Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Watu wa Soka,
Leo Singida Big Stars tumeshiriki kongamano la mpira wa miguu maarufu kwa jina la Tanzania Football Summit 2022 linaloendelea hapa visiwani Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine muhimu, tumefanya mazungumzo na kocha mstaafu wa klabu ya Chelsea Avram Grant, mchezaji wa zamani wa Senegal Khalilou Fadiga na wadau wengine mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali waliofika katika kongamano hilo litakalohitimishwa kesho Juni 26, 2022.
Mazungumzo yetu yalilenga kujenga na kuimarisha mahusiano pamoja na kubadilishana uzoefu wakati huu ambao tunaendelea na maandalizi ya Ligi Kuu ya NBC msimu ujao wa 2022/2023.