roma Kuhusu Waziri Katambi.

Kutoka X ukurasa Wa Roma Kuhusu Waziri Katambi.

1787913637671.jpg
 
Wizara ya mambo ya ndichi ina~deal na petty issues….badala ya ku~deal na vitu serious.

Waziri una deal na mashalove & Pipitilda
badala ya kulinda mipakani huko zinaingia pombe feki daily zinaenda kuua figo za maelfu ya mahomeboys na dada zetu, ajira zenyewe hamuwapi vijana wanashindwa kumudu dialysis gharama wanapoteza maisha!

Halafu hapo utasema wizara inalinda raia na mali zake!!?🤷‍♂️

Unazungumzia maadili ya kuongea lugha chafu mitandaoni, USA 🇺🇸 Rais Trump anatukanwa na raia ile F****word tena public kabisa kwenye press na raia haguswi na ndio nchi ina mahospital bora,shule na vyuo bora, umeme & maji havikatiki,barabara safi, na ajira za kutosha!!

Wewe maadili yamekusaidia nini mtu nina bachelor ya Architecture GPA 3.5 na naendesha boda tena ya mkataba mwaka wa nne huu kazi hamna, kwa siku naingiza elfu saba, utasema kuna maisha hapo?

Wewe unaekazania maadili una population ya watu milioni 70, unatangaza ajira elfu 45!!
Sasa kuna taifa hapo?

Simaanishi kama taifa tusiwe na maadili au utamaduni, lakini ni petty issues….. kundi la wale mates wangu walipaswa kuitwa hata basata tu wakamalizana nao chaap kwa, kama wazazi/walezi……easy tu, lakini sio waziri wa wizara!!

Kama tunataka kukemea maadili, tukemee maadili ya utekaji na ufisadi na mauaji ya ndugu zetu, hayo ndio maadili ya msingi na uwaite wahusika uwakemee live tuone kama tulivyoona kwa wale wasanii!!

Unaacha kuwaita askari walioua ndugu zetu october 29 uwakemee na kuwawajibisha, unamuita yule sista du anayeuza jeans, unamuita Nicole….kisa anaonyesha kifua!!?

Nini kifua babu, nchi za wenzetu unakuta striper anacheza uchi kabisa usiku club na mchana ni daktari / nurse anatibu watu na ndio ajira yake na analipa kodi na hela anayotengeneza humgusi….na ana degree kasoma na husikii kaitwa na waziri wala Mkuu wa mkoa! Dunia ndio ipo huko!!

CAG kila mwaka anasoma report wizi wa Billions of bags 💰 na huoni mtu akiwajibishwa…..sasa hayo ndio maadili ya kukemea public tena, sio mtuambie tunamalizana kwenye vikao vya kamati sijui za halmashauri…NO!!

Watu wanatekwa kiholela, wanapotea wanakufa….kila kiongozi anayehojiwa anakataa kuwa hakuna utekaji….husikii hata mmoja akikemea…..then leo wizara ya mambo ya ndani head liner unakaa kikao na GiGi money, Anko T unawakemea na mnalazimisha kabisa iwe news kubwa!!

Yani hukemei mtu anaua watu, unakuja unamkemea gigi kavaa mpasuo!?

Hivi tuna taifa kweli hapa jamani!?

Hii nchi ina maigizo sana

Soma Malu, pipytida, Dudu baya, Gigy money, Anko T, Noel na Mwijaku waitwa central station


Waziri ni CHAWA asiye na akili wala utu
 
Mwaka Jana nilikuwa Indiana USA yule senator wao anaitwa Todd Young nadhani alikuwa anatukanwa live na democrats aiseee nikajiuliza hawa wangekuwa bongo Leo wote wangekuwa wameshapotea Sasa senator wa USA na karais ka afrika nani mwenye nguvu duniani?
 
Mtu aje anieleze vizuri kosa la Uncle T, juma lokole na Noel tafadhali

Hao hawakutakiwa kuitwa, umma Ulishinikiza hadi wakaitwa sasa unajiuliza hao ni wasanii was nini?
Wabongo wanachekesha sio poa 😂😂😂
 
Kwani tulishamalizana na hawa maadui watatu wa taifa la Tanzania Ujinga, Maradhi na Umaskini?
Sasa kama wanaotuongoza ni wajinga vilevile! Ujinga utaondokaje?
 
Kusudi haiambiwi pole kushindwa kwako kumudu gharama za dialysis tatizl zilotokana na pombe hili pia la kumlaumu katambi?

Tujitafakari aisee
Sasa mbona serikali inawashika wauza gongo?
 
Si kwamba hatuna viongozi wenye uwezo ,na katambi c kwamba hajui vipaumbele, nafasi za kuteuliwa mara nyingi ukishaapa. 1.unamsoma aliekuteua ,ukishamsoma ni mtu wa aina gan na ana taka Nini unaecheza mlemle
Ukienda kinyume hakuna anaekupigia cm zaid
Asbh ukiamka kig'ora hakuna nan yupo tayar kuwa mbuzi wa sikukuu .Kila mmoja analinda kibarua chake
 
Roma, wabongo hawawezi kukuelewa, wao wanachotaka ni serikali ipinge Ushoga, hilo la utekaji. Mauaji, miundombinu bora, ajira, Etc, hayo sio mambo yao.

Wabongo tatizo kuu ni USHOGA, hayo mengine walaaaaa, usijipe tabu brooh, wee kula maisha huko Duniani.

Nb: Wenye Duku Duku pandeni muwezavyooo 😂😂😂😂
Lakini tuwe wakweli, ushoga sio mzuri. Ukitaka kuamini ushoga sio mzuri ngoja mtoto wako au ndugu yako awe shoga. Utatamani ulie, utatamani ucheke, utatamani ujifukie chini ardhini, utatamani uruke juu kama ndege kwa kifupi utakuwa chizi.

Wazungu kuridhia ushoga ni kwasababu ya kumkataa mwenyezi Mungu (atheism and paganism) angalia warumi 1:18-28

Na pia pesa au maendeleo sio kila kitu angalia 1 Timotheo 6:10. Mungu ndio kila kitu, ndio maana rais John Magufuli alisema tumtangulize Mungu mbele. Hata wanafunzi wa hii shule ninayofundisha pale ubaoni wanapenda kuandika GOD FIRST.

Sasa haina maana kwa kuwa comment zangu nyingine zinamkosoa rais Magufuli kwenye masuala ya demokrasia. Basi ninamkosoa kwenye kila kitu.

Note: Demokrasia ni nzuri sana kwenye taifa la wakristu na waislamu wacha Mungu waliofanikiwa kuishi kwa amani.

Haina maana taifa la wacha Mungu halitakuwa na maasi yatakuepo hata ******* na wafiraji watakuepo (kwa uchache japo) lakini kunakuwa na sheria za kuzibiti hayo mambo siyo kuyabariki
 
Mshamba tu huyu Minister, sijui katoka kijiji gani na kiswahili chake cha kwenye Kamusi.
 
Back
Top Bottom