Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Wakati mwingine uhitaji wa huduma za kisheria huja bila mtu kutarajia kama ilivyo kwa magonjwa au kifo vitu ambavyo huwekewa bima(bima ya afya na bima kwa ajili ya kifo) ukiacha mbali bima ya vyombo vya moto pale vinapopata ajali na bima nyinginezo.
Moja ya sababu ya kuwa na bima ni gharama ya huduma/tatizo husika kuwa kubwa huku huduma hiyo ikiwa ni muhimu na haikwepeki mfano maradhi/kuuguwa.
Binafsi, naona uhitaji wa kuwa na huduma ya bima ya afya kwa kiasi kikubwa unafanana sana na uhitaji wa kuwa na bima ya huduma za kisheria kutokana na umuhimu wa huduma yenyewe kwa jamii huku gharama zake zikiwa juu kuliko uwezo wa wananchi walio wengi kumudu gharama hizo na mfano ni gharama za kulipa mawakili.
Hivyo, nadhani ni busara tukafkiria kuwa na chombo(mfano National Legal Services Insurance Fund) kitakachohusika na utoaji wa bima za huduma za kisheria ambazo zitatolewa kwa mwanachama pale atapokumbana na matatizo yatayompelekea kuhitaji usaidizi wa huduma za kisheria iwe mahakamani au iwe ni katika kugharamia gharama za kupewa ushauri wa kisheria au vinginevyo.
Kitu hiki inawezekana hakipo si Tanzania pekee,bali duniani kote ila hii kwangu sio sababu ya kutofikiri kuwa na chombo cha aina hii kama ilivyo NHIF na nyinginezo.
Tujiulize,kama wafanyakazi wanakatwa mishahara yao kuchangia vyama vya wafanyakazi kwa matumaini kuwa vyama hivyo ndio mtetezi wao mfano siku mtumishi akipata matatizo kama ya kufukuzwa kazi,kusimamishwa kazi,n.k, ni kwanini tuone ni jambo la ajabu kuwa na bima ya huduma za kisheria wakati matukio ya watu kuhitaji huduma za kisheria ni mengi kuliko matukio ya wafanyakazi kuhitaji msaada wa vyama vyao kuwatetea wanapopata matatizo makazini?
Huduma hii inaweza kuwa ya hiari kwa mtu kuchangia kwa mwezi na siku akipata matatizo yanayopelekea kuhitaji msaada wa kisheria, basi chombo kitakachoundwa kitamgharamia iwe ni katika kumlipa wakili wa kumsimamia mahakamani au vinginevyo na hata kulipa gharama ya kesi ikiokea mwanachama ameshindwa kesi na kutakiwa kulipa gharama ya kesi.
Bima hii inaweza kuwekwa katika makundi kutokana na kiwango mtu anachochangia kwa maana ya bima ku-cover huduma za kisheria kulingana na kiwango mwanachama anachochangia.
Sheria itakayotumika kuanzisha chombo hiki pia iweke kanuni na mashariti ya kuzingatia katika utoaji wa huduma hii kama vile vigezo na mashariti ya kuangaliwa/kuzingatiwa kabla ya msaada wa kisheria kutolewa kwa mwananchama.
Faida ya kuanzisha chombo au taasisi kama hii, pamja na mambo mengine, itakuwa ni kutoa ajira kwa vijana na makundi ya watu wengine katika jamii watakaoweza kuajiriwa katika taasisi hii.
Kila jambo huanza na wazo na wazo ndio huleta jambo.