Kutokana na kelele nyingi, Simba haikuwa inacheza mpira aliokuwa anataka Robertinho

Kutokana na kelele nyingi, Simba haikuwa inacheza mpira aliokuwa anataka Robertinho

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Nakumbuka kuangalia clip moja ya Mwalimu Nyerere akisema "kama ilivyo kwa UKRISTO, dunia haijawahi kuufuata UJAMAA kwa asilimia 100" kwa maana hiyo ni ngumu au siyo sahihi kuhukumu kama mitazamo na mifumo hiyo ni sahihi au siyo wakati haijawahi kufuatwa kikamilifu.

Simba ya kipindi cha Juma Mgunda ilikuwa inacheza mpira wa back passes nyingi, alipokuja tu Robertinho na falsafa zake za direct football alishtua wengi maana back passes zilikoma ghafla ndiyo kelele zikaanza kuwa Simba inacheza mpira wa butua butua. Kutokana na shinikizo, ikabidi aruhusu sehemu ya mpira ambao watu walikuwa wanalilia lakini hapo unadili na mifumo miwili inayokinzana. Ukweli ni kuwa falsafa ya Robertinho haijawahi kuwa practiced pale Simba ukiacha gemu 2 au 3 za mwanzo toka alipokuja.

Leo hii mnapolialia kuwa Simba haina kasi, eti wachezaji wanacheza taratibu mno, mkumbuke huo ni ugonjwa ambao Robertinho alijaribu kuutibu lakini mkamkemea. Hili suala nimeliongelea sana siku za nyuma, pitia nyuzi hizi:

Post # 564 - FT: Simba 0-3 Raja Casablanca | CAF Champions League

Post # 9 - Ukweli kuhusu Simba Sports Club

Post # 364 - FT|| Horoya AC 1-0 Simba SC | CAF Champions League | Stade General Lansana Conte | 11.02.2023

Post # 21 - Jicho la tatu: Mgunda ndiyo mtu wa kwanza anayefaa kulaumiwa kwa matokeo mabovu Simba
 
Sihitaji amani,nipo tayari kwa Vita!
20231110_171832.jpg
 
Nakumbuka kuangalia clip moja ya Mwalimu Nyerere akisema "kama ilivyo ukristo na ujamaa, dunia haijawahi kufuata mifumo hiyo kwa asilimia 100" kwa maana hiyo ni ngumu au siyo sahihi kuhukumu kama mitazamo hiyo ni sahihi au siyo wakati haijawahi kufuatwa kikamilifu.

Simba ya kipindi cha Juma Mgunda ilikuwa inacheza mpira wa back passes nyingi alipokuja tu Robertinho na falsafa zake za direct football alishtua wengi maana back passes zilikoma ghafla ndiyo kelele zikaanza kuwa Simba inacheza mpira wa butua butua. Kutokana na shinikizo, ikabidi aruhusu sehemu ya mpira ambao watu walikuwa wanalilia urudi lakini hapo unadili na mifumo miwili inayopingana. Ukweli ni kuwa falsafa ya Robertinho haijawahi kuwa practiced pale Simba ukiacha gemu 2 au 3 za mwanzo toka alipokuja.

Leo hii mnapolialia kuwa Simba haina kasi, wachezaji wanacheza taratibu mno, mkumbuke huo ni ugonjwa ambao Robertinho alijaribu kuutibu lakini mkamkemea. Hili suala nimeliongelea sana siku za nyuma, pitia nyuzi hizi:

Post # 564 - FT: Simba 0-3 Raja Casablanca | CAF Champions League

Post # 9 - Ukweli kuhusu Simba Sports Club

Post # 364 - FT|| Horoya AC 1-0 Simba SC | CAF Champions League | Stade General Lansana Conte | 11.02.2023

Post # 21 - Jicho la tatu: Mgunda ndiyo mtu wa kwanza anayefaa kulaumiwa kwa matokeo mabovu Simba
Kila timu ina falsafa yake. Simba haikuitwa LUNYASI bila sababu. Barca inaweza cheza butua za Chelsea ya Mourhino Wakatalunya wakafurahi kisa inashinda?
 
Kila timu ina falsafa yake. Simba haikuitwa LUNYASI bila sababu. Barca inaweza cheza butua za Chelsea ya Mourhino Wakatalunya wakafurahi kisa inashinda?
Hiyo lunyasi imefanya tukaitwa mwakarobo na ili tutoke hapa kuna mambo inabidi yabadilike. Einstein aliwahi sema kurudia jambo hilo hilo na kutegemea matokeo tofauti ni ishara ya ukichaa.
 
Walisema kocha aingie kwenye mfumo wa Chama.....
Kipindi kile wanashindashinda, kwenye vijiwe na wachambuzi wa kibongo wakawa wanasema
" si unaona sasa, kocha kakubali kuingia kwenye mfumo wa chama, ona tunavoshinda kirahisi"

Tz ina wajuaji wengi sana, na inavoonekana kwenye ngazi za maamuzi wamejaa unprofessionals, uchebe aliwahi andika hili kipindi anaachana na simba. Inawezekana wanaowatia presha makocha ni watu wasio na uelewa na mpira.

Ni kama Singida BS, jinsi muhasibu wa taifa anavyompangia kikosi kocha.
 
Kumbe ndo hivyo
 
Back
Top Bottom