Kutokana na changamoto za kibiashara mkoani Geita nafikiria kuhama mkoa, naomba mnishauri

Kutokana na changamoto za kibiashara mkoani Geita nafikiria kuhama mkoa, naomba mnishauri

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2021
Posts
338
Reaction score
683
Wakuu habarini za leo!?

Lengo kuu la Uzi huu ni kutaka mawazo mbadala ama ushauli kutoka kwenu. Mimi mkazi wa Geita mjini mwenye miaka 24, sjaoa na Wala Sina mtoto. Naweza kusema kwasasa mm ni mzawa wa geita mjini japo kua skuzaliwa hapa ila nimeishi tangu mwaka 2002 mpaka leo.

Mwaka 2018 mwezi wa 11 nilifungua biashara ya mpesa kwa mtaji wa laki 8 baada ya kua nimelipia kila kitu. Baadae nikaongeza huduma za mitandao yote mpaka Sasa.

Changamoto.

-Mwaka 2019 Mwezi wa 3 nilitapeliwa laki 3,
-mwaka 2020 mwaka haukua mzuri kwangu ki biashara.
Mwezi wa 4 mwizi alitoboa "singboard" kwakua flame yangu kwa nyuma ni guest aliingia kulala kama mteja akapanda juu ya uwaz ulio kua chooni na kukwea chuu ya dari la nyuma tukaibiwa flame zote.

Mimi niliibiwa hela cash 1.5 milion + sim viswaswadu nilivo kua naviuza 15 pic.

- Mwezi wa kumi niliamua kuboresha ofisi nikasuka grill kwa juu na nje, kuna siku alikuja mdogo wangu nikamuacha kama dk 20 akaja jamaa kununua sm kumbe alikua tapeli akapigwa sm kubwa infinix smart 5 kwa wakati huo nilipoteza 200k

- Baada ya wiki mbili mbele nikiwa nimefunga kikufuri changu nimeenda kununua vocha upande wa pili mida ya saa 10 jion akaja kibaka akiwa na master key, akafungua kakomeo na kupora simu kubwa smart phones 5 na cash laki 9 = 2.4 milion ya kilicho porwa, ila mungu mwema jirani yangu alimuona mwizi na kupambana nae, nilipo Rudi ofisini nikapigiwa sm mpaka mwizi alipo nikaokoa kila kitu kilicho kua kimeporwa.

- Baada ya wiki mbili nikatuma pesa ki makosa laki 6 na mteja alikua anadaiwa songesha 1000 ilipo katwa nikawa Sina uwezo wa kurejesha muhamala huo hata nilipo piga sm Vodacom sikusaidiwa kwaio nikawa nimepoteza laki 6.

- Biashara ya mazoea ya urafiki. Hii hitokana na baadhi ya marafiki wakikwama hunitimbia nilipo na kuja kunieleza shida zao nakosa namna naamua kuoa Kidogo nawapa.

-Zingine nakumbuka ni changamoto binafsi sio za ofisi, ni zile za matumizi muhimu.

Mafanikio:

Kwa mpesa zamani camisheni ilikua ina Soma 400k kwa voda
Tigo. 60k

Ila kwa Sasa biashara imekua ngumu Sana hivyo naishia kupata 300k

Nilibahatika kukuza mtaji mpaka milion 4.8 mpaka kufikia mwaka 2020 mwezi wa 9. Nikafanya maboresho ya ofisi Kidogo nikaanza kuuza sm kubwa ila kwa ma ingira niliyopo biashara haiwend kabisa. Sm ndogo nauza 1 pic au 2 pic kwa wiki nzima na faida yangu ni 3000 kwa kila pic ya sm. Kwaio nimesitisha biashara ya sm, nimebakiza mpesa.

Location ya biashara.

Nipo geita mjini mtaa wa shilabela. Huu mtaa kwa juu kama 1 km kuna poli lenye vichaka ambapo ni chimbo la wavuta bangi karibu wote wa hapa mtaani na mitaa jirani.

Baada ya kuvuta huja kujichanganya mtaani hivyo mtaa wangu una vibaka wengi sana.

Kwa kua Geita haija kaa ki biashara sion mtaa mwingine wa kwenda kufanya biashara, isipokua mtaa wa nyankumbu umechangamka lakin ni nyumbani kwa baba na mama hivyo sihitaji kufanyia huko biashara maana nilijaribu nikaferi.

Maoni yangu:

Ninawaza kuhama mkoa niingie kwenye mikoa ya kibiashara.

Haya mdau nambie ungekua ni wewe ungefanyaje ?
 
Mkuu pole sana, nakushauri pambana hapo hapo, mzee wangu amepata maisha kwa kufanya biashara kwenye mazingira yenye vikwazo vya wizi kama ulipo wewe, kikubwa ongeza umakini sana ujue mbinu za matapeli.

Pia umesema Nyakumbu ni kuzuri kwa maana ya usalama na vp kuhusu biashara je kuna mzunguko kama huo wa shilabela?
 
Nashukuru Sana mkuu.

Nyankumbu mzunguko upo unaweza ukawa sawa na hapa au zaidi kwakua nyankumbu ni njia panda.

Ila shida ya Nyankumbu kwa biashara ya huduma za kifedha vibanda vimekua vingi hivyo ni ngumu kupata kamisheni kubwa kwa kua wateja mnawagawana saana, vinvinevyo mpaka uwe na mtaji wa kutosha kufungua na hiduma za kibenk at least hapo utapata kikubwa Kidogo.
 
Kwa mtaji wako jaribu Dodoma maeneo ya chidachi,changombe,ndachi.
Sawa kaka nashukuru, mwezi wa 4 nilipita Dodoma nikawa naangalia fursa za biashara ambazo naweza kifanya hapo.

Ninawaza niende kwenye miji ambayo kuna vyuo Sana, kama Dodoma moro na Dar huko naambiwa mzunguko ni mkubwa kuliko huku nilipo
 
[emoji257][emoji67]‍🦽[emoji67]‍🦽[emoji67]‍🦽 pole mkuu ila kila kitu nikua na Mungu ndani yake
 
[emoji257][emoji67]‍🦽[emoji67]‍🦽[emoji67]‍🦽 pole mkuu ila kila kitu nikua na Mungu ndani yake
Hakika mkuu. Japo kua nilikua nawaza nihame mji,

Maana geita watu wake wanategemea waajiliwa kufanya mizunguko wa kifedha hivyo tarehe kama hizi za kati kati ya mwezi zinakua ngumu afu hapa inaskia mwingine anafanya biashara kwingine na anapiga pesa ya kutosha tu. Kidogo inanifanya kuwaza hivyo
 
Mkuu mm nipo Sengerema nina mtaji wa 1.5 M natafuta site ya kuanzisha mpesa kutokana na mtaji wangu siku ukitaka kuachia site hapo Geita nambie nije uniuzie...
 
Pole na changamoto za maisha na kibiashara

Unacho paswa kufanya ni kuendelea kuboresha ofisi swala LA kuuza simu moja ni LA kawaida kabisa unahitaji uongezee baadhi ya vifaa ikiwepo vya umeme

Hivyo utaweza kuiona faida lakini kwa hii biashara ya miamala kwamba itakupa uhakika wa kutoboa kwenye maisha hapana
 
Ni PM nikupe machimbo ya biashara mdogo wangu tena kwa muda mfupi unarudi ulikotoka.
 
We jamaa haupo makini ndio maana wanakuibia sana, tukio la kuibiwa na mteja wa guest lilipaswa kuwa last warning lisijirudie tena. Ilipaswa baada ya lile tukio ukienda hta chooni chukua hela zako zote na simu tia kwenye begi ndio ufunge...hyo shilabela naipata vizuri kuna wezi usipime.
 
Unaweza kusema sipo makini kwakua mazingira ya wizi hujayaelewa.

Ni hivi hapa nilipo Ni jumba la gest ambapo kwa mbele Ni flame na wezi hawakupitia mlangoni waliingia gest kama wateja then wakafanya mission yao ndani kwa ndani Sasa ulitaka niweje makini bro ? Yan hata mlinzi hakujua maana milango haikuvunjwa Wala nini.
 
Mm mbona nipo Geita na biashara zinaenda vzr tu mbona, hapo shilabela kuna jamaa zangu wanafanya vzr sana na biashara za nguo

Au ww umelazimishwa kufanya biashara ya mobile banking pekekeeee?
 
Unaweza kusema sipo makini kwakua mazingira ya wizi hujayaelewa.

Ni hivi hapa nilipo Ni jumba la gest ambapo kwa mbele Ni flame na wezi hawakupitia mlangoni waliingia gest kama wateja then wakafanya mission yao ndani kwa ndani Sasa ulitaka niweje makini bro ? Yan hata mlinzi hakujua maana milango haikuvunjwa Wala nini.
Baada ya hpo umesema uliibiwa tena baada ya kutoka kidogo ...hpo ndipo nimekuona haupo makini

Ninapoishi kumewahi kuwa na matukio ya wizi kila mara ilibidi kuchukua hatua za ziada ili nisiibiwe yaani nikienda kukojoa lazima nifunge mlango

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Naenda kununua vocha umbali wa mita mia, ulitaka nibebe sm zote kwenye kabati niende nazo mkuu pamoja na hela zote au ulitaka nifanye nini ili niwe makini.?

Maana Mimi niliona hapa Cha muhimu ni kuboresha kufuri Nikanunua kufuri "Yale" nikaimalisha ulinzi.
 
Back
Top Bottom