Executivesister
JF-Expert Member
- Aug 7, 2012
- 514
- 594
Uza kila kitu ila frame muachie mtu kwa muda aweke hela zake alafu hamia Dar, weka hela zako sehemu salama kama Bank, hakikisha wewe ni mcha Mungu kama unataka kutafuta pesa kweli mambo ya madem weka kando kidogo kwa muda, fikia kwa ndugu usimwambie umefuata nini na asijue una hela, ndugu zako unawajua mwenyewe, ukiwa Dar hakikisha una tembelea sehemu kama kariakoo, ilala Boma pale fika saa 12 asubuhi,tandika n.k,kazunguke hayo masoko 3 kwanza na mengine utayajulia huko.
Angalia nini kinapendwa huko Mkoani kwenu kwa kuwa tayari una mtaji Utajua cha kufanya, achana na biashara ya hlela, anza kuuza nguo za watoto za mtumba utapata ilala na tandika, za special utazipata kariakoo, au mashuka au nguo za wanawake, usijifanye mjuaji Dar na usimuamini mtu, hata kama mlikutana kijijini ukifika Dar huyo anaweza kuwa mtu mwingine kabisa. So unaweza Kuanza kusafirisha au ukakomaa kuuza hapo hapo Dar wenyeji watakuelekeza, usikimbilie kupanga nyumba hadi uujue mji vizuri.
Ukitaka kukaa kwa ndugu kwa amani ondoka alfajiri urudi jioni, ukirudi ukiingia bafuni fua nguo zako huko huko, Acha bafu safi, ukijipendekeza kubaki nyumbani utatumwa hadi ukome, hadi watoto utaachiwa uangalie, ishi kwa mahesabu. Nadhani ukisoma hapa utapata chochote.